BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, September 23, 2010

HAYAWI HAYAWI SASA.....KIBOKO CHA ORIGINAL KOMEDI HIKI HAPA...LEO USK

ZE COMEDY SHOW

Leo pale kati show hii inaanza..kupitia "The # 1 youth channel" EATV..washkaji wamesota sana..kwa muda ambao ungekuwa wewe ungeshakata tamaa..ila kuanzia leo ni bata tu coz show ndo itakuwa kwa hewa..tusubiri tuone kama je ni kiboko kweli cha Original Komedi waliokuwa hapa na sasa bata zinaliwa TBC 1??Jibu unalo wewe mwenyewe...

COMING SOON..."PINK FRIDAY" BY NICKI MINAJ

"PINK FRIDAY"(COVER)

Baada ya kugonga copies kibao na mzigo wa kwanza "Massive Attarch"....Nicki Minaj toka lebel ya Young Money sasa anashusha mzigo mwingine matata sana "Pink Friday"...Huu ni mzigo wake mpya kabisa ambao mpaka sasa bado hajatambulisha mkono hata mmoja toka humo ndani...ni juzi tu ndo ametamka rasmi jina la mzigo wenyewe na kutambulisha official cover(kama unavyoona)..Mzigo utadondoka kitaa rasmi Nov 23 mwaka huu..nausubiri ile mbaya..

KIDBWOY AENDELEA VZR..AHAMISHWA WODI..

KIDBWOY

Wadau na fans wengi walitaka kujua mchizi anaendeleaje..baada ya kuripotiwa kuvamiwa na kuumizwa vibaya na mtu asiyefahamika anayesadikiwa kuwa ni msanii....Mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa TETEMESHA Records ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Free Africa ya Mwanza Sandu George Mpanda al-maarufu kama KidBwoy kwa sasa hali yake inaendelea vzr..ameweza kuzinduka na kuzungumza japo kidogo baada ya kuwa nusu kaputi kwa zaidi ya masaa 15 baada ya tukio...ila habari mpya zinasema mshkaji imebidi ahamishwe wodi ili kuhepuka usumbufu wa fans kibao ambao daily walikuwa wanajitokeza hospitali ya Bugando alikolazwa kwa nia ya kumjulia hali na kutaka kupigapiga nae stori ishu ambayo madaktari wake wamesema si salama sana kwa sasa coz anahitaji mapumziko zaidi...awali alikuwa wodi no C 606 ghorofa ya sita...kwa sasa amehamishiwa wodi ambayo bado haijawekwa wazi ili apate mapumziko na kuharakisha kupona kwake...Get Well Soon Kid.

HAPPY B'DAY JERMAIN DUPRI...

JERMAIN DUPRI

Mdau leo tar 23 Sept ni siku ya kuzaliwa kwa mmoja kati ya watayarishaji wakali nnaowaaminia wa muziki nchini Marekani Jermain Dupri...so mchizi anasheherekea siku yake leo..kama nawe ni B'day yako leo fahamu kuwa unashea b'day na star huyu...Happy B'day Jermain Dupri..

Tuesday, September 21, 2010

OLD SKOOL....."H-TOWN"...

H-TOWN

F.A NA AMANI NDANI YA B_HITS...

F.A

Habari zinasema mwanamuziki Amani kutoka Kenya wiki hii atatimba ndani ya jiji la Lukuvi kupiga bonge moja la show la East African Bash na wakati huohuo kupata wasaa wa kuingiza vokoz kwenye bongebonge moja la beat la mtu mzima Pancho Latino pale B_Hits ili kukamilisha mzigo mpya wa Hamis Corleone Mwinjuma aka F.A..sasa mimi na wewe tuusubiri tuuone au sio..

AMANI