BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, April 8, 2010

RACHEL K NA SHAVU ZITO KAMPALA.

Rachel Kiwanuka(Rachel K)
Mwanamuziki sexiest nchini Uganda Rachel Kiwanuka aka Rachel K amekula shavu lakutosha tu baada ya kusaini mkataba na kampuni moja ya kutengeneza soda nchini humo wa kuwa balozi wa soda hiyo.Habari zilizonifikia hivi punde zinasema kampuni hiyo ambayo nikiitaja nitakuwa naitangazia biashara bila kunilipa  imemchagua Rachel baada ya kuridhishwa na juhudi zake mbalimbali za kimuziki za mwanamuziki huyo anayenivutia hata mimi,Rachel amechaguliwa miongoni mwa wanamuziki kibao wa kike nchini humo wanaovutia kimaumbile na wanaofanya vizuri katika muziki pia.Rachel ambaye siku za nyuma alidaiwa "kutoka kikuchkuch hotae" na mwanamuziki mwingine wa kiume mwenye mvuto hasa nchini humo Moris Kirya na baadae wote wawili kukana anaungana na wakongwe wenye fwedha kama Bebe Cool,Bobby Wine na wengineo ambao wako katika mikataba minono kama mabalozi wa bidhaa na makampuni mbalimbali kitu ambacho kimekuwa kikinenepesha waleti zao zaidi ya kutegemea mauzo ya albums na shows.Bongo inakuwaje??Wasanii kama mmelala hivi??au mtazamo wangu tu??

0 comments: