BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Wednesday, May 12, 2010

MSHAHARA WA HASHEEM THABEET HUU HAPA.

HASHEEM THABEET MANKA
Jana mdau wakati niko njiani natoka zangu ofisini nikawa nasikiliza "Jahazi" la Cap. Gadna na mzee wa "kama pundaaaa!!" Kibonde,hapo nikapata bahati ya kusikiliza mahojiano ya mcheza kikapu mtanzania ndani ya NBA Hasheem Thabeet Manka,yalikuwa mahojiano ya kibiashara zaidi kama ambavyo Gadna mwenyewe alivyoyatambulisha,yalizungumzwa mengi lakini kati ya yote moja tu ndo lililonishtua kidogo,ni MSHAHARA wa jamaa.Hasheem analipwa na Merphis Grizzlies pesa za kitanzania zaidi ya milioni 190 kwa wiki,ambapo ukipiga kwa hesabu ya harakaharaka ni zaidi ya milioni 450 kwa mwezi,na hiyo ni mbali na marupurupu mengine ikiwa ni pamoja na kulipiwa mishahara ya wasaidizi wake wa karibu na gharama zote za mazoezi na chakula,kitu pekee ambacho jamaa anakifanya toka katika package yake hiyo ni malipo ya nyumba anayoishi huko Marekani.Sasa hapo ndo nikagundua kumbe hata ile Vogue aliyomnunulia mamake ni mshahara wake wa wiki moja na nusu tu.Safi sana Hasheem,we Tanzanians are very proud of you dude,keep it up,tuko pamoja.

0 comments: