BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 7, 2010

MNM's ALBUM OF THE WEEK(RISE UP By CYPRESS HILL)

Its a very good day,furahi-day(friday),naamni uko poa sana mdau na fans wa MNM Blog,leo kama kawa kama dawa tunakutana katika MNM's album of the week,kila ijumaa huwa nakuletea album moja kali na kukupa maelekezo kidogo khs album hiyo,kama vipi uitafute na kuiweka katika maktaba ili ijae mizigo mikali,wiki iliyopita nilikuletea "Raymond Vs Raymond" ya Usher Raymond,leo niko na watu wa HipHop zaidi,album inaitwa "Rise Up" ya Cypress Hill.


RISE'UP(COVER ALBUM)

Hawa jamaa wanagonga shughuli zao Los Angeles,na ni kundi linaloundwa na washkaji watatu ambao ni B-Real,Sen Dog na producer wao Dj Muggs,wamekuwa katika maisha ya ghetto na kujihusisha zaidi na biashara za dawa za kulevya kabla hawajajitumbukiza katika muziki,na Cypress Hill ndio wana-HipHop wa kwanza kukubalika na kutangaza Spanish HipHop.


CYPRESS HILL

"Rise Up" ni album yao ya kwanza chini ya uongozi wa Snoop Dogg ndani ya "Priority Records",ngoma "rise up" ambayo ndio imebeba jina la albam hii imetengenezwa na producer Tom Morello wa Rage Against the Machine Fame na zaidi unazungumzia watu kusimama imara na kupigania kile wanachokiamini.


CYPRESS HILL(1991 ALBUM)

Kabla ya album hii machizi wameshaachia albums zingine kibao tu,ndani ya "rise up" kuna ngomaz kali kumi na tano ambazo ni "It Ain't Nothing" Feat;Young De(wa huko), "Light it Up", "Rise Up" Feat;Tom Morello, "Get it Anyway", "Pass the Datch" Feat; Evidence&Alchemist, "BangBang", "K.U.S.H", "Get Em Up" na zingine kibao.


CYPRESS HILL(IV ALBUM)

Tukirudi kwenye Billboards Top 200 albums "Rise Up" ya Cypress Hill iko nafasi ya sabini na nne(74) na inazidi kupanda kadri muda unavyozidi kwenda,so hawa ndio Cypress Hill bwana kama unawafeel hebu wasapoti kwa kutafuta albam yao hii halafu uone kunani ndani,poaaaaaaa!!!!!!

0 comments: