BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, April 30, 2010

MNM'S ALBUM OF THE WEEK(Raymond Vs Raymond By Usher Raymond)

Hey!hey!Wadau na fans wa blog ya burudani,kwanza kabisa niombe radhi kidogo.Kwakweli wiki hii mambo ya mtandao naweza sema yamenichanganya sana,kuna mambo mengi sana nilipanga kukupatia mdau na fans wangu lakini mtandao uliniangusha sana,lakini sio ishu.Leo ni ijumaa tuangalie yale ya kiijumaa ijumaa zaidi au sio??KARIBU sasa katika ile segment yetu ya kila ijumaa "My album of the week".Baada ya wiki iliyopita kuwa na mchizi toka NAIJA leo narudi pande zilezile za mbele kupitia albums ambazo zinafanya vizuri sana kwa sasa,leo niko na mtu mzima USHER RAYMOND na kitu "Raymond Vs Raymond".

                       RAYMOND VS RAYMOND(FRONTFACE)

Hii ni albam ya sita ya mchizi ambayo imetumbukia kunako maduka 30st March kwa U.S.A,baada ya albam yake ya tano ya 2008 ya "Here I Stand" ambayo kwa wachambuzi wa masuala ya burudani kama mimi hivi tunaweza sema ilimbwela(ilishindwa kufanya vizuri),na hii ilitokana na kushindwa kabisa kuuza baada ya wiki mbili nzuri za mwanzo za kimauzo wakati albam hiyo inaingia sokoni,albam hiyo ilitanguliwa na "Confessions" ambayo iliuza kinoma,baadhi ya singles kutoka ndani ya "Confessions" ziliweza kushika no 1 karibu nusu nzima ya mwaka na kuvunja rekodi ya charts mbalimbali duniani.Lakini ilionekana kama ni self-confession ya Usher mwenyewe ambae kwa wakati huo alikuwa akishughulikia talaka ya aliyekuwa mkewe TAMEKA FOSTER.

                      RAYMOND VS RAYMOND(BACKFACE)

Mzigo umetoka LaFace Records na una jumla ya ngoma 14 za ukweli,mbili zizokwishaachiwa ni "Hey Dady(Dady's Hom)" feat;Plies na huu ambao duh! unasumbua sana saivi "OMG" feat;Will.I.am.Zingine ni "There goes my baby","Lil Freak"feat;Nicki Minaj,"She don't know"feat Ludacriss,"Mars Vs Venus","Pro Lover","Foolin' around","Papers","So many girls","Guilty"feat T.I,"Okay" na "Makin' love(into the night).

                           HERE I STAND(USHER RAYMOND)

Hope maelezo hayo yanatosha sana kukufanya uitafute albam hii na kutoa muda wako kuisikiliza pia au vipi,cha kuongeza tu ni kuwa hivi nnavyoipost hii ishu hapa kwenye blog ya burudani "Raymond Vs Raymond" iko katika nafasi ya tano ndani ya chat zinazoaminika za BILLBOARDS katika albam 200 bora za wiki hii.Asentiiii!!!!

0 comments: