BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, June 24, 2010

OLD SKOOL.........."SALT 'N' PEPA....

SALT N PEPA

Hope utakuwa unawakumbuka halafu kama una-wish warudi vile,kama ni hivyo basi uko ka' mimi,leo nimesikia ngoma yao moja "lets talk about sex" duh!!nikakumbuka mbali sana,ni SALT N PEPA,kundi lililokuwa linaundwa na akina dada wawili na Dj wao mmoja(mwanadada pia),so jumla walikuwa watatu,Cheryl "Salt" Wray,Sandra "Pepa" Denton na Deidra Roper aka Dj Spinderella ambaye alijiunga baadae na kuchukuwa nafasi ya dj wao wa kwanza kabisa Latoya Hanson,kundi lilifanya kazi kuanzia mwaka 1985 mpaka 2002,zaidi walifanya muziki wa Hiphop na dance na makazi yalikuwa ni katika kitongoji cha Queens New York City.Lebel walizofanya nazo kazi ni Next Plateau,London/Polygram na Red Ant Entertainment.

SALT N PEPA

Singo yao ya kwanza ilikuwa ni "Super Nature" na baadae mwaka huohuo 1985 wakatoa tena "The Showstopper" ambayo ilitumika kama soundtrack katika movie "Revenge of the Neds",kiukweli hii ni single iliyowaonesha njia sana baada ya kuchezwa sana katika vipindi mbalimbali vya redio zilizokuwa zikicheza sana muziki wa rap wakati huo na kuifanya kuwa hit ile mbaya.Albam yao ya kwanza ni "Hot,Cool & Vicious ya mwaka 1986,mwaka 1988 wakaachia "A Salt with a Deadly Pepa",mwaka 1993 ikaja "Very Necessary" baada ya hapo wakaparaganyika halafu wakarudi tena mwaka 1997 na mzigo "Brand New",mwaka 2000 wakashusha "Salt N Pepa:The Best of",rasmi Salt N Pepa ikafa 2002.Wako wapi sasa???sikia hii.....Pepa(Sandra) aliolewa na Treach wa Naught By Nature July 27 1999 na wakatalikiana July 31 2001,mwaka 2008 akatoa kitabu "Lets Talk About Pep" ambacho humo aliizungumzia Salt N Pepa na kupanda na kushuka kwake kimuziki,aliuza sana.Salt(Cheryl) yeye alisema kabisa kuwa muziki hana hamu nao tena na hatakuja kujihusisha tena na masuala ya muziki katika maisha yake yote yaliobakia,sasa anafanya shughuli zake mwenyewe.Deidra ni mtangazaji wa redio moja inaitwa KKBT 100.3 fm L.A na show anayopiga inaitwa "The Backspin" na Dj Mo'Dav,pia anagonga ngoma katika clubs mbalimbali hapo L.A.Unaonaaa!!!

0 comments: