BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, April 9, 2010

MY ALBUM OF THE WEEK(BATTLE OF THE SEXES by LUDACRIS)

Wadau na fans wa blog ya burudani(muziki na maisha) kuanzia ijumaa ya leo nitakuwa nakuletea "my album of the week",hapa nitakuwa nakuletea uchambuzi kiduchu wa albumz mbalimbali za hapa nyumbani na za mbele pia kila ijumaa ili kama vipi nawe unenepeshe maktaba yako ndogo nyumbani,mapumziko ya weekend uyatumie kusikiliza kwa makini sana albam hiyo.Leo nakuja na mzigo mzito na mpya kabisa wa mtu mzima LUDACRIS unaitwa "BATTLE OF THE SEXES"

Hii ni sura ya mbele ya cover album ya  "Battle of the Sexes" ya Luda.
Na hii ni sura ya nyuma ya albam hii ambayo "bado mupya" kabisa,imeingia kitaa rasmi March 9 na ndani kuna "mikono" kumi na nne iliyojaa kiukweli,hit mbili tayari ziko on air na zinaharibu sana utaratibu pande hizo,nazo ni "My Chick Bad(feat Nicki Minaj)" na "How Low",zingine zilizoko ndani ni "Everybody Drunk(feat Lil Scrapy)","I do it all night(feat Shawna)","Sex Room(feat Trey Songs)","I Kno Yu got a Man(feat Flo-Rider)","Hey Ho(feat Lil Kim&Lil Fate)" na "Party No Mo(feat Gucci Mane)".Zingine ni "Can't live with Yu(feat Monica)","Feeling so Sexy(feat Shawna)",'Tell Mi a Secret(feat Neyo)","My Chick Bad rmx(feat Dimond,Trina&Eve)" na "Sexting".Mzigo wote umefanywa na wapishi kibao wakali kama Pharell Williams wa The Neptunes,SwizBits,Gaggie,The Runners,Bangladesh,Infinity,Dj Montay,T-Minus na wengine kibao.Kwa taarifa yako mpaka ijumaa ya leo "Battle of the sexes" iko nafasi ya kwanza katika Billibords Top 200 albums,so?? ndo hivyo kama vipi ruka nayo weekend hii iwe pooooaaaa kama yangu itakavyokuwa,chiaoooooo!!!!WEEKEND NJEMA!!!

WAMEFANANA KWELI??AU MACHO YANGU TU!

                                                 Justine Timberlake
                                                    Robin Thickel
Wadau kuna mtu aliniambia kuwa anawafananisha sana hawa jamaa,kwa sura,wanavyovaa na kuimba pia.Ikabidi niingie kazini kulichunguza hili,duh nikaja gundua kuwa kuna ukweli ndani yake,Justine Timberlake na Robin Thickle ni kama brothers hivi?(sina maana ya ndugu).Sasa hebu nawe tuambie basi unawaonaje?ni kweli wanashabihiana au macho yetu tu,labda wengine tuna makengeza teh!teh!teh!teh!

Thursday, April 8, 2010

DNA KWELI UMEOKOKA??AU .........

DnA(kwenye Banjuka Ogopa video)
Mwanamuziki toka Kenya aliyeishtua East Afrika kwa hit "Banjuka" DNA(Dreams And Ambition) ameokoka,kiukweli ni habari njema sana kwangu,na ni habari niliyoifurahia mno,lakini namuuliza DNA "kaka umeokoka kweli?na umeamua kabisa kuachana na kila cha dunia hii?"Najua utajiuliza sana mdau wangu kwanini nimeuliza maswali hayo,sababu ni kwamba,stars wengi wamekuwa wakitangaza kuachana na kila kitu na kuokoka lakini baada ya muda mfupi tumeshuhudia wakirudi dhambini,ni kwanini?sio hapa East Afrika tu,hata Ulaya na Marekani tumeshuhudia hayo,mifano ipo mingi sana,sasa narudia tena DNA kweli umeokoka??hutatuangusha??Wadau na mashabiki wako tupo pamoja nawe na tutakuombea kwa nguvu zote kuhakikisha hurudi nyuma.DNA sasa ametoka na mzigo mkali unaitwa "mtoto wa SONKO"(mtoto wa MUNGU)akiwashirikisha waimba injili maarufu nchini humo Kambua na Issac Kahurah,mzigo ni mkono wa ULOPA na tunamtakia mafanikio katika maisha yake mazuri ya wokovu.

RACHEL K NA SHAVU ZITO KAMPALA.

