BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Saturday, June 12, 2010

SORRY KWA UKIMYA FAN....NI BATA TU....

Inakuwaje fans??naamini mko pouwa ile mbaya na weekend iko sawasawa,najua wengi mko busy kwenye Tv zenu mkifuatilia mpango mzima wa World Cup pande za kwa MADIBA,sio ishu,mzee wa MNM niko safi kabisa,msione kimya jamani,haya ni mambo ya bata ndogondogo na kubadili mazingira,kwa sasa niko Iringa na mpango mzima ulianza hivi.....


Hapa tuko maswahiba watatu,Arnie Gizzle,mie mzee wa MNM  katikati na mdogo wetu Mark Mgeja,hapa ni baada ya break fupi ya msosi maeneo fulani ya Ruaha M'buyuni mwendo mfupi kabla hatujaingia Iringa town kula bata......


Hapa niko na mdau wangu wa masuala ya burudani,anaitwa Fransic Godwin,ni mwandishi wa habari maarufu sana pande za Iringa,kama zali vile tulikutana katika safari yetu tukaona sio ishu tukipata kitu cha kumbukumbu....


Huu ndio mchuma uliotufikisha salama salmini Iringa,tunamshukuru sana dereva kwa kuwa makini na kutufikisha poa kabisa....ajali nyingi sana siku hizi.....

Thursday, June 10, 2010

THE DREAM AACHIA VIDEO MPYA...."MAKE UP BAG"

THE DREAM

Jana mdau na fans wa MNM Blog nimebahatika kuiona video mpya ya mchizi hapo juu The Dream kwa mara ya kwanza ikirushwa hewani(premiered),ilikuwa katika 106&PACK Show ya BET katika segment yao moja yaitwa "World Premier" ambayo hucheza videos kwa mara ya kwanza kabisa,ngoma ya jamaa yaitwa "Make Up Bag" na ndani kamtupia mtu mzima T.I,ni kutoka kwenye mzigo wake unaokwenda kwa jina la "Love King",ni kali kwakweli.

MTAMBUE HUYU....."TARAJI P. HENSON".

TARAJI PENDA

Ni Taraji P. Henson ambaye alizaliwa Sept 11 1970,wkt nchi yake ikiadhimisha kumbukumbu ya kulipuliwa kwa Trade Centre,yeye mdada anasheherekea birthday yake,ni actress na mwimbaji pia,alizaliwa Northeast Washington DC,mama yake ni Bernice Gordon na baba yake ni Boris Henson ambaye ni US marine na mmiliki wa kampuni yake mwenyewe ya mambo ya fabrication,alilelewa na bibi na babu yake huko Southern Maryland,alisoma Oxon Hill High School na baadae NC A&T ambapo alisomea ufundi umeme na baadae akahamia Howard University,akashinda tunzo ya Triple Threat halafu akaja ku-graduate degree ya Theatre Arts palepale Howard University.


 
KTK POOSE

Taraji ana mtoto mkubwa wa kiume Marcel ambaye alimzaa mwaka 1994.Taraji ameshatokea kwenye muvi kibao tu kama Bad Boy I(2001) "Four Brothers"(2005),"Talk to me"(2007),"Smokin' aces"(2007),"The family that prays" ya Tyra Perry(2008),"Not easily broken"(2009) na "Hurricane season"(2009).Mbali na muvi zote hizo Taraji pia ameshatokea katika michezo kibao ya jukwaani kama "The curious case of Benjamin button" ambapo alitumia jina la Queen na mama yake na Benjamin ambao ulimfanya akawa nominated katika tunzo za Oscar kama "The Best Supporting Actress".Pia ameshafanya vipindi vingi tu vya Tv kama "Lifetime", "The Division" na ABC's "Boston Legal" kwa msimu mmoja.Sio hizo tu pia alitokea kama Angela Scott kwenye ABC's tv show "Eli Stone"(dec 2008),Fox tv show "House"(2005) na CBS's tv show "CSI"(2006),halafu katika episides kadhaa za "Sister,sister".

THE BEAUTY TARAJI

Kimuziki sio kivile sana,ametumbukiza vokoz katika track "Its Hard out here for a pimp" ya Three 6 Mafia,ngoma iliwini Academy Award kama Best Original Song(2006) ambapo pia alipata nafasi ya kuuimba wimbo huo katika kilele cha tunzo za Oscar March 5 2006 akiwa pamoja na washkaji wa Three 6 Mafia,mbali na yote hayo pia Taraji ameshawahi kutokea katika videos za wasanii kibao tu,mfano "Testfy" ya Common(2005),alitokea kama mke wa jamaa aliyetaka kuuawa,pia kwenye "Just like Me" ya Jammie Fox na T.I.Huyu ndio TARAJI PENDA HENSON.MTAMBUE sasa.

TARAJI P. HENSON


UJUMBE WA PRODUCER KWAME KWA MAPRODUCER WA KIBONGO..

KWAME

Mchizi ni mkali,na ninaposema ni mkali ninamaanisha ni MKALI kwelikweli,anaitwa KWAME,ukisikia hili jina kwa mara ya kwanza waweza fikiria labda mchizi ni m'bongo,au kama si m'bongo basi labda atakuwa kutoka Afrika Magharibi vile,ni producer ambaye juzi kati amezungumza kitu nikaona sio ishu,inaweza kuwasaidia maproducer wetu wa kibongo au wale wenye ndoto za kuwa maproducer baadae,ni kwamba mchizi kasema kazi ya music production kinachomata ni "OUTPUT" ya producer mwenyewe na  wala haichangiwi na wingi wa mashine azitumiazo producer huyo,mfano ni kwamba ukisikia ngoma kali basi jua si lazima studio au producer aliyefanya ngoma hiyo awe na mashine nyiiingi pale studio,akaongeza kwamba producer aweza kuwa na laptop tu na akafanya bonge la beat la kushangaza ulimwengu huu wa MUSA.So ushapata jibu sasa,wale wanaodata na wingi wa mashine studio huku output ikiwa POOR litazameni NENO la jamaa,ni KWAME.

Wednesday, June 9, 2010

TOMORROW ON "MTAMBUE HUYU"......TARAJI P. HENSON

TARAJI P. HENSON

MNM MEETS.......BANDAGO NIXON HAULE...

BANDAGO HAULE

NAME;BANDAGO NIXON HAULE

NICK NAME;BANDAGINYO

OCCUPATION;PRESENTER/RAPPER

LOCATION;MBEZI BEACH

AGE;25yrz

HOBBIES;MUSIC,MOVIES,COMEDIES,OUTING etc.

OLD SKOOL...UNAWAKUMBUKA HAWA??...

TOTAL

Wanaitwa TOTAL,kundi lililofanya vizuri sana miaka ya 1994-2000,kutoka New York na walikuwa wanafanya R+B,Hiphop and Soul,na lebels walizokuwa wanafanya nazo kazi ni Bad Boy/Arista Records,lilikuwa linaundwa na Keisha Spivey,Pamela Long na Kima Laynor,kwa sasa Keisha ni mama wa familia,aliolewa na muigizaji Omar Epps(mcheki ktk JUICE) mwaka 2004 na wanaishi Califonia na tayari wana watoto wawili binti K'marie(2004) na wa kiume Amir(2007),Pamela yeye anaishi New Jersey,ni memba wa Agape Family Worship Centre iliyoko Rahway,NJ,AMEOKOKA,na sasa anatayarisha albam yake inaitwa "Undeniable" ambayo itatoka mwaka 2011 na Kima tayari yuko katika ngoma ya mdogo wake rapper Vita "what u want".Total itarudi soon coz wako kwenye mazungumzo ya kulirudisha kundi,so kama umewamiss wasubiri....

Tuesday, June 8, 2010

ITS EMINEM ONCE AGAINNN PIPOOOO!!!!!......

RECOVERY (KWA MBELE)

Mchizi jana kaachia mkono mpya kabisa na ndo nimetoka kuusikiliza sasa,ni mnoma joh!ni mnoma bana!yuko na PINK na mkono waitwa "Won't back Down",huu ni baada ya "Not Afraid" ambao ukoo juu kama ndege,album inadondoka kitaa rasmi tar 22 mwezi huu,usikonde ntakuja kuipitia hapa katika "album of the week" halafu nkujuze ikoje,kama kawa covers zake huwa za kiubunifu zaidi,cheki hii hapo juu(kwa mbele) halafu chini(kwa nyuma).RECOVERY by Eminem...Coming Soon..

RECOVERY(KWA NYUMA)


HAPPY B'DAY KENEEN IVORY WAYANS......

KENEEN IVORY WAYANS
Yap!yap!yap!ni brother hapo juu,anaitwa KENEEN IVORY WAYANS,toka ktk familia yenye vipaji,ya waigizaji,akiwa kama brother mkubwa anaeongoza familia ameweza kufanya mengi kama muigizaji katika movies mbalimbali,wadogo zake DAMON WAYANS,SHAWN WAYANS na MARLON WAYANS pia wako tight ile mbaya katika upande huohuo wa movies japo Shawn na Marlon wao wanafanya zaidi comedies.

DAMON WAYANS
Jamaa waweza mpimia katika "Scary Movie", "The Most Wanted"(amekamua balaa) na "The Glimmer Man",hizo ni baadhi tu,zipo zingine kibao,Shawn na Marlon wako katika movies kibao pia kama "Above the Rim"(na mtu mzima PAC) na kazi yao poa sana yaitwa "Little Man"(lazima uvunje mbavu sana) ambayo brother(Keenen) kai-direct mwenyewe,na mapema sana walishawahi kutamba na comedy yao walioiita "The Wayans Brothers Show".Damon waweza mcheki katika "Wake Up,This is America" na "Leaves the Palladiums".Nionavyo mimi Keneen na Damon wamefanana sana,halafu Shawn na Marlon pia wamefanana sana.

WAYANS BROS(KENEEN,SHAWN,MARLON&DAMON)

Basi mdau kama washeherekea birthday yako leo nakujuza kuwa una-share birthday na Brother mkubwa kutoka familia hii ya Wayans na muigizaji maarufu KENEEN IVORY WAYANS ambaye alizaliwa tarehe kama ya leo,mwezi kama wa leo mwaka 1958.Happy B'day Brother.