BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Monday, May 17, 2010

SOMO ZAIDI LINAHITAJIKA KWA WASANII WETU JUU YA HIZI TUNZO.

ALI KIBA
                                                       
Nimesikitika sana kwakweli na kujiuliza mengi sana,hivi sanaa yetu ya muziki inakwenda wapi jamani??Kama wasanii wetu ndio hawa ambao vichwa vyao ni kama vina mtindio ya ubongo??Mdau weekend hii iliyopita Tanzania yetu ilikuwa na tukio la kihistoria hasa kwa upande wa sanaa hii ya muziki,Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010,ni tukio ambalo kila mpenda burudani alikuwa karibu kuweza kujua kipi ni kipi upande huo na tumeshuhudia mengi,wa kuboronga ukumbini tumewaona na mapungufu yaliyosalia kwa waandaaji wa tuzo tumeyaona pia,leo sitaki kuzungumzia sana juu ya yale ambayo nilipata nafasi ya kuyazungumza kwenye kipindi cha "tupo pamoja" cha TTV kabla ya tunzo zenyewe,leo naomba nizungumze juu ya maoni mbalimbali ya wasanii au wanamuziki wenyewe baada ya tunzo hasa wale waliokuwa katika vipengere(categories) mbalimbali ndani ya tunzo hizi,nimewasikia wengi,lakini mimi naona waandaaji wa tunzo hizi(TBL) katika miaka ijayo wajitahidi kutoa semina juu ya wasanii kukubali matokeo yoyote yatakayopatikana baada ya tunzo zenyewe.Mi naona wasanii wetu wengi hawana upeo kabisa juu ya mambo haya ya tunzo,msanii wa kibongo akishaingizwa kwenye category yoyote tayari anajiona keshachukuwa tunzo,hakumbuki kwamba huu ni ushindani wa yeye na wenzake kibao ambao pia wako katika category hiyo na kati yao wote yeyote anaweza kuchukuwa tunzo hiyo,inapotokea yeye asichukuwe basi inakuwa lawama mtindo mmoja na kutishia kujitoa katika tunzo za miaka inayokuja kitu ambacho mimi naona sio dawa,halafu kitu kingine msanii anatazama jina lake zaidi ya ni nini kilichomfanya aingie katika category fulani,eti kwa sababu yeye ni msanii mwenye kijina kidogo kimuziki  basi anataka abebe tunzo zote hata zile ambazo kiukweli ni ngumu kwake kubeba kwa mwaka huo.Mfano naomba nimzungumzie Ali Kiba,nimepata bahati ya kumsikia akihojiwa sehemu fulani akiziponda tunzo na kudai kuwa eti yeye alistahili kuchukua na anashangaa kwanini hajachukua.Ali Kiba alikuwa katika category mbili ambazo ni msanii bora wa kiume wa mwaka na wimbo wake wa "usiniseme" uliingia kwenye category ya wimbo bora wa afro pop.Sasa kimatokeo ni kwamba msanii bora wa kiume wa mwaka alichukua Banana Zorro ambaye kiukweli alistahili tunzo hiyo,Banana kwa mwaka mzima wa 2009 amesimama vizuri kimuziki na hakuna anayeweza kubisha katika hilo,Banana ni mwanamuziki ambaye kwa sasa haimbi kwa playback,anaimba live na anamiliki bendi yake mwenyewe ambapo anatumbuiza sehemu mbalimbali kila weekend,lakini pia Banana mwaka jana ameweza kuhit vizuri na wimbo wake "zoba" sambasamba na B-Band,sidhani kama kweli Ali Kiba alitegemea kumpiku mtu kama Banana katika category hiyo,Ali Kiba bado anaimba kwa kutumia Cd na kupiga vishoo vidogovidogo kwenye sebule za watanzania waishio ulaya na hicho tu si kigezo cha kumfanya awe msanii bora wa kiume wa mwaka.Ushindi wa category ya pili aliyowekwa Ali Kiba ulikwenda kwa wimbo wa Marlow "PiiPii",wimbo ambao hauna ubishi kabisa kustahili kuchukua tunzo hiyo,kwa kudhihirisha hilo basi tunzo hii si tunzo ya kwanza kwa wimbo huo ni tunzo ya pili,ya kwanza ilipatikana toka Kenya,sasa Ali Kiba alitegemea kweli "usiniseme" umfanye yeye achukuwe tunzo hiyo??ni habari ya kuchekesha kidogo,wimbo wenyewe una video mbovu mwanzo mwisho,na video hiyo ilipata airtime sababu yeye ni Ali Kiba na si kingine,na tukizungumzia hit,wimbo wenyewe hauku-hit kivile kama ulivyokuwa "PiiPii" wa Marlow zaidi ya kuhit'ishwa kilazima na wanaojua promo.Kutokana na hilo basi mi naona msanii kama Ali Kiba na wengine wenye vichwa vigumu wanatakiwa wapewe darasa kabla ya kilele cha tunzo zenyewe ili wasizungumze "utumbo" wao wanaouzungumza hivi sasa,kuna mifano mingi lakini kutokana na muda naomba niishie hapa ili mengine mengi wayazungumze wenzangu wanaokerwa na ishu ka' hizi,chiaooo!!!!

0 comments: