BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 7, 2010

SHAVU KWA IRINGA PIPO.....


Iringa pipo!!!!!, hii ni sehemu ingine ya ku-enjoy na kujifunza mengi kila j2 pale Shooters zamani Bottoms Up kuanzia kumi jioni mpaka nne usiku,ka-uchakavu ni buku mbili tu(2000),so! see u there this sunday.

TULIYOPATA NAFASI YA KUYAZUNGUMZA NDANI YA "TUPO PAMOJA" SHOW YA TTV.

BIZZO NA GIZZLE

Mdau jana nilifanya kukudokeza kiduchu tu khs mualiko wangu kwenye kipindi cha "Tupo pamoja" ndani ya TTV na nikakuahidi leo nitakwambia ni nini zaidi ambacho tulikizungumza.Mengi yamekwishazungumzwa juu ya mapungufu ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards na kutokana na hilo basi sisi hatukuona ni sawa kama tukiendelea kuzungumzia mapungufu hayo,cha zaidi ambacho sisi tulizungumza ni TAMASHA lenyewe la makabidhiano ya tunzo,maandalizi na mambo ya msingi ya kuzingatia kwa kamati ya maandalizi ya tunzo hizi "technically" na muundo mzima wa show kwa ujumla,kingine cha muhimu ambacho tuliona si busara kama tutakikalia kimya ni "appearance" ya wanamuziki na wasanii wenyewe hasa wa kizazi kipya katika tamasha lenyewe,kiukweli wasanii wetu hawajui ni namna gani "watokee" katika dhifa muhimu kama hizo,namna gani wavae,tumeshuhudia wengi wakichemka kimavazi hasa wasanii wa kiume.Nisiseme mengi wadau na fans,nnachoomba tuelekeze macho na masikio yetu kwenye tv zetu leo ijumaa saa 3;00 usiku pande za TTV ili tujue zaidi.Thanx!

COMING SOON..........

Hii ni segment mpya kabisa mdau,inaitwa "coming soon",hapa nitakuwa nakuletea albums ama movies mbalimbali za mbele na bongo pia ambazo zinakuja hivi karibuni,leo naanza na mzigo huu.

THANK ME LATER(COVER ALBUM)

Anaitwa Drake na mzigo mpya kabisa ambao hivi sasa uko katika promo ya nguvu,unaitwa "Thank Me Later" na unatoka mwezi ujao tar 15,nausubiri kwa hamu,wewe je???

"MAKENGEZA YANGU" LEO.......

BOBBY VALENTINO

JEREMIAH

Haya jamani yenu macho,juu ni Bobby Valentino na chini ni Jeremiah,hawafanani kweli wadau????

MNM's ALBUM OF THE WEEK(RISE UP By CYPRESS HILL)

Its a very good day,furahi-day(friday),naamni uko poa sana mdau na fans wa MNM Blog,leo kama kawa kama dawa tunakutana katika MNM's album of the week,kila ijumaa huwa nakuletea album moja kali na kukupa maelekezo kidogo khs album hiyo,kama vipi uitafute na kuiweka katika maktaba ili ijae mizigo mikali,wiki iliyopita nilikuletea "Raymond Vs Raymond" ya Usher Raymond,leo niko na watu wa HipHop zaidi,album inaitwa "Rise Up" ya Cypress Hill.


RISE'UP(COVER ALBUM)

Hawa jamaa wanagonga shughuli zao Los Angeles,na ni kundi linaloundwa na washkaji watatu ambao ni B-Real,Sen Dog na producer wao Dj Muggs,wamekuwa katika maisha ya ghetto na kujihusisha zaidi na biashara za dawa za kulevya kabla hawajajitumbukiza katika muziki,na Cypress Hill ndio wana-HipHop wa kwanza kukubalika na kutangaza Spanish HipHop.


CYPRESS HILL

"Rise Up" ni album yao ya kwanza chini ya uongozi wa Snoop Dogg ndani ya "Priority Records",ngoma "rise up" ambayo ndio imebeba jina la albam hii imetengenezwa na producer Tom Morello wa Rage Against the Machine Fame na zaidi unazungumzia watu kusimama imara na kupigania kile wanachokiamini.


CYPRESS HILL(1991 ALBUM)

Kabla ya album hii machizi wameshaachia albums zingine kibao tu,ndani ya "rise up" kuna ngomaz kali kumi na tano ambazo ni "It Ain't Nothing" Feat;Young De(wa huko), "Light it Up", "Rise Up" Feat;Tom Morello, "Get it Anyway", "Pass the Datch" Feat; Evidence&Alchemist, "BangBang", "K.U.S.H", "Get Em Up" na zingine kibao.


CYPRESS HILL(IV ALBUM)

Tukirudi kwenye Billboards Top 200 albums "Rise Up" ya Cypress Hill iko nafasi ya sabini na nne(74) na inazidi kupanda kadri muda unavyozidi kwenda,so hawa ndio Cypress Hill bwana kama unawafeel hebu wasapoti kwa kutafuta albam yao hii halafu uone kunani ndani,poaaaaaaa!!!!!!

Thursday, May 6, 2010

MY INTERVIEW IN "TUPO PAMOJA" SHOW ON TTV..

Mambo vipi wadu na fans wa blog ya burudani MNM??naamini mko pouwa kabisa au vp?mzuka!!Fans wangu leo nilipata nafasi ya kufanyiwa mahojiano kidogo na kipindi cha "Tupo Pamoja" na mtangazaji mahiri Arnie Gizzle wa TTV,chamno kilikuwa ni tamasha la makabidhiano ya tunzo za  muziki za Kili Tanzania ambazo zitafanyika wiki ijayo tar 15 pale Diamond Jubilee,hapa nakuwekea baadhi ya picha nilizopata nafasi ya kuzipata....enjoy!!!

                        ARNIE GIZZLE AKITAMBULISHA SHOW

                                                            ME CHILLIN'

                                   ANOTHER POOSE(READY 4 THE SHOW)

               ARNIE GIZZLE MAKINI,NIKIDADAVUA MAMBO

                                     VERY VERY MAKINI....

                                TALK!TALK!TALK BOY...TALK

         PRODUCER WA SHOW BIG THOM AKITOA MAELEKEZO

            BAADA YA SHOW,TUKASHOW LOVE KWA PAMOJA

               ME WITH PRESENTER WA SHOW ARNIE GIZZLE

Usikonde,leo hebu enjoy na hizo halafu kesho ni mpango mzima hapahapa kwenye blog ya burudani MNM,nitakwambia ni nini hasa tulikizungumza khs Kili Music Awards,na show hii lini utaiona kwenye tv yako,pia "album of the week" ninao Cypress Hill na "makengeza yangu" segment itaendelea kama kawa,tukutane kesho HAPA HOME,si ndio??Paaaa!!!!

Wednesday, May 5, 2010

HAPPY BIRTHDAY CRAIG DAVID....

Leo tar 5 May ni siku ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Craig David, alizaliwa tar kama ya leo 1981 nchini Uingereza.Craig David kiukweli mi nampenda sana japo ana muda mrefu kama yuko kimya hivi,so kama unazaliwa leo basi fahamu kuwa unashea birthday na brotherman huyu.Happy birthday mtu mzima Craig David.

                                               CRAIG DAVID

THIS FRIDAY ON "MY ALBUM OF THE WEEK"

Ijumaa hii kwenye MNM's "album of the week" nitakuwa na machizi hawa hapa chini...........na kitu yao mupyaaaaaa kbs.....


                                    CYPRESS HILL

So!!!kama vipi usikose kupita hapa.........kucheki na kuona kama waweza itafuta uufaidi uhondo ulioko ndani,USIKOSE!!!!

MNM MEETS...........FELIX D. KAOMBWE.

                                       FELIX D. KAOMBWE

Haya!haya!haya tena wadau na fans wa blog ya burudani MNM,leo ni j5 ingine tena tunakutana katika ile segment yetu ya "MNM Meets",na leo niko na mchizi toka pande za Tabora na ni mkali ile mbaya katika yale anayoyafanya,sasa hebu cheki profile yake hapa down....
                                  
                                 NAME;Felix D. Kaombwe
                                 NICK NAME;FDK-One(Pekee) 
                                         OCCUP;Radio Presenter&producer
                                 MEDIA;Ebony fm
                                 LOCATION;Dar-Es-Salaam
                                 AGE;32yrz
                                 HOBBIES;Music,Movies,Sports etc

                                        FDK-ONE DOIN' HIS THING(SIBUKA FM)

Haya mdau,na wewe kazi kwako,kama unataka kutokea hapa kwenye blog ya burudani fanya hivyo fasta,nitumie picha na maelezo yako kiduchu halafu nifanye mpango mzima.(bizzo4shizzo@ymail.com au renatuskiluvia@ymail.com)

Tuesday, May 4, 2010

HALLE BERRY SAIV NAOMBA IWE ZAMU YANGU BASI...

                               HALLE BERRY WIT DAUGHTER

Hizi ni habari zilizonishtua kidogo na kujiuliza jamani tatizo ni nini??Aliyekuwa mke wa supastaa wa R&B Erick Bennet na mshindi wa tuzo ya Oscar ambaye ni model mkali na mwenye mvuto huko nchini Marekani Halle Berry amepigana chini na jamaa yake wa sasa Gabriel Aubry ambaye pia ni model kutoka Canada.Habari zinasema wawili hao wamemwagana miezi michache nyuma lakini hawakupata nafasi ya kutangaza rasmi.

Chamno kinasema hatua hiyo imetokana na Gabriel kutokuwa na juhudi ya kuyafanya mahusiano ya wawili hao yawe endelevu(usiniulize kivipi) na hivyo Halle Berry kuamua kusitisha malove-dav kwa jamaa japo wataendelea kushiriki kwa pamoja kama wazazi kumlea binti yao "very cute" aliyepatikana enzi za kufana kwa "kuch-kuch hotae" kati yao.Gabriel mwenyewe anasema "sina cha zaidi cha kusema lakini ni wakati mgumu kidogo niliowahi kuupitia,Halle ni mmoja kati ya watu wazuri,wenye upendo,malengo na mvuto niliokwishawahi kukutana nao,imetokea na sasa tuangalie yajayo".Baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na Erick Bennet Halle Berry ndo akawa na jamaa huyu,sasa nani atafuata??naomba iwe mimi basi jamani???.....

MPAKA HUYU??BADO MIMI TU.....

                                          BIG DADY KANE

Rappa wa muda mrefu kunako game ya muziki huu nchini Marekani Big Dady Kane(BDK) afunga ndoa.Big Dady ambaye jina lake halisi ni ANTONIO MONTERIO HADY amefunga ndoa na aliyekuwa galfriend wake wa siku nyingi Shawnette jumamosi ya wiki iliyopita na kufuatiwa na bonge la party la kisupastaa huko pande za North Carolina.

Mshkaji wake mmoja ameandika kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa amefurahi na kusema kuwa ilikuwa party nzuri kati ya alizowahi kuhudhuria,awali mchizi alimpiga chini demu wake huyu(Shawnette) na kuwa katika mahusiano na Madonna kabla ya kumwagana na kumrudia tena na Shawnette.Ni hatua ya kiutu uzima na MNM inampongeza mchizi kwa kuona sio ishu ngoja avute kitu ndani ili maisha yaendelee,bado mie......teh!teh!teh!