BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, April 20, 2010

HAPPY BIRTHDAY LUTHER VANDROS!!(RIP)

                                                    LUTHER VANDROSS
Anaitwa Luther Ronzoni Vandross ambaye alikuwa mkali wa kuogopwa wa muziki wa R&B,mtunzi na mtayarishaji pia,jamaa alizaliwa tarehe kama ya leo 20 April 1951,so kama wewe unasheherekea birthday yako leo fahamu kuwa una-share birthday na Star huyu.
Jamaa alipata nafasi ya kufanya albums zipatazo 9 ambazo ni (tarehe na mwezi ilipoingia kitaa kwenye mabano) "Never too Much"(01/02/1981),"The Best of Love"(01/02/1989),"Songs"(27/09/1994),"Your Secret Love"(01/10/1996),"One Night with you[the best of love]"(30/09/1997),"I know"(11/08/1998),"Super Hits"(22/08/2000),"Luther Vandross"(19/06/2001) na ya mwisho ambayo ni kali balaa inaitwa "Dance with my father"(10/06/2003).
Albums hizo zilipata nafasi ya kuuzwa zaidi ya nakala milioni 25 duniani kote na aliweza kulamba tuzo zinazoheshimika nane za Grammy.Rasmi alifariki July 01 2005.HAPPY BIRTHDAY&R.I.P Luther Ronzoni Vandross

0 comments: