BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, June 3, 2010

A NEW RADIO SOAP..."DETOUR OF REAL LOVE"

CHARACTERS WA DETOUR OF REAL LOVE

"Detour of Real Love" ama "Njia Ndefu ya Penzi la Dhati" ni tamthilia mpya ya radio ambayo imeandaliwa kwa ufundi mkubwa ili kuwapa burudani wapenzi wa tamthilia za radio wenye hamu ya kupata drama yenye mfumo wa filamu kupitia radio.Tamthilia hii ya ukweli inamhusisha kijana handsome aitwaye Ian ambaye anapata mkate wake wa kila siku kwa shughuli ya ukonda wa daladala. Katika kazi zake za kila siku anakutana na dada mrembo, msomi na mtoto wa tajiri aitwaye Rachel ambaye anapanda daladala hiyo akiwa na mpenzi wake Erick ambao wanasoma chuo kikuu. Upole, werevu na mvuto alionao Ian unampagawisha Rachel na kumfanya afanye kila aliwezalo kumpata kijana huyo bila kujali tofauti zao za maisha. Baada ya Erick kunyang'anywa mpenzi wake na konda Ian, anaamua kulipiza kisasi kwa kuwawinda wapenzi hao wapya. Furaha fupi na ahadi aliyoipata Ian kwa kupendwa na Rachel inadumu kwa muda mfupi na kuyaona maisha kama jehanamu. Fuatilia tamthilia hii kila siku za jumatatu saa tano usiku na kurudiwa jumatano muda kama huo."Detour of Real Love" imeandikwa na mwandishi anayekuja juu Tanzania aitwaye Victor Chuma na kutayarishwa na Fredrick "Skywalker" Bundala. Muziki katika tamthilia hiyo umetayarishwa na Skywalker na Amba producer kutoka Iringa.

0 comments: