BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 21, 2010

KIPINDI CHA PLANET BONGO EATV CHAPOTOSHA UMMA(Pt I)

             Wadau habari zenu,naamini hali zenu ni njema kabisa na ujenzi wa taifa unaendelea kama kawaida,leo nina mengi sana ya kuzungumza juu ya yale yaliyonikera,kama wiki tatu sasa nimekuwa karibu sana na kipindi cha PLANET BONGO cha EATV nikikifuatilia kwa ukaribu zaidi.Kwa wale wafuatiliaji wa kipindi hiki wiki hizi tatu kipindi kilikuwa kinarusha exclusive toka Mwanza(Rock City) pamoja na Arusha(A-Town).Kutokana na hilo nimepata nafasi ya kugundua kitu, kipindi ambacho mtangazaji wa PLANET BONGO Abdalah alikitengeneza Mwanza ni wakati alipopata nafasi ya kwenda kwenye show ya mwanamuziki wa Nigeria J-Martins iliyofanyika jijini humo hivi karibuni na kile kipindi cha Arusha hakukitengeneza yeye,bali alichukuwa kipindi ambacho kilitengenezwa na mtangazaji mwingine wa kituo hicho Bhoke Egina aliyekuwa anafanya kipindi cha 5 CONNECT wakati huo na kilikwishawahi kutumika kabla ndani ya kipindi hicho cha 5 CONNECT.

               Kilichonisukuma kuandika makala haya ni muendelezo ambao Abdalah aliufanya na kunitatiza,sijui idea hii aliipata wapi,napata shaka kuwa mtangazaji huyo halikuwa kusudio lake la kwanza kufanya hivyo wakati anatengeneza kipindi hicho,nadhani ni idea ambayo ilikuja katikati kabisa na inawezekana ilikuja wakati tayari sehemu ya kwanza ya Mwanza na ya pili ya Arusha imeshakwenda hewani,na kilichofanyika ni ”ilimradi” kipindi cha wiki ya tatu kipatikane ili wiki ipite,hii si dalili nzuri kwa crew nzima ya kipindi pamoja na mtangazaji huyo aliyepatikana toka katika mchakato mrefu na mgumu uliohusisha vijana zaidi ya 500 waliokuwa wakiiwania nafasi hiyo mwaka juzi.Kipindi cha PLANET BONGO cha wiki hii ya tatu kilifanywa kwa kulinganisha mikoa hii miwili iliyotumika kutengeneza vipindi vilivyopita(Mwanza na Arusha),kwamba wapi kuna muziki zaidi?Mwanza au Arusha?na wengi waliopata nafasi ya kuzungumza ni wafanyakazi wa EATV,nilipata nafasi ya kumtambua Dj Kim na maproducer wa vipindi mbalimbali vya kituo hicho,na wote walitoa tathmini kutokana na kile kilichofanywa katika vipindi vilivyopita.Yalizugumzwa mengi lakini mwisho wa siku aliyekuwa akitazama kipindi aliweza kupata matokeo japo hayakutangazwa,Arusha ilionekana INA MUZIKI zaidi ya Mwanza,chimbuko la muziki wa HIPHOP lilionekana Arusha.
                 Kuna mwanafalsafa mmoja alikwishawahi sema “NO RESEARCH,NO RIGHT TO SAY” akiwa na maana “BILA TAFITI,HAKUNA HAKI YA KUSEMA”,kitu ambacho crew ya kipindi cha PLANET BONGO imekifanya,crew hiyo imesema bila kufanya utafiti wa kutosha,binafsi sidhani kama hawa jamaa walikuwa na haki ya kulinganisha kimuziki mikoa hiyo miwili kwa kutumia “tuvipindi huto tuwili” walitotutengeneza.Mimi ni mwenyeji wa Mwanza,nimezaliwa Mwanza,nimekulia Mwanza,kwahiyo Mwanza naijua vizuri na muziki wa Mwanza naujua vizuri sana(hakuna anayeweza kunidanganya).Binafsi nimekuwa mdau wa muziki Mwanza tangu napata akili za kiutu uzima,nimefanya kazi kama mtangazaji wa redio zaidi ya moja kanda ya ziwa na nimekuwa niki-deal na muziki huo kanda ya ziwa kwa zaidi ya miaka nane, ndo maana nimeamua kuzungumza haya,naamini Mwanza kuna MUZIKI zaidi ya kokote TANZANIA hii,utafiti huo nimekwisha ufanya japo si utafiti rasmi,nina utetezi na sababu nyingi na za msingi za kusema hivyo,naomba nianze kutoa utetezi wangu kwanza kutoka katika vipindi hivyo vya PLANET BONGO vilivyorushwa.

