BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 14, 2010

BATA ZOTE HAPA...


Iringa tusisahau,MPANGO MZIMA uko hapa J2 hii pale Shooters zamani Bottoms Up,twende tumetupia halafu bata mwanzo mwisho,tukutane hapa.

MNM's "ALBUM OF THE WEEK" UNTITLED By R-KELLY...

Wiki iliyopita katika album of the week mdau na fans wangu,nilikuwa na CYPRESS HILL na kitu mupya kabisa "RISE UP",hiyo ilikuwa katika HIPHOP naamini ulii-enjoy sana na inawezekana unayo hivi sasa,leo niko katika R&B,tena yule King wao,R-KELLY,na album yake ya sasa "UNTITLED",mpaka sasa jamaa ana singles mbili kali hewani,awali aliachia "ONE" ambayo alimtupia KERI HILSON humo,na sasa ameachia "BE MY NO 2".


Album imeingia mtaani rasmi Septemba 29 mwaka jana chini ya Jive Records & Zomba na ndani ina ngoma 16 kali ambazo zimetengenezwa na R-Kelly mwenyewe na producers kibao kama Lil Ronnie,Gas,Jazze Pha,Infinity,Dj Campa,Los Da Mistro,T-Town Production,Christopher "Deep" Underson,The Pentagon na wengine kibao.Baadhi ya ngoma zilizomo ndani ni pamoja na "Craizy Night" Feat;Rock City, "Text Me", "Exit", "Echo", "Like I do", "Fallin from the Sky", "I Love the Dj", "Elsewhere", "Number One" Feat; Keri Hilson", "Religious" na zingine kibao ambazo siwezi kuzitaja zote hapa.


UNTITLED(ALBUM COVER)

Mdau album hii wiki mbili tu za kwanza ilikimbilia platinum,kama unapenda R&B na SLOWJAMS kama mimi,hii kitu si ya kukosa kabisa,fanya uitafute halafu uone mpango mzima ukoje huko ndani.

LEO USIKU KTK "TUPO PAMOJA" SHOW ON TTV.


ARNIE GIZZLE AKIWA NA KALLAGE

Leo usiku katika "Tupo Pamoja" show ya Tumaini Tv(TTV) Arnie Gizzle ataongea na mtayarishaji mkali wa video za kibongo John Kallage wa "Kallage Pictures",usikose hiyo katika side B,katika side A mchizi ataongea na jamaa kutoka Manzese Ney wa Mitego,usikose mida ya saa tatu kamili za usiku mpaka kuendelea.


NEY KTK SHOW

"MAKENGEZA YANGU" TOO MUCH,CHEKI HAWA...

 
NOTORIOUS B.I.G
                                                

 
GORILLA BLACK
                                                

Wiki iliyopita katika segment yetu hii tulikuwa na Bobby Valentino na Jeremiah,na nikauliza je hawafanani kweli??bado tunaendelea kupitia mstaa mbalimbali ambao mi nahisi wanafanana,sasa wiki hii cheki hao juu,Notorious B.I.G na Gorilla Black,nipe maoni wawaonaje??hawafanani kweli??au makengeza yangu too much sasa?

Thursday, May 13, 2010

FID NA GOMA JIPYA...

FID Q
                                                 
Ni habari ambazo nimezipokea muda si mrefu toka kwenye facebook kuwa,mchizi toka Mwanza Fareed K aka Fid Q aka Ngosha now anapika ngoma ambayo soon itakuwa masikioni mwako,ngoma inaitwa "ngosha the swagga don" na ktk koras kasimama Naj,cha kushangaza zaidi ni kwamba Fid ameimba katika vesi ya pili,mikono ni ya Mako Chali pale Mj Records,tusubiri tuoneee!!!!!!!

COMING SOON!!ROSCOE DASH WT "READY SET GO!"

READY SET GO!(COVER ALBUM)
                          
Dogo nimemuona juzi tu BET katika show inaitwa 106&Pack akiutangaza mzigo wake huu,unaitwa "Ready set Go!,utatoka june 1 mwaka huu,yaani mwezi ujao tu,Roscoe Dash ni mmoja kati ya marapa wachanga ambao wanakuja kuwa noma sana,usisubiri ahit ndo uanze kumfuatilia,waweza anza sasa. 

ROSCOE DASH
                                                          

Wednesday, May 12, 2010

THIS FRIDAY ON MNM's "ALBUM OF THE WEEK".....

UNTITLED(COVER ALBUM)
                          
Ijumaa hii nimeona nikurudishe ktk R&B,na nitakuwa na mfalme wa R&B R-Kelly,mzigo unaitwa "Untitled",usikose kuona ni nini ambacho jamaa amekifanya humu ndani,kama kawa mchizi hulenga mulemule,TUTAONA!!                           

ITS A BOB MARLEY DAY PIPO!!!!!!!

 
BOB AKINYONGA KITU
                                     
Pipo leo ni siku ya Bob Marley,tar 12 May ya kila mwaka wapenzi na fans wote wa muziki wa regge wanakumbukia siku ambayo dunia nzima ilizizima kwa majonzi baada ya kupokea taarifa ya kushtua ya kifo cha muasisi na mfalme wa muziki wa regge duniani Robert Nesta Marley almaaruf kama Bob Marley,hiyo ilikuwa mwaka 1981,ni miaka takribani 29 sasa toka jamaa atangulie kwa ugonjwa wa kansa ya mguu.


BOB MARLEY
                                             
Kiukweli kwa miaka yote hii 29 ambayo huyu jamaa amekuwa hayupo ktk game hakuna aliyetokea kama yeye,uongo??So Rastafarians wote MNM inawatakia Bob Marley Day njema,harakati ziendelee....

MSHAHARA WA HASHEEM THABEET HUU HAPA.

HASHEEM THABEET MANKA
Jana mdau wakati niko njiani natoka zangu ofisini nikawa nasikiliza "Jahazi" la Cap. Gadna na mzee wa "kama pundaaaa!!" Kibonde,hapo nikapata bahati ya kusikiliza mahojiano ya mcheza kikapu mtanzania ndani ya NBA Hasheem Thabeet Manka,yalikuwa mahojiano ya kibiashara zaidi kama ambavyo Gadna mwenyewe alivyoyatambulisha,yalizungumzwa mengi lakini kati ya yote moja tu ndo lililonishtua kidogo,ni MSHAHARA wa jamaa.Hasheem analipwa na Merphis Grizzlies pesa za kitanzania zaidi ya milioni 190 kwa wiki,ambapo ukipiga kwa hesabu ya harakaharaka ni zaidi ya milioni 450 kwa mwezi,na hiyo ni mbali na marupurupu mengine ikiwa ni pamoja na kulipiwa mishahara ya wasaidizi wake wa karibu na gharama zote za mazoezi na chakula,kitu pekee ambacho jamaa anakifanya toka katika package yake hiyo ni malipo ya nyumba anayoishi huko Marekani.Sasa hapo ndo nikagundua kumbe hata ile Vogue aliyomnunulia mamake ni mshahara wake wa wiki moja na nusu tu.Safi sana Hasheem,we Tanzanians are very proud of you dude,keep it up,tuko pamoja.

MUZIKI NA MAISHA(MNM) MEETS....LADY VC

VAILET AMON CHONYA

NAME;VAILET AMON CHONYA
NICK NAME;LADY VC
OCCAPATION;RADIO PRESENTER
MEDIA;87.5 KILI FM
SHOW;RUSH HOURS
LOCATION;MOSHI/KILIMANJARO
AGE;28yrz
HOBBIES;MUSIC,MOVIES,NOVELS etc

Haya mdau,leo niko na mdashosti toka pande za kaskazini ambaye kiukweli anaijua kazi na anaipiga kwelikweli,nasema hivyo coz mi nilishawahi kupiga nae mzigo pande hizo,yuko sawa,sasa wiki ijayo unaweza kuwa wewe,hebu nicheki kwenye bizzo4shizzo@ymail.com au renatuskiluvia@ymail.com nitumie picha na ki-profile kifupi halafu tuone au vp.

Tuesday, May 11, 2010

2MORROW ON "MNM MEETS".......


Nani??labda wewe uliyenitumia profile yako,pita hapa kesho uone....see you 2morrow.

SUNDAY BEST YA BET NI NOMAAA........


Unataka kuona watu wanaimba??wanaimba kweli na si kutania??hebu pitapita kwenye Tv yako hasa BET uone,ni noma mdau,jana usiku katika zururazurura yangu pande za BET nikabambiana na auditions za shindano la kuimba nyimbo za injili lijulikanalo kama "Sunday Best" season 3 ambalo lilikuwa New Orleins,duh nikagundua kuwa kuna ma-underground hatuwajui na wanaimba.


Ni kama "Gospel Star Search" kwa hapa kwetu,ila wenzetu wako very serious na wanaweza,mpaka nikajiuliza hivi mimi ndo ningekuwa judge ningemchagua yupi na kumuacha yupi,judges katika shindano hilo ni waimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Marekani Kirk Franklin, Tina Campbell na nduguye Erica Campbell wanounda kundi la "Mary Mary".Hebu tazama BET halafu ukiigumia utanipa majibu.NOMA!

                                    MARY MARY

Monday, May 10, 2010

HAPPY MOTHERS DAY!!!!!!!


Wadau na fans wa blog ya burudani "Muziki Na Maisha"(MNM),naamini weekend yako ilikuwa poa sana na j3 hii kila kitu kiko katika mstari,nakushukuru kwa kuendelea kuifuatilia blog hii,wadau jana j2 ilikuwa ni siku ya mama dunia "world mothers day",je wewe ilimfanyia nini mama yako??si lazima umnunulie zawadi kubwa sana lakini hata kama ni kidogo ni kipi ulichokifanya kwake?ulimfanya aone japo raha kidogo na kumsahaulisha uchungu wakati anakuzaa wewe??Mimi binafsi nilimfanyia mengi mama yangu na kama haitoshi,leo natumia blog hii ya burudani kumwambia kuwa "NAJIVUNIA KUWA MMOJA WA WATOTO WAKE",najua ananipenda sana,nami namjibu "NAKUPENDA SANA MAMA",HAPPY MOTHERS DAY MAMA KILUVIA.