BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, August 6, 2010

MNM'S ALBUM OF THE WEEK.."ELEMENT OF FREEDOM" By ALICIA KEYS"

ELEMENT OF FREEDOM(COVER)

Huu ni mzigo wa nne wa Alicia Keys Dean ambao uliachiwa rasmi Dec 11 2009 chini ya MBK na J Records..mzigo ulirekodiwa kuanzia May mpaka Sept 2009 ndani ya The Oven Studios pale Long Island, New York US..producers waliohusika ni pamoja na Alicia Keys mwenyewe, Jeff Bhasker, Swizz Beatz, Noah "40" Shebib na Kerry "Krucial" Brothers.Mdau mzigo huu ni noma..ni mkali balaa coz umekwenda mpaka nafasi ya pili kwenye US Billboard 200 Chart na kuuzwa zaidi ya nakala 417,000 wiki yake ya kwanza tu kitaa..

SWIZZ & ALICIA(LOV GON' GUD)

Kihistoria hii ndo albam yake ya kwanza kuuza kiasi hiki US na UK ..baada ya mwezi wa kwanza tu ukatukiwa platinum na RIAA japokuwa style ya Alicia ya kuimbia key ya chini(low key style) pamoja na uandishi wake ni vitu ambavyo vimekuwa vikisababisha mauzo yasiyoridhisha ya albams zake zilizopita..hii imekuwa tofauti kabisa..na mpaka June 8 2010 mzigo ulikuwa tayari umeshagongwa nakala 1,305,000 kwa Marekani tu.Mwenyewe alisema "nimetengeneza albam hii baada ya kupitia mengi magumu...ni kama kuondokana na mgandamizo wa moyo,najisikia huru sasa"..Singles zilizotangulia ni "Doesn't Mean Anything" ambao uliachiwa Sept 22 2009, "Try Sleeping With a Broken Heart" Nov 17 2009, "Empire State of Mind" pt II Feb 22 2010, "Un-Thinkable(Am Ready)" May 22 2010 na baadae ni "Put it in a Love Song" ambao utaachiwa mwezi ujao...

SWIZZ & MASHONDA(LOV GON' BAD)

Sasa check mikono iliyomo humo ndani..."The Element Of Freedom (Intro)", "Love Is Blind", "Doesn’t Mean Anything", "Try Sleeping With A Broken Heart", "Wait Til They See My Smile", "That’s How Strong My Love Is", "Unthinkable (I’m Ready)", "Love Is My Disease", "Like The Sea", "Put It In A Love Song" Feat. Beyonce, "This Bed", "Distance And Time", "How It Feels To Fly" na "Empire State Of Mind (Part II)"...Kama bado unasuasua kuutafuta na kuusikiliza mzigo huu...pole sana ndugu yangu.


0 comments: