BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 21, 2010

KIPINDI CHA PLANET BONGO EATV CHAPOTOSHA UMMA(Pt I)

             Wadau habari zenu,naamini hali zenu ni njema kabisa na ujenzi wa taifa unaendelea kama kawaida,leo nina mengi sana ya kuzungumza juu ya yale yaliyonikera,kama wiki tatu sasa nimekuwa karibu sana na kipindi cha PLANET BONGO cha EATV nikikifuatilia kwa ukaribu zaidi.Kwa wale wafuatiliaji wa kipindi hiki wiki hizi tatu kipindi kilikuwa kinarusha exclusive toka Mwanza(Rock City) pamoja na Arusha(A-Town).Kutokana na hilo nimepata nafasi ya kugundua kitu, kipindi ambacho mtangazaji wa PLANET BONGO Abdalah alikitengeneza Mwanza ni wakati alipopata nafasi ya kwenda kwenye show ya mwanamuziki wa Nigeria J-Martins iliyofanyika jijini humo hivi karibuni na kile kipindi cha Arusha hakukitengeneza yeye,bali alichukuwa kipindi ambacho kilitengenezwa na mtangazaji mwingine wa kituo hicho Bhoke Egina aliyekuwa anafanya kipindi cha 5 CONNECT wakati huo na kilikwishawahi kutumika kabla ndani ya kipindi hicho cha 5 CONNECT.

               Kilichonisukuma kuandika makala haya ni muendelezo ambao Abdalah aliufanya na kunitatiza,sijui idea hii aliipata wapi,napata shaka kuwa mtangazaji huyo halikuwa kusudio lake la kwanza kufanya hivyo wakati anatengeneza kipindi hicho,nadhani ni idea ambayo ilikuja katikati kabisa na inawezekana ilikuja wakati tayari sehemu ya kwanza ya Mwanza na ya pili ya Arusha imeshakwenda hewani,na kilichofanyika ni ”ilimradi” kipindi cha wiki ya tatu kipatikane ili wiki ipite,hii si dalili nzuri kwa crew nzima ya kipindi pamoja na mtangazaji huyo aliyepatikana toka katika mchakato mrefu na mgumu uliohusisha vijana zaidi ya 500 waliokuwa wakiiwania nafasi hiyo mwaka juzi.Kipindi cha PLANET BONGO cha wiki hii ya tatu kilifanywa kwa kulinganisha mikoa hii miwili iliyotumika kutengeneza vipindi vilivyopita(Mwanza na Arusha),kwamba wapi kuna muziki zaidi?Mwanza au Arusha?na wengi waliopata nafasi ya kuzungumza ni wafanyakazi wa EATV,nilipata nafasi ya kumtambua Dj Kim na maproducer wa vipindi mbalimbali vya kituo hicho,na wote walitoa tathmini kutokana na kile kilichofanywa katika vipindi vilivyopita.Yalizugumzwa mengi lakini mwisho wa siku aliyekuwa akitazama kipindi aliweza kupata matokeo japo hayakutangazwa,Arusha ilionekana INA MUZIKI zaidi ya Mwanza,chimbuko la muziki wa HIPHOP lilionekana Arusha.
                 Kuna mwanafalsafa mmoja alikwishawahi sema “NO RESEARCH,NO RIGHT TO SAY” akiwa na maana “BILA TAFITI,HAKUNA HAKI YA KUSEMA”,kitu ambacho crew ya kipindi cha PLANET BONGO imekifanya,crew hiyo imesema bila kufanya utafiti wa kutosha,binafsi sidhani kama hawa jamaa walikuwa na haki ya kulinganisha kimuziki mikoa hiyo miwili kwa kutumia “tuvipindi huto tuwili” walitotutengeneza.Mimi ni mwenyeji wa Mwanza,nimezaliwa Mwanza,nimekulia Mwanza,kwahiyo Mwanza naijua vizuri na muziki wa Mwanza naujua vizuri sana(hakuna anayeweza kunidanganya).Binafsi nimekuwa mdau wa muziki Mwanza tangu napata akili za kiutu uzima,nimefanya kazi kama mtangazaji wa redio zaidi ya moja kanda ya ziwa na nimekuwa niki-deal na muziki huo kanda ya ziwa kwa zaidi ya miaka nane, ndo maana nimeamua kuzungumza haya,naamini Mwanza kuna MUZIKI zaidi ya kokote TANZANIA hii,utafiti huo nimekwisha ufanya japo si utafiti rasmi,nina utetezi na sababu nyingi na za msingi za kusema hivyo,naomba nianze kutoa utetezi wangu kwanza kutoka katika vipindi hivyo vya PLANET BONGO vilivyorushwa.

KIPINDI CHA PLANET BONGO EATV CHAPOTOSHA UMMA(Pt II)

                Kwanza Abdalah hakujiandaa kutengeneza kipindi rasmi cha kuja kuishindanisha Mwanza na Arusha,kitu alichokifanya ni kutengeneza kipindi cha “bora liende” ili tu mwisho wa siku ionekana hakwenda Mwanza burebure,ni dhahiri alirekodi kipindi kabla ama baada ya show ya J-Martins,kwahiyo kulikuwa na haraka ya ama kuwahi mambo mengine ya msingi zaidi yaliyomfanya aende Mwanza au kuwahi kufanya haraka ya kujiandaa na safari ya Arusha kuendelea na tour ya J-Martins ambayo kiratiba ilikuwa ipigwe siku moja baada ya show ya Mwanza,na ndio maana aliweza kuzungumza na wasanii kutoka studio moja tu ambayo ni mpya na wasanii wote ma-underground na ambao hawana hata experience ya kuzungumza na MEDIA,Dullah alizungumza na producer SAMTIMBER na baadhi ya wasanii wanaofanyakazi katika studio za A2P Records,tukianzia na hapo, A2P Records sio studio ya mfano kwa MUZIKI wa Mwanza,ni studio ndogo bado,tena sana tu,kufanyakazi na baadhi ya wasanii kutoka hapa Dar haina maana tayari imekwishakuwa studio ya mfano,wasanii toka Dar hawajaanza leo kusafiri mpaka Mwanza kurekodi nyimbo,wameanza tangu enzi ENRICO yuko Mwanza akimiliki MWANZA RECORDS mwaka 2001.Kama Dullah alikuwa na nia ya kutengeneza kipindi Mwanza cha ushindani wa kweli angekwenda katika studio zenye muda kidogo Mwanza na kutengeneza kipindi hicho,mfano angekwenda basi MO RECORDS akaonana na producer Q ambaye sasa yuko huko baada ya kuondoka BONGO RECORDS,au angekwenda basi TETEMESHA RECORDS akapata nafasi ya kuiona studio ambayo imekwisha tengeneza HITS kibao ambazo zinachezwa kwenye redio stations kibao kila kukicha bila hata ya wapenzi wa muziki kujua kuwa kumbe nyimbo hizo zimetoka MWANZA,studio ambayo imewatoa wasanii kibao akiwemo HUSSEIN MACHOZI ambaye hakuna asiyemjua leo. Kuliko kufanya alichokifanya.
              Mbali na hivyo bado huwezi kupata ripoti ya ukweli KIMUZIKI kwa kuongea na producer mmoja tena mgeni na ma-undergroung wawili watatu,historia ya muziki wa eneo fulani huwezi kuipata hivihivi tu,ni lazima uvuje jasho kwa kuwatafuta WAZAWA halisi wa eneo husika,zungumza na watu wa MEDIA wenzio wa muda mrefu eneo hilo,zungumza na wasanii wa zamani wa eneo husika,zungumza na mapromota pamoja na malegendari mbalimbali katika kiwanda cha burudani katika eneo husika utapata ripoti sahihi,kitu ambacho huyu mshkaji wetu hakufanya hata kwa asilimia moja,ndo maana napata wasiwasi kwamba inawezekana PLANET BONGO sasa inaanza kumshinda Dullah.Vitu vyote hivyo vinahitaji maandalizi makubwa na ya muda mrefu,sio kuripuaripua,Dullah angefanya hivyo au la,angemaliza mtiririko wake kawaida bila kufanya mlinganisho KIMUZIKI kati ya Mwanza na Arusha.Kwa waliopata nafasi ya kuzungumzia tathmini kimuziki kati ya Mwanza na Arusha katika sehemu ya tatu ya exclusive hiyo, walimtolea mfano mwanamuziki H-BABA,ni vitu vya kuchekesha sana kwakweli,H-BABA ni mwanamuziki mzuri ila sio ishara ya muziki wa Mwanza japo ametokea Mwanza,H-BABA ni “kitukuu” cha muziki huu Mwanza.
                Mi nakumbuka back in a days,mwanzoni mwa miaka ya 1990 watu kama Hayati HAMAD aka TERMINATOR X(RIP),watu kama kina PAUL JAMES(PEE JAY) ambaye sasa ni mtangazaji wa Clouds na mwenzake YAQUB waliokuwa wanaunda kundi la GGV,Dj YUSUPH(yuko UK now),KASSIM MTINGWA(nduguye RUKIA MTINGWA wa VODACOM) na K-SOLO waliokuwa wanaunda kundi la WEPWAA(Wepesi Wa Akili) na makundi mengine kama III-DA FAD,II NATURE BOYS(lililomkuza FID Q) na baadae THA ROTTEN BROTHERS,BH MOBB(Toka Bugando Hill Side), G.W.A(Gangstars With Atitude),SWAHILI GENERATIONS(Toka Mlango Mmoja),CHICAGO WHITE SOX,KING KIFF NIGGA(mwandishi wa magazeti ya Sani,blogger pia),JONTWA JOKERI toka Pasiansi ambako ndo chimbuko la muziki wa Dancehall na Raggae Maffin(Ni mchungaji leo na anamiliki kanisa lake),RWEYMAN na SHIJA(RAGGEA NATION) na washkaji wengine kadha toka mikoa ya jirani kama BOB HAISA &SWEET K na jamaa flani walikuwa wanajiita PMD(PLUS MINUS DIVIDE) toka Shinyanga na wengine wengi ambao siwezi kuwataja wote hapa,hao ni baadhi ya malegendari wanaothibitisha kuwa muziki Mwanza umeanza kitambo na si juzijuzi kama inavyoonekana,wakati huo matamasha ya muziki huu yalikuwa yanafanyika GADHI HALL pale kwenye makutano ya barabara za Nyerere,Kenyatta na Makongoro,LIBERTY CINEMA mtaa wa Liberty na ukumbi wa sinema wa zamani ambao baadae ulikuja kuwa ukumbi wa disko TIVOL barabara ya Posta,baadhi ya malegendari wengine ambao hawakuwa wasanii lakini wadau wakubwa ni kama DAUDI NYALA(DAVID LATTAH) huyu ni mdogo wake na Mh.Antony Diallo,DJ ENGENEER(alikuwa MC wa matamasha karibu yote wakati huo),MARCO TIBASIMA,OSCAR MAKOYE(DJ OSCAR MARK),DJ MILIONARE(Jacob Usungu),DJ EDDY GRAND(Delux Disco),RENA CALIST(Promota),MC STOPA(Muhsein Mambo)na wengine kibao tu ambao wapo na wanaweza kupatikana kuthibitisha hilo.

LEO USIKU KTK "TUPO PAMOJA" SHOW ON TTV.


Kutokana na maombi ya watazamaji kibao ambao hawakupata nafasi ya kucheki "tupo pamoja" show ya TTV wiki iliyopita,kwa kuwa wengi walikuwa karibu kufuatilia utoaji na upokeaji wa tunzo za Kilimanjaro Tanzania,kipindi cha "tupo pamoja" cha wiki iliyopita kitarudiwa leo,katika SIDE A alikaa kitini mtu mzima Ney wa Mitego na SIDE B aliwekwa "kitimotozz" mtayarishaji bora wa video Bongo(2008-2009) John Kallage wa Kallage Pictures,usikose show hii ya ukweli na mtu mzima ARNIE GIZZLE kwenye "kioo" chako mishale ya saa tatu kamili usiku,Don't Miss d' Show.TUPO PAMOJA.

MNM'S ALBUM OF THE WEEK..."AMAZIN' BY TRINA...

Baada ya wiki iliyopita kumtembelea KING wa wote katika R&B huko mbele mtu mzima R-Kelly,na tukaichambua na kuitazama kwa pamoja albam yake ya sasa "UNTITLED", leo tunaweka usawa wa kijinsia kwa kumcheki mdada anaitwa KATRINA LAVERNE TAYLOR aka TRINA na mzigo wake unaotisha unaitwa "AMAZIN".Mwanadada huyu alizaliwa Dec 3 mwaka 1978 na sasa amekuwa nominated katika tunzo za BET katika category ya "The Best Female Hiphop Artist" 2010.Kihistoria Trina anatoka MIAMI Florida United States na amekulia katika maisha ya tabu sana,kimuziki alianza kusikika katika collabo na Tricky Daddy ngoma iliitwa "Nann Nigga" mwaka 1998,baadae akasaini Slip-N-Slide Records akaachia mzigo wake wa kwanza mwaka 2000 kwa jina "Da Baddest B***ch",baadae akaanza kuachia albams mwaka hadi mwaka kama "Diamond Princess"(2002),"No Patients"(2004),"Glamorest life"(2005),"Here We go Again"(2006) and "Still the Baddest"(2008).

TRINA

Amazin iliachiwa rasmi kitaa tar 4 mwezi huu wa tano,kwahiyo bado ni mpya kabisa na ndani una mikonoz kumi na tano minene mwanzo mwisho,kama "Thaz Ma Attitude", "Million Dolla Gal" feat; Keri Hilson&Diddy, "On Da Hush" feat; Shonie, "Dang a Lang" feat; Lady Saw&Nicki Minaj, "I want it all" feat; Monica Arnod, "White Gal" feat; Flo Rida&Git Fresh, "My Bitches", "By Myself", "Always" feat Monica, "Currency" feat Lil Wayne&Rick Ross, "Make way" feat; Lyfe Jennings, "Let Dem Hos fight" feat; Kalenna, "Showing Out" na "Carpricon".
DA BADDEST B***CH

Mzigo una urefu wa dk 56 na sekunde 25 na ni kutoka EMI,Slip-N-Slide na DP Entertainment,umepikwa na producers wakali wafuatao,Jim Jonsin,CP Hollywood,Travis Spicey,Mario Winanz,Oddz and Endz,Maxwell Smart,Cozmo na Schife&Ohzee.Nyimbo zilizotangulia ni "Thats my attitude" ulioachiwa Oct 17 mwaka jana,"Million Dolla Gal" ulioachiwa Jan 7 mwaka huu,"Always" ulioachiwa muda mfupi kabla mzigo haujadondoka kitaa na BONGE moja la ngoma lililonifanya nikuletee mzigo huu wiki hii "Currency" aliofanya na Lil Wayne na Rick Ross ambao ndo umeachiwa sasa hivi.Albam hii "AMAZIN" ya Trina iko nafasi ya 49 wiki hii katika Billboards Top 200 albums,niko chini ya miguu yako mdau na fans wa MNM,tafuta albami hii halafu tulia usikilize kwa makini,NI BONGE MOJA LA ALBAM.Thanx!

 
AMAZIN(COVER ALBAM)

TODAY IN "MAKENGEZA" YANGU SEGMENT.......

Wiki iliyopita tulikuwa na jamaa wawili ambao kiukweli wanafanana sana mpaka namna wanavyochana kimuziki,alikuwa ni marehemu NOTORIOUS BIG na Bwn Mdogo GORILLA BLACK,je leo??????........

SOLANGE


BEYONCE

Ni Solange Knowles na Beyonce Knowles,hawa mdau wangu ni ndugu kabisa,lakini wangapi ndugu lakini bado hawafanani??sasa nataka uniambie,japo hawa ni ndugu lakini je wanafanana kweli??au "Makengeza" yangu bado hayajapona?

Thursday, May 20, 2010

TOMORROW ON MNM'S ALBUM OF THE WEEK...

AMAZIN'(COVER ALBUM)
                                                              
Don't ever,ever,ever dare to MISS IT,2morrow here on MNM Blog.

COMING SOON.......WHITE MARIA.

WHITE MARIA(MOVIE COVER)
                                                     
Hii next week itakuwa kitaani kwako,ukiitafuta utaipata,mzigo mwingine wa Stiven Kanumba lakini huu sasa unatoka Game 1st Quality na utasambazwa na haohao,movie hii itatukumbusha "The red valentine" na zingine ambazo Wema Abraham Sepetu na Stiven Kanumba walihusika kwa pamoja na ambazo zilikuwa kali balaa,ilishutiwa mwaka 2008,mimi naingojea kwa hamu sana nione kunani huko ndani,hasa kwakuwa pia hawa watu walikwishawahi kuwa katika "mapenzi matamu" then "mapenzi mabaya",itafute pia...

PROPAGANDA YA FID SASA INAPATIKANA ONLINE.

PROPAGANDA

Albam ambayo imeingia kitaa si zaidi ya miezi mitatu iliyopita "Propaganda" ya Fid Q sasa waweza inunua kupitia mtandao,Fid ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita ameachia kitu yake mpya "Fid the Swaga Don" akiwa na Naj,Quick na Adam Mchomvu ameniambia ngoma hiyo iko nje ya albam ya "propaganda" na itapatikana ktk compailation albam ya Mako Chali pale Mj Records,fanya kuinunua "propaganda" kupitia http://www.reverbnation.com/store/artist_484986 uzidi kuinenepesha library yako home.

USIKU WA REGGE(MUSIC LIVE)


Huu ni upendeleo mwingine kabisa kwa wakazi wa Iringa(I town),usiku wa regge now ndani ya ukumbi wa IDYC(zamani MAKOSA) jumapili hii,live band huku zikipigwa ngoma mbalimbali za legendaries wa regge duniani kama Robert Nesta Marley(Bob Marley) na wengineo wengi,pia bata mdogo mdogo kwa kwenda mbele,usiikose hii mwana,"kauchakavu" mlangoni ni buku tatu tu za kibongo kuanzia saa mbili usiku mpaka "mswaki",tukutane pale.

Wednesday, May 19, 2010

TOP 9@9 SHOW NEW LOGO..

TOP 9@9 NEW LOGO
                                                           
Show sio mpya,show ina muda kidogo kwa hewa,ni Top 9@9 kila jumatatu na jumanne pale Kiss fm kuanzia saa tatu kamili mpaka nne kamili,unasikiliza nyimbo tisa kali mwanzo mwisho,host ni Ezden the rocker kama kawa kama dawa mpango unasongeshwa,hiyo ni logo mpya kabisa ya kuitangaza show hii,so kama uko pande ambazo Kiss fm unaipata basi hebu skilizia halafu tuone...

IRINGA PIPO LEO USIKU...

AKUDO IMPACT

Leo usiku pale VIP Club Iringa kazi kwenu,Akudo Impact(Vijana wa Masauti) wako pale kwa ajili yako wewe mpenda burudani,nenda pale ukapekechepekeche pamoja nao au vp,kazi kwenu kama "viunu" vipo...

MNM MEETS.....EVANSON LISEKI..

EVANSON LISEKI

NAME;Evanson Liseki
NICK NAME;Folosani
OCCUPATION;Student
LOCATION;Moscow(Russia)
 AGE;28yrz
HOBBIES;Basketball,Soccer,Music

Haya mchizi kauza kama unavyomuona hapo juu,miaka miwili ijayo atapanda cheo na kuitwa Dr. Evanson Liseki coz ndicho anachobukua pande hizo,ni mwenyeji wa Mwanza,kazi kwako sasa mdau,fanya fasta nawe nicheki kwa photos zako na kiji-profile kidogo ili uuze ndani ya MNM Blog,tumia bizzo4shizzo@ymail.com au renatuskiluvia@ymail.com halafu mpango mzima j5 ijayo.

KAKA PUNGUZA ILE KITU YA "BOB"...

BOBY WINE
                                                                  
"The gheto president" Boby Wine inasemekana wiki iliyopita alikimbizwa hospitali moja jijini Kampala baada ya hali yake kubadilika ghafla na baada ya kupimwa ikagundulika jamaa ana malaria na madaktari kuamua kumlaza.Lakini habari za ndani kutoka kwa washkaji zake wa karibu aliokuwa aki-hang nao siku hiyo wanasema mchizi alikula ile kitu ya "bob"(bangi) kwa kiwango cha juu sana,inawezekana alikuwa na malaria kweli lakini kiwango cha "mboga" aliounguza that day ndo iliifumua malaria hiyo,so brother kama fanya kupunguza hivi coz kwani unashindana na nani??

Tuesday, May 18, 2010

HABARI NJEMA....


Hizi ni habari njema kwenu wadau wa blog hii ya burudani MNM,blog yenu inazidi kuboreshwa zaidi na zaidi,sasa twaweza kuchat kupitia blog hii,upande wa kulia wa blog kuna chat room kwa ajili yenu fans kufanya chochote mtakacho,isipokuwa matusi tu ndo hayahitajiki,pia kuanzia sasa tutakuwa na "video ya wiki" upande huo huo wa kulia wa blog,waweza kuclick na youtube itafunguka nawe kuweza kucheki hiyo video yetu ya wiki,na kuanza,leo tunaanza na video inayobamba kinoma ya mwanadada kutoka "Young MONEY" Nicki Minaj,kitu inaitwa "Massive Attack",ENJOY!!

"THIS IS IT" IN STORES NOW....

THIS IS IT(POSTER)
                                               
Mzigo unatoka "KANUMBA THE GREAT FILMS" na ni movie ya kwanza kutoka ndani ya kampuni hiyo ya Kanumba mwenyewe,nakukumbusha kitu,movie zote ambazo jamaa alikuwa anazifanya awali zilikuwa zinatoka "GAME 1st QUALITY TZ LTD".Hii ni moja kati ya project zake mwenyewe nje ya Game 1st Quality Tz Ltd na zingine zinakuja kibao tu,iko kitaa hivi sasa na kwa taarifa nilizonazo inauzwa kama pipi,hebu fanya kujichukulia copy yako fasta kabla mzigo haujakwisha,mimi weekend hii nitatulia home kuutumbulia macho,nione maujanja ya mchizi.

Monday, May 17, 2010

SOMO ZAIDI LINAHITAJIKA KWA WASANII WETU JUU YA HIZI TUNZO.

ALI KIBA
                                                       
Nimesikitika sana kwakweli na kujiuliza mengi sana,hivi sanaa yetu ya muziki inakwenda wapi jamani??Kama wasanii wetu ndio hawa ambao vichwa vyao ni kama vina mtindio ya ubongo??Mdau weekend hii iliyopita Tanzania yetu ilikuwa na tukio la kihistoria hasa kwa upande wa sanaa hii ya muziki,Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010,ni tukio ambalo kila mpenda burudani alikuwa karibu kuweza kujua kipi ni kipi upande huo na tumeshuhudia mengi,wa kuboronga ukumbini tumewaona na mapungufu yaliyosalia kwa waandaaji wa tuzo tumeyaona pia,leo sitaki kuzungumzia sana juu ya yale ambayo nilipata nafasi ya kuyazungumza kwenye kipindi cha "tupo pamoja" cha TTV kabla ya tunzo zenyewe,leo naomba nizungumze juu ya maoni mbalimbali ya wasanii au wanamuziki wenyewe baada ya tunzo hasa wale waliokuwa katika vipengere(categories) mbalimbali ndani ya tunzo hizi,nimewasikia wengi,lakini mimi naona waandaaji wa tunzo hizi(TBL) katika miaka ijayo wajitahidi kutoa semina juu ya wasanii kukubali matokeo yoyote yatakayopatikana baada ya tunzo zenyewe.Mi naona wasanii wetu wengi hawana upeo kabisa juu ya mambo haya ya tunzo,msanii wa kibongo akishaingizwa kwenye category yoyote tayari anajiona keshachukuwa tunzo,hakumbuki kwamba huu ni ushindani wa yeye na wenzake kibao ambao pia wako katika category hiyo na kati yao wote yeyote anaweza kuchukuwa tunzo hiyo,inapotokea yeye asichukuwe basi inakuwa lawama mtindo mmoja na kutishia kujitoa katika tunzo za miaka inayokuja kitu ambacho mimi naona sio dawa,halafu kitu kingine msanii anatazama jina lake zaidi ya ni nini kilichomfanya aingie katika category fulani,eti kwa sababu yeye ni msanii mwenye kijina kidogo kimuziki  basi anataka abebe tunzo zote hata zile ambazo kiukweli ni ngumu kwake kubeba kwa mwaka huo.Mfano naomba nimzungumzie Ali Kiba,nimepata bahati ya kumsikia akihojiwa sehemu fulani akiziponda tunzo na kudai kuwa eti yeye alistahili kuchukua na anashangaa kwanini hajachukua.Ali Kiba alikuwa katika category mbili ambazo ni msanii bora wa kiume wa mwaka na wimbo wake wa "usiniseme" uliingia kwenye category ya wimbo bora wa afro pop.Sasa kimatokeo ni kwamba msanii bora wa kiume wa mwaka alichukua Banana Zorro ambaye kiukweli alistahili tunzo hiyo,Banana kwa mwaka mzima wa 2009 amesimama vizuri kimuziki na hakuna anayeweza kubisha katika hilo,Banana ni mwanamuziki ambaye kwa sasa haimbi kwa playback,anaimba live na anamiliki bendi yake mwenyewe ambapo anatumbuiza sehemu mbalimbali kila weekend,lakini pia Banana mwaka jana ameweza kuhit vizuri na wimbo wake "zoba" sambasamba na B-Band,sidhani kama kweli Ali Kiba alitegemea kumpiku mtu kama Banana katika category hiyo,Ali Kiba bado anaimba kwa kutumia Cd na kupiga vishoo vidogovidogo kwenye sebule za watanzania waishio ulaya na hicho tu si kigezo cha kumfanya awe msanii bora wa kiume wa mwaka.Ushindi wa category ya pili aliyowekwa Ali Kiba ulikwenda kwa wimbo wa Marlow "PiiPii",wimbo ambao hauna ubishi kabisa kustahili kuchukua tunzo hiyo,kwa kudhihirisha hilo basi tunzo hii si tunzo ya kwanza kwa wimbo huo ni tunzo ya pili,ya kwanza ilipatikana toka Kenya,sasa Ali Kiba alitegemea kweli "usiniseme" umfanye yeye achukuwe tunzo hiyo??ni habari ya kuchekesha kidogo,wimbo wenyewe una video mbovu mwanzo mwisho,na video hiyo ilipata airtime sababu yeye ni Ali Kiba na si kingine,na tukizungumzia hit,wimbo wenyewe hauku-hit kivile kama ulivyokuwa "PiiPii" wa Marlow zaidi ya kuhit'ishwa kilazima na wanaojua promo.Kutokana na hilo basi mi naona msanii kama Ali Kiba na wengine wenye vichwa vigumu wanatakiwa wapewe darasa kabla ya kilele cha tunzo zenyewe ili wasizungumze "utumbo" wao wanaouzungumza hivi sasa,kuna mifano mingi lakini kutokana na muda naomba niishie hapa ili mengine mengi wayazungumze wenzangu wanaokerwa na ishu ka' hizi,chiaooo!!!!

"THANK ME LATER" HAIKO KI-BUSSINES-DRAKE


Sijajua bado tatizo ni nini,sijui ni kutokujiamini ama lah,Drake anayetegemewa kudondosha mzigo wake mpya tar 15 ya mwezi ujao unaokwenda kwa jina la "Thank Me Later" amelonga katika moja ya interview zake kuwa albam hii haiko kibiashara kivile japo itauzwa kama kawa,sijamuelewa mchizi ana maana gani kusema hivyo coz hivi sasa yuko na ma-interviews ya kumwaga katika kuipromo albam hiyo,hebu ngoja tuone....