BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, July 2, 2010

"MTAMBUE HUYU".....THE LATE LYNDEN DAVID HALL

Jamaa alizaliwa May 7 1974 Wandsworth,South London,ni mwanamuziki aliyekuwa anafanya muziki wa Soul na Neo-Soul,lakini pia alikuwa mwandishi na mtayarishaji muziki(producer).Maelezo ya huyu mchizi sio marefu sana,mwaka 1999 Hall alikuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka U.K kupigiwa kura nyingi na kupata Best Male Artist,tunzo ambayo hutolewa na "Britain's Blues & Soul" magazine,mzigo wake wa kwanza "Medicine 4 my Pain" wa mwaka 1997 na mikono miwili mikali kutoka humo ndani "Do I qualify" na "Sex Cinderella" ilisumbua vibaya-vibaya na kujizolea mashabiki lukuki sio U.K tu bali dunia nzima.Naweza sema ndio mikono iliyonifanya hata mimi pia nikamfahamu huyu mchizi.

THE OTHER SIDE(ALBUM)

Mwaka 2000 Hall akaachia mzigo mwingine "The Other Side" ambamo ndani yake kulikuwa na mikono kibao tu iliyoshika na kusumbua mno.


LYNDEN DAVID HALL

Mwaka 2003 akatokea katika movie "Love Actually" ambayo ilichezwa na Keira Knightley na Chiwetei Ejiofor,humo ndani Hall aliimba katika harusi(ya kifilamu) ya mastaa hao,miaka miwili baadae akaachia albam yake ya tatu na ya mwisho "In Between Jobs" chini ya record lebel yake mwenyewe "Random Records",pia ni albam iliyoonesha mafanikio sana kwake japo naweza sema Lynden David Hall hakupata nafasi ya kuyafaidi mafanikio hayo,coz mwaka huohuo alianza kuugua sana kutokana na "cell transplant" alizowekewa Jan ya 2005,Lynden David Hall alipata ugonjwa wa "Hodgkin's Lympoma" Octoba mwaka 2003.14 Feb 2006 Lynden David Hall akafariki dunia mikononi mwa mkewe mpendwa Nikkie Hall,alifariki akiwa na miaka 31 tu.

MEDICINE 4 MY PAIN(ALBUM)

Muda mfupi kabla ya kifo chake akiwa hospitalini David Hall na mkewe walifanya tamasha lenye mafanikio(Lynden Wish Concert) ambalo lilifanyika London Jazz Cafe kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasaidia wenye matatizo,tamasha ambalo kwa mara ya kwanza liliwakusanya wanamuziki wote weusi nchini humo kwa ajili ya kuchangia fedha hizo ambazo pia zilitengeneza kitu kinaitwa "Lynden Wish Charity" ambayo iko mpaka kesho.May 23 2006 The African Leukaemia Trust waka-organize kumbukumbu ya kumkumbuka Lynden David Hall ambayo ilifanyika The Kensington Roof Gardens ambayo wanamuziki kibao wali-perfom,London Community Gospel Choir wakaimba wimbo "All You Need is Love" ambao David Hall aliuimba katika "Love Actually" movie,wimbo ambao uliwatoa wengi waliohudhuria machozi,Huyu ndie Marehemu Lynden David Hall,mtambue sasa...

0 comments: