BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, April 23, 2010

NEXT WEEK ON www.muzikinamaisha.blogspot.com

Kama ujuavyo fans wangu,leo ni ijumaa,siku ya "kufunga shule" kama kawa,hii ina maana kukutana tena hapa ni mpaka j3 ya wiki ijayo,wiki ijayo naamini itakuwa wiki njema sana kwetu sote koz ni wiki ya mwisho wa mwezi teh!teh!teh!(mambo ya mikukuta).So kabla sijakutakia weekend njema,hapa nakudokeza japo kiduchu tu nini utegemee wiki ijayo hapa kwenye blog yenu ya burudani.

                                   JERRY SPRINGER

*Jerry Springer with a New Brand Tv Show "Baggage" na kila kitu kuhusu huyu jamaa.
*Pt II ya makala yangu ya "special kwa kizazi cha Bongo Fleva",sehemu ya kwanza tayari, so nitaendeleza pt ii yake.
*Mtazamo wangu na ushauri wangu kidogo kuhusu bendi mpya ya hiphop ya Chid Benz (La Familia the Band) na bendi zingine za kijasiriamali.
*Kama kawa ijumaa nitakuwa na zile segment zetu mbili za "makengeza" yangu na "My album of the week",si vya KUKOSA.
*Pia kuanzia j5 ya wiki ijayo na kila j5 nitaleta segment mpya ya "Muziki na Maisha meets",hili ni shavu kwako mdau na fans wangu wote,nitakuwa na nafasi ya kutoa picha na profile kuhusu mdau yeyote wa muziki na maisha blog,si lazima awe star,so kama utataka utokee hapa,basi sio ishu hii ni nafasi kwako itumie,nitumie picha zako zozote na ukiwa popote na profile yako kwa ufupi kupitia emails hizi bizzo4shizzo@ymail.com na renatuskiluvia@ymail.com halafu j5 yoyote nitakutundika hapa.


*Birthday za mastaa na bila kusahau ma-breaking news kibao ya kiburudani ya ishu za mbele na hapa Bongo pia,so usikose kupitia blog hii weekend hii nzima,wiki ijayo na siku zote,pia usisahau ku-comment kwa lolote.NAKUTAKIA WEEKEND NJEMA,lets meet on Monday tukijaaliwa.Thanx.  

THE DUDE IS IN TOWN(WELCOME BACK HOM)

                                  HASHEEM THABEET MANKA

Mdau na fans wangu,jana katika pitapita zangu kwenye foleni zetu za mataa ya jiji hili ni kama sikuamini vile,pembeni yangu ikapaki gari moja ya maana sana,achana na hizi Range Rover Sport zilizojaa hivi sasa hapa town za milioni 45 mpaka 50,ilipaki Range Rover Vogue halisi ya "ukweli" ambayo bei yake kwa harakaharaka ni kama 250 mil za kibongo na ndani yake alikuwamo mchezaji anayechezea timu ya mpira wa kikapu ya Merphis Grizzlies inayoshiriki ligi nambari moja ya kikapu duniani ya NBA Hasheem Thabeet Manka,sasa ndo nikagundua kumbe mshikaji  yuko town.Karibu home bwana,mvua mvua ndo hii na kijotojoto kimepungua kidogo tuna-enjoy kiaina.

                                    RANGE ROVER VOGUE

MY ALBUM OF THE WEEK(Elevated by J-MARTINS)

Mdau na fans wiki iliyopita nilipata nafasi ya kukumwagia uhondo unaopatikana katika albam ya mwanadada Erykah Badu iitwayo "New Amerykah pt II(the return of Ankh)",naamini hivi sasa albam hiyo itakuwa ktk library yako ndogo nyumbani(gheto) si ndio??Leo fans narudi home Afrika,na niko na mchizi ambaye hivi leo ana show pande za Rock City(Mwanza) pale VillaPack pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba,anaitwa J-Martins.Na nataka nikufahamishe kuwa hivi majuzi tu(mwezi uliopita) mchizi alikuwa na tour moja ndefu sana U.K.

                                                    J-MARTINS(ELAVATED)

Jamaa ni mwandishi na ni producer pia katika studio za Don Family Records jijini Lagos,na ame-produce albams zote za wadogo zake(si wa tumbo moja) P-Square,pia ame-produce mwenyewe albam yake hii,albam ya Bracket na albam zingine kibao,kwahiyo akaona sio kesi nae kaamua kufanya albam yake mwenyewe.J-Martins alianza kuachia ngoma ambayo iliwashtua wengi "Good or Bad" na ambayo ilianza kusikika hapa Bongo kabla ya kwingine kokote Afrika hii(kwenye show ya kwanza ya P-Square Bongo mwaka juzi),baadae akaachia hit ingine "Oyoyo" na now anafanya poa sana na "Iva".

                                 J-MARTINS (UK TOUR)

Albam ina mikono kumi iliyoshiba ambayo ni "Oyoyo","Iva","Believe","Jukpa"feat;Bracket,"Change",
"Tonight"feat;Phyno&Douglas na "Good or Bad"feat;Victor.Zingine ni "Chameleon"feat;IllBliss,Waje&Real Macoy,"Kudi"feat;Wyre toka Kenya na "So fly remix"feat;Victor,Muna&Jesse Jagz.Rasmi iliingia kitaa Nov 2 mwaka jana 2009.So hebu fanyafanya uicheki halafu unipe matokeoooo au sio???

"MAKENGEZA" YANGU THIS WEEK(HEBU CHEKI HAWA HAWAFANANI KWELI JAMANI)

Jamani sasa hivi blog yenu ya burudani iko sawa so unaweza ku-comment mara kibao uwezavyo,wadau na fans baada ya wiki iliyopita kuwaleta mabrotherman wawili ktk segment yetu hii ya "makengeza" ambao walikuwa ni Jason Delulo na Chriss Brown na kukuuliza kama wanafanana au ni makengeza yangu tu,leo nakuja na hawa mabrother wengine wawili,but kabla sijawaweka hapa kwanza nashukuru kwa wote walioshiriki wiki iliyopita,naamini tutaendelea kushirikiana zaidi na zaidi,sasa leo niko naaaaaaaa!!!!!!

                                                                  AVANT
 
                                                R-KELLY

Hebu sasa niambie mdau wangu,hawa jamaa hawafanani kweliii???

Thursday, April 22, 2010

"NDOA" YA BONGO MOVIES NA EMPTYSOULZ PRODUCTION DEAD!!

Ile "ndoa" kati ya kipindi maarufu kinachorushwa EAtv kinachodili na superstars wa filamu za kibongo na kampuni iliyokuwa inatengeneza kipindi hicho EmptySoulz Production imefika mwisho.

                                                      JOYCE KIRIA NKONGO

Mpaka sasa blog ya burudani "muziki na maisha" haijapata "chamno" kilichotokea kati ya kampuni inayomiliki kipindi hicho(Local Movies)  na EmptySoulz Production.Kipindi hicho ambacho awali kabla hakijaanza kutengenezwa na EmptySoulz kilikuwa kinatengenezwa na Screen Media hivi sasa kinatengenezwa na PiliPili Entertainment na episode ya kwanza ya Pilipili Entertainment imeanza kuonekana j5 ya jana.

                                                EMPTYSOULZ PRODUCTION

KESHO KTK "MAKENGEZA" YANGU!!!

Kesho ni ijumaa fans wangu,so kama unafuatilia vizuri blog yetu ya burudani kama kawa kama dawa ile segment yetu ya "makengeza" itaendelea,nitakuwa na akina nani ambao mimi nahisi wanafanana??Don't ever miss it.

                                                   

HAPPY BIRTHDAY KAKA'

                                               KAKA

Leo tar 22 April ni birthday ya mshikaji hapo juu ambaye alizaliwa tar kama ya leo mwaka 1982,star huyu anakipiga kwenye klabu ya Real Madrid ya Hispania na pia timu ya taifa ya Brazil,jezi anayoivaa ni no 8.So kama unasheherekea birthday yako leo basi unashea birthday na superstar huyu wa soka.Blog ya burudani inawatakia wale wote wanasherehekea birthday zao leo Happy birthday.

Wednesday, April 21, 2010

RAPPER MWINGINE PIMP C AKUTWA AMEKUFA.

                                                          PIMP C
Baada ya jana blog ya burudani kuripoti juu ya kifo cha rapper mkongwe na memba wa kundi la Gangstarr GURU,leo blog hiihii ya burudani inaripoti juu ya kifo cha rapper mwingine PIMP C(pichani) ambae amekutwa amekufa  asubuhi ya leo kwenye chumba cha hotel aliyofikia,imeripotiwa kuwa mtu mmoja alipiga no 911 na L.A Country Fire kumkuta amelala juu ya kitanda chake akiwa tayari ameshakata roho.
PIMP C ambaye jina lake halisi ni Chad Batler alikuwa mmoja kati ya memba wawili wa bendi ya Hiphop ijulikanayo kama UGK,bendi ambayo ilijichukulia umaarufu sana baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Jay Z "Big Pimpin" mwaka 2000,mara ya mwisho walionekana kwenye video ya wimbo wa OutCast "International Player Anthem(i choose you)".
Perfomance ya mwisho ya mshkaji huyu ilikuwa pamoja na rapper mwingine Too Short na ilifanyika pale House of Blues L.A jumatatu ya wiki hii.R.I.P brother.

IJUMAA HII KTK MY ALBUM OF THE WEEK.......

                                    J-MARTINS
Ijumaa hii nitakuwa na albam ya mchizi huyu kutoka pande za Nigeria ambaye hivi sasa yuko kwenye ardhi ya J.K akipiga tour yakutosha tu,albam inaitwa "Elevated".Usikose kupitia blog hii ya burudani ili kujua zaidi......au vipi!!!!

Tuesday, April 20, 2010

BREAKING NEWS,GURU AFARIKI DUNIA.

Hizi ni habari ambazo zimenishitua sana kwakweli na kuniharibia siku yangu nzima,rapper wa kundi la Gangstarr GURU(43yrz) niliyemripoti kuendelea vizuri siku si nyingi nyuma hatimaye hatunaye tena,rapper huyu anayeheshimika sana amefariki dunia jana tar 19 asubuhi baada ya kuugua sana saratani na amekuwa akirudirudi kwenye koma mara kwa mara,akizungumza na vyombo vya habari jana jioni producer Solar amesema mchizi ameugua sana kwa takribani mwaka mzima na madaktari bingwa wamejitahidi sana kuokoa maisha yake lakini inaoneka kama MUNGU kampenda zaidi yetu,tutamkumbuka sana mchizi kwa ngoma kali,flows za ukweli na rylics za maana,"GURU umeondoka wewe lakini umetuachia ngoma zako kibao ambazo tutazitumia kukukumbuka".R.I.P.
GURU

HAPPY BIRTHDAY LUTHER VANDROS!!(RIP)

                                                    LUTHER VANDROSS
Anaitwa Luther Ronzoni Vandross ambaye alikuwa mkali wa kuogopwa wa muziki wa R&B,mtunzi na mtayarishaji pia,jamaa alizaliwa tarehe kama ya leo 20 April 1951,so kama wewe unasheherekea birthday yako leo fahamu kuwa una-share birthday na Star huyu.
Jamaa alipata nafasi ya kufanya albums zipatazo 9 ambazo ni (tarehe na mwezi ilipoingia kitaa kwenye mabano) "Never too Much"(01/02/1981),"The Best of Love"(01/02/1989),"Songs"(27/09/1994),"Your Secret Love"(01/10/1996),"One Night with you[the best of love]"(30/09/1997),"I know"(11/08/1998),"Super Hits"(22/08/2000),"Luther Vandross"(19/06/2001) na ya mwisho ambayo ni kali balaa inaitwa "Dance with my father"(10/06/2003).
Albums hizo zilipata nafasi ya kuuzwa zaidi ya nakala milioni 25 duniani kote na aliweza kulamba tuzo zinazoheshimika nane za Grammy.Rasmi alifariki July 01 2005.HAPPY BIRTHDAY&R.I.P Luther Ronzoni Vandross

MMESHINDWA??NAOMBA MJI WADAU.

Ilikuwa ni j5 ya wiki iliyopita,nilitoa kama ka-quiz hivi,nilitoa picha ya mtoto huyo hapo juu na kuuliza "Guess who is this",najua wengi walishindwa ku-comment coz najua blog yetu ina tatizo kidogo kwenye ku-comment,lakini wale waliopata nafasi ya kuniandikia emails wote walikosa,jamani huyu niiiiiiiii!!!!!!!
MAKO CHALI,producer mkali wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo,yuko pale MJ RECORDS.Thanx kwa wote walionitumia emails na tuendelee kushirikiana na blog yetu ya burudani.

THANX BRO CHOKA!!

Akhsante sana Dj Choka kwa yote ulioweza kunisaidia ili blog yetu ya burudani iwe bomba zaidi na iendelee kutoa burudani na jumbe mbalimbali za kiburudani kwa wadau na fans wake,uendelee kuwa na moyo huohuo na MUNGU AKUZIDISHIE.Amin!

Monday, April 19, 2010

DRAKE "ANAVYOHARIBU" WATU WETU!!!

Inakuwaje wadau & fans wa blog yetu ya burudani??Weekend ilikuwaje??naamini ilikuwa bomba sana au sio??mi binafsi weekend yangu ilikuwa poa sana,ok!ni jumatatu ambayo nimekuja na hii ishu moja nzito ambayo naomba tuijadili kidogo,koz nimekaa nimejifikiria sana na nikaona sio ishu nikishea nanyi fans halafu tuone inakuwaje.

                                                                    DRAKE
Juzi jumamosi nilikuwa home katika yale mapumziko ya weekend, nikaona sio kesi ngoja leo nitoe muda wangu nisikilize vipindi vya Bongo Fleva katika redio mbalimbali,kama tujuavyo wabongo tulioko hapa nyumbani(Bongo) jumamosi ni siku ambayo karibu redio zote zinakuwa na vipindi vya Bongo Fleva kuanzia mapema sana asubuhi kwahiyo kwa msikilizaji kazi yake inakuwa ni ku-touch dial tu kubadilisha station moja kwenda ingine kuendelea kusikiliza fleva.Sasa wakati nasikiliza, kituo kimoja hivi kikawa kinatambulisha nyimbo mpya za wasanii zilizowafikia,hapo nikapata nafasi ya kusikiliza nyimbo nyingi tu ikiwamo wimbo mpya wa Moxie ambao ndo umenipelekea kutaka kushea nanyi hili jambo.
                                                                 MOXIE 
Moxie kaachia ngoma mpya baada ya "chupa nyingine" aliyoifanya pale Fish Crab kwa Lamar,hii ngoma mchizi kafanyia Kiumbe Records kwa producer mmoja anaitwa Masoud,ngoma ni kali mdau wangu lakini kupitia ngoma hii nimemfahamu MOX mwingine kabisa tofauti na yule nimjuae mimi,Mox huko ndani ame-rap kidogo sana na sehemu kubwa kaimba(amini usiamini).Kichwa cha habari cha waraka huu ni "DRAKE ANAVYOHARIBU WATU WETU",Drake ni rapper ambaye kwa sasa yuko hot ile mbaya na track zake kibao zimefanya na zinafanya vizuri mpaka sasa,but style yake ya kuimba ni MBAYA na INABOA(nionavyo mimi),Drake sio mwimbaji,ni rapper,kwahiyo anapoimba anakuwa hana "tuning" ya sauti,anaimba kwa sauti kama anayotumia pia ku-rap,cha zaidi ana-"melody" na always anakuwa "onkey".Kinachofanyika ili ku-sound vizuri kile ambacho Drake anafanya ni "outotuning".Outotune ni software fulani ambayo ikiwekwa katika voko za mwanamuziki baada ya kurekodi huweza kutia nakshi na kuiremba sauti ili iwe na mvuto zaidi kwa msikilizaji(mambo ya teknolojia).Sasa wasanii wa kibongo ambao tuliwazoea katika zile styles zilizokuwa zinaonesha "realskills" zao leo wanafanya kama Drake,kweli???kitu ambacho mi sidhani kama kuna mtu yeyote anaweza akashindwa kukifanya,kuimba just kuimba kwa sauti yako halafu producer akaku-"outotune" nani anashindwa??
                                        MIKE TEE
Mdau hicho ndicho Moxie amekifanya kwenye ngoma yake hii mpya,na nataka nikuambie kitu mdau,sio Moxie tu ambaye ametumbukia katika mkumbo huo,wako wengine pia,kama vipi tafuta ngoma ya sasa ya Mike Tee "i love you" halafu sikiliza koras na ngoma ya sasa ya J-Mo "i need some money" sikiliza koras pia.Ni hayo tu mdau na fans wangu,unless otherwise ngoma zote zimesimama na ziko tight sana.Ukishindwa ku-comment hapa tafadhali nicheki katika bizzo4shizzo@ymail.com.
                                         J-MO