Rachel Kiwanuka(Rachel K)
Mwanamuziki sexiest nchini Uganda Rachel Kiwanuka aka Rachel K amekula shavu lakutosha tu baada ya kusaini mkataba na kampuni moja ya kutengeneza soda nchini humo wa kuwa balozi wa soda hiyo.Habari zilizonifikia hivi punde zinasema kampuni hiyo ambayo nikiitaja nitakuwa naitangazia biashara bila kunilipa  imemchagua Rachel baada ya kuridhishwa na juhudi zake mbalimbali za kimuziki za mwanamuziki huyo anayenivutia hata mimi,Rachel amechaguliwa miongoni mwa wanamuziki kibao wa kike nchini humo wanaovutia kimaumbile na wanaofanya vizuri katika muziki pia.Rachel ambaye siku za nyuma alidaiwa "kutoka kikuchkuch hotae" na mwanamuziki mwingine wa kiume mwenye mvuto hasa nchini humo Moris Kirya na baadae wote wawili kukana anaungana na wakongwe wenye fwedha kama Bebe Cool,Bobby Wine na wengineo ambao wako katika mikataba minono kama mabalozi wa bidhaa na makampuni mbalimbali kitu ambacho kimekuwa kikinenepesha waleti zao zaidi ya kutegemea mauzo ya albums na shows.Bongo inakuwaje??Wasanii kama mmelala hivi??au mtazamo wangu tu??

UNAMJUA HUYU??STAY TUNED HABARI ZAKE ZINAKUJA.

PROKID(Heads&Tales cover album)

Tuesday, April 6, 2010

HONGERA LIBERATUS MUSIBA!!!


Hongera mshikaji wangu wa longtime na kufa na kuzikana Liberatus Musiba aka Odele aka Baba Nyambela kwa kutuletea mtoto mzuri wa kike aitwae Nyambela,mimi nimefurahi sana kwakweli kwa 7bu imekuwa surprise kwetu wengi,lakini kwanini hukutaka kutuambia kuwa mkeo mpendwa Junko Kato ni mjamzito??naamini ulitaka kufanya surprise na kweli umefanikiwa,mimi sina mengi kwakweli ila kukupongeza na kukukaribisha katika ulimwengu huu wa "kuitwa baba",wenzako tulishakutangulia muda kidogo,nawatakia furaha njema wewe na familia yako yote huko Tokyo Japan,msalimie mkeo Junko na "mgeni wetu" Nyambela.

THE PLAYER IS BACK!!!

Tiger Woods

Jana katika pitapita zangu kwenye channels za Tv nikagumiana na hii bana,jamaa ambaye miezi kama mitano hivi iliyopita aliuza sana magazeti huko pande za Obama kwa kashfa ya "uplayer"(kutoka na wanawake kibao) star wa gofu Tiger Woods alikuwa live BBC akizungumza na waandishi wa habari.Kikubwa ambacho mshikaji alikuwa anazungumza ni kuhusu ishu yake hiyo."napenda kuomba msamaha kwa fans wangu wote kwa yote yaliyotokea,kiukweli nimekosea sana na imekuwa ni kama funzo kwangu,na tayari yamepita,sitaki kuyapa nafasi tena,kwa sasa natazama zaidi yajayo na naahidi nimejirekebisha na hamtasikia tena chochote kibaya kutoka kwangu,nilikuwa na wakati mgumu sana lakini namshukuru MUNGU yamepita"alisema.Wadau hii ni baada ya miezi mitano ya kutokuzungumza chochote kuhusu kashfa yake hiyo na hajaweka wazi nini anatarajia kufanya juu ya kuparaganyika kwa familia yake kulikotokana na kashfa hiyo,hebu mimi na wewe tutupie macho na masikio yetu pande hizo tuone....

HAPA NAVIO,HAPA TIMBERLAND DUH!!

Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba mchizi kutoka Kampala anakwenda kwa jina la Daniel Kigozi aka NAVIO amekula shavu kufanya ngoma na producer na rapper kutoka nchini Marekani Timberland.Navio ambae yuko kwenye lebo ya Talent 256 anasema sasa ndoto zake zinatimia coz amehustle kwa muda mrefu sana kufanya kazi na star yeyote toka mbele,nadhani hii ndo nafasi ya jamaa kutoka kimataifa,hebu tumsikilizie au vp....

POLENI KWA BATA NDEFU!!!

         Poleni kwa bata ndefu wadau na fans wangu wote wa blog ya burudani,kiukweli ndugu zangu Pasaka kwangu ilikuwa njema sana,na namshukuru MUNGU kwa Pasaka njema,naamini kwako pia ilikuwa njema,Pasaka kwakweli wadau mimi binafsi sikupata nafasi ya kutoka kwenda popote zaidi ya ibada tatu nilizopata nafasi ya kuhudhuria,nilipata nafasi ya kuhudhuria ibada ya Pasaka jumamosi ya mkesha wa Pasaka usiku kwenye Kanisa Katoliki Dayosisi ya Manzese Uzuri,nikashuhudia igizo maalum la pasaka,kiukweli niliienjoy sana,jumapili pia nikahudhuria ibada ya pili palepale kanisani,baada ya ibada nikatulia nyumbani nikicheki muvi za hapa na pale mpaka siku ikaisha,jumatatu ya jana nilihudhuria pia ibada ya pili palepale kanisani kwetu Manzese na baada ya hapo nikajongea zangu kazini kama kawa,so pasaka ilikuwa kama hivyo,hebu nawe pia nijuze unambie pasaka yako ilikuwaje???ukishindwa kucomment nicheki katika bizzo4shizzo@ymail.com