10 comments:

Unknown said...

Tumekusoma Kaka,unaonaje km ungedondosha sababu kadhaa japo kwa dondoo tu, ili asiyejua kitu kabisa apate japo mwanga..?

Anonymous said...

Kumbe shida yako ni Arusha kusemwa n muziku mzuri zaidi ya mwanza.Hahahahaa,huna mpya

RENATUS KILUVIA said...

Thanx kwa comments,i need mo and mo!!

Anonymous said...

kija arusha kulikua na radio kabla ya mwanza ilikua ianitwa URS MWAKA 1993 sema ilikua haisikiki nje ya mkoa na x plastaz sio wakongwe ila wewe ndo unajua ni wakongwe wa arusha kaaa chini uandike vitu vya akili lasivyo wewe na blog yako mtaonekana hamna la maana lolote

Anonymous said...

Anonymous no 4 nenda TCRA kaombe kitabu cha orodha ya radio stations na mwaka zilizoanzishwa usome vzr,redio ya kwanza ni Sauti ya Injili Moshi mwaka 1993,then radio One Dar halafu Radio Free Africa Mwanza,huyu jamaa yuko right.

Anonymous said...

Yani watoto wa ARACHUGA wabishi kishenzi hlf data hawana! We anonymous 4 soma tena hii makala,Mr Renatus kaweka data hajabishana tu,amekuwa very critical,soma tena makala,sio kwamba anatafuta umaarufu lazima ukubali jamaa ni kichwa kwa jinsi makala inavyosomeka,me nampa Big up sana and Kip it up mtu mzima!...READING UK

Anonymous said...

Tatizo nimeliona,watoto wa siku hizi wagumu kuelewa sana,sijui sababu ni nini,sijui bangi?hawajamuekewa jamaa,wanakalia kubisha tu,hiki kizazi cha bongo fleva bwana tabu tupu,na ndio maana hata shuleni mnafeli,kusoma hamtaki mnakalia yo wosup!yo wosup!someni vizuri hiyo makala halafu mjibu kwa hoja na data zilizokamili,sio kelele kelele tu na ujiko usiokuwa na lolote.Mdau London UK.

Anonymous said...

kija hujui mziki vzuri japo pale lake ulikua unafwata maadili ya mziki vzuri lakin saiv upo dar ushaanza uswahili kaka

RENATUS KILUVIA said...

Teh!teh!teh!akhsante kwa kunifuatilia kwa ukaribu mshkaji wangu,naamini unanifahamu vizuri japo hujajitambulisha ili nami nikufahamu,ila lengo langu lilikuwa ni kuanzisha MJADALA na si kushindana ili kufahamu nani anajua muziki vzr na nani hajui,pengine wewe labda unajua zaidi yangu au zaidi ya wengi ila hujajitokeza,so take trouble tufahamishe wadau na fans wa MNM Blog,hii si blog yangu,ni blog yetu sote,tuitumie,mimi kama runner wa blog nakaribisha mawazo ya mtu yeyote,tatizo letu wabongo tuko fasta sana katika kuongea ila ni wavivu wa kufikiri na kupresent kitu on paper na ndio maana watu weupe wametuzidi kwa kila kitu,fanya hivi andika artical yako ukii-critisize hii halafu nitumie ktk mail zangu,mimi nitaitundika hapa bure bila gharama yoyote,angalizo muhimu ni kwamba isiwe ni ya matusi au kumvunjia mtu yeyote heshima(defamation) ili tusiiharibu blog yetu au vipi??asante kwa comments na kutoa muda wako kupita MNM.Shukrani.

Anonymous said...

haina noma kija ila punguza ushabiki halafu always focus kwenye reality blog itakua poa ila ukianza leta individualism ni sooooo