BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, January 28, 2011

HAPPY BIRTHDAY BIG BRAH!!!


Happy Birthday kaka...but tambua kuwa nimekuzidi siku kumi na moja..teh teh teh!!Edwin Bashir aka Cuzin!!

ON "KIJA'S 15" THIS FRIDAY......


 On "Kija's 15" ijumaa hii...ni movies..movies..movies..za Bongowood and Hollywood...kibongobongo nazungumza na mchizi ambaye siku za nyuma alikuwa akijishughulisha na u-dereva wa taxi ambayo ni kama ameupotezea kwa sasa...na kutokana na hilo anaelezea jinsi game linavyolipa kwa sasa..anaitwa DAUDI MICHAEL TARIMO...msikilize pia yeye...


 Kimbelembele wiki hii nimeamua kucheki na movie ya kimalavidavi hivi...mzigo unaitwa "NO STRINGS ATTACHED"...mzigo ni mkali mwanzo mwisho...unaonesha namna ambavyo unatakiwa ku-behav pale mtu uliyekuwa nae kimapenzi anapoamua kuwa na mtu wako wa karibu...ni mzigo unaodhihirisha kuwa uhusiano wa kawaida kwa waliowahi kuwa "inlove" inawezekana.


Saa 10;30 jioni ya ijumaa hii...ndani ya "VUTA PUMZI" show ya BonSly..Ebony fm ndo mpango mzima..usiikose hii..

 

Thursday, January 27, 2011

NAWALETEA KWENU MANENO YA ATHMAN MUSSA "MWALUBADU"



“Ninataka kuwaonyesha raia kuwa kazi naweza hata peke yangu  ndiyo maana nimemua kucheza komedi fupi yenye maana na inakwenda ZIFF kuonyeshwa huko katika tamasha kubwa zaidi mwezi wa saba, lengo langu kwa sasa ni kuwa muigizaji wa kimataifa”

Mwalubadu amesema kuwa anatarajia komedi hii kuwa ni tofauti kabisa na komedi ambazo amekuwa akionekana kwa sababu nyingi huwa hatungi yeye bali ushirikishwa tu lakini hii mtunzi ni mwenyewe,
Ntafanyia huku huku  Iringa kwa mara ya kwanza natolea mzigo huku.

Monday, January 24, 2011

IN "CAMPASS CONNECT" TONIGHT...


Ni bonge,bonge la latenyt show ambalo hutakiwi kulikosa...leo usiku..ktk "brokenheart" segment utasikia story ya kuumiza ya dada mmoja anaitwa Joyce...utamshauri pia ukipenda..na "Monday Love" leo topic inasema...unaamini katika love at the 1st sight ??kwamba inawezekana tu eti ile mara ya kwanza kumuona mtu then uka-fall papo hapo??au ni tamaa??ni mjadala mzuri ambao hakika utakufaa sana...



katika tafsiri ya nyimbo leo niko na rekodi kali ile mbaya.."I was Made to Love u" by Gelard Levert..utaisikia maana yake kwa kiswahili...yote ni katika "Campas Connect" leo j3..saa 4;00-6;00 usk..kupitia 106.5 Mlimani redio..."Elimu Kwanza"

Thursday, January 20, 2011

STARTING TOMORROW..MY NEW SEGMENT IN "VUTA PUMZI" SHOW ON EBONY FM


Ni dakika chache sana kwa kuzifikiria kikawaida kichwani..but ni nzito na muhimu sana kwa ajili ya kuifungua weekend yako...ni segment yangu mpya itakayoanza ijumaa ya kesho na kila ijumaa ndani ya "Vuta Pumzi" show..si pengine ni EBONY fm (87.8..Iringa, 88.2..Moro&Dom na 94.7..Mbeya).."KIJA'S 15" ni live from Dar es Salaam Tanzania na hutakiwi kuikosa...bila hii bado hujaanza Weekend,itakuwa na nini ndani??bado ni surprize!!!

Tuesday, January 18, 2011

IN R&B THANG....CHICO DEBARGE!!


Jina halisi ni Jonathan Athur..ambaye alizaliwa June 23 1966 Detroit Michigan US..ni mdogo wake na mmoja kati ya memba wa Motown Family Act Debarge...alianza kuimba miaka ya 80's akiwa chini ya Motown  na albam yake ya kwanza "Chico Debarge"
 ilibeba hit "Talk to Me"..hii ilitoka 1986...baada ya hapo ikafuata album ya pili "Kiss Serious" mwaka 1988...bahati mbaya akafungwa jela kutoka na dili za dawa za kulevya..akapotea kimuziki na akaachiwa katikati ya miaka ya 90's...



 Akarudi Motown na akafanya albam "Long Time No See" mwaka 1997 ikafuata "The Game" mwaka 1999 na hakukaa sana akaondoka na kuhama lebel...akahamia Koch Records ambapo akaachia mzigo "2003's Free"...album ya sasa inaitwa "Addiction" ambayo aliiachia July 14 2009 chini ya Kedar Entertainment Group...mchizi ana watoto watano na tyr amekwisha mpa talaka mkewe aliyemzalia watoto wanne coz mtoto wa tano alizaa na mwanamuziki na muigizaji Nona Gaye.Its R&B Thang!!Kazi imeanza!!

MULT-TALENTED DUDE..SKY WOKA WE NI NOUMER..


Nafahamu kwamba b4 hajaingia ktk utangazaji alikuwa mmoja kati ya ma-MC wanaoogopeka sana Musoma town pale..but baada ya kuingia katika utangazaji ikawa kama imesahaulika vile..naona sasa anarudi mdogomdogo coz mara ya mwisho nilimsikia akichana katika track ya kwanza kbs ambayo huwa haitajwi(sijui ni kwanini) ya Hussein Machozi "Samahani" aliyoifanya pale Tetemesha na mikono ya Kid ikahusika sana...baadae nikaja nikasikia bonge bonge moja la track yake mwenyewe aliyofanya na Farida "Ree Kay"(sijui iliishia wapi ile) pale pale Tetemesha...Anaitwa Fredrick Bundala aka Sky Woka..sasa ana mikono miwili mikali sana..kinachonivutia ni namna anavyofanya muziki wake...mfano hii ya sasa swahili version ya "Am coming Home" ya Diddy Dirty Money" ni noumer..Sky we ni mkali sana...but naomba uendelee kufanya muziki huohuo unaoufanya sasa..don't change man.

Monday, January 17, 2011

ITS MY BIRTHDAY....NA KAZI NDO INAANZA 4 2011..


Ni kitambo kirefu najua mlinimiss ile mbaya...mlimiss vitu ambavyo naamini katika kipindi chote ambacho sikuwa hapa mmeshindwa kuvipata sehemu nyingine yopyote...na ndo maana nimekuwa nikishuhudia IDADI ya wahudhuriaji ikiongezeka japo sikuwa natupia chochote hapa...KIUKWELI mmenipa MOYO sana na nimeamini ninyi ni funs wa UKWELI sana kwangu na MNM kwa ujumla..THANX SO MUCH...sina cha kuwalipa kwa namna yoyote tofauti na kurudi kwa NGUVU zote kuwapa kile mlichokimis...am HERE NOW..nipokeeni jamani...leo ikiwa ni SIKU yangu ya KUZALIWA naitumia kukupeni taarifa kuwa now MNM is alive..tuendeleeni kupashana hili na lile...infos hapa ndo mahali pake..4 anything check nami katika mail yetu ileile bizzo4shizzo@ymail.com....au inbox me kwenye facebook...www.facebook.com/renatuskiluvia...au kiurahisi gonga pale palipoandikwa "niko huku pia" pembezoni mwa blog hii...THANX!!

BEST COMEDIAN FOR 2010..ATHMAN MWALUBADU..


Ni mchizi wangu na workmate wangu pia...nami huwa nikikutana nae tu naanza kupasuka mbavu kabla hata hajaongea wala kusema chochote..nilijua huku atafika..anaitwa Athman Musa Mwalubadu..mchekeshaji na mtangazaji wa Ebony fm(the no oneRadio Station in Southern Highland )...ambaye juzi kati amenyaka tuzo ya mchekeshaji bora wa mwaka 2010 toka Film Central Awards ambazo zilitolewa na mtandao maalum wa kutangaza kazi za filamu hapa Tanzania ujulikanao kama filmscentral.co.tz....na hii imempatia tunzo Mwalubadu ambaye hajashiriki comedies nyingi kivile sana kama wachekeshaji wengine tunaowaona kila siku...Big Up Bro...naamini safari bado INASONGA..na wataisoma namba au sio???

Wednesday, December 22, 2010

KIMYA KINGI??....MNM NEW SEASON COMIN' SOON 2011...

Naweza sema ilikuwa ni kipindi kirefi na kimya kirefu sana japo nilikuwa nadondosha vitu kimachalechale sana...but now fans wa MNM Blog kaeni tyr kwa msimu mpya wa 2011...kama kawa kama dawa wale woote ambao mlimiss ishuz kibao...kama ma-infoz na ishu ka hizo stay tuned..narudi upya kabisa na segments za hatari na infoz za kumwaga..hiyo ni katika msimu mpya wa Muziki Na Maisha Blog 2011..MNM "here we stay"....

Wednesday, December 15, 2010

TRUE LOVE IS HERE "CAMPAS CONNECT"...



Campus Connect” is the romantic late night radio show…aired on 106.5 Radio Mlimani of Dar es Salaam University @ 22;00pm-00;00am in every Mondays and WednesdaysShamimu Mlacha aka Shaney is the host of this show..”Campus Connect” talks about love and relationships, building love awareness to youths and adults, teach people how to behave in love and to forgive…”Campus Connect” is the place of comfort to broken hearted people…slow jams, soul music & all good music here is the place to be…This is ”Campus Connect”…we believe in TRUE LOVE.Lets be there!!For anything please use contacts below….Don't u ever miss this show...



Contacts;


Email;shamimumlacha@yahoo.com


www.facebook.com/campasconnect

Thursday, November 25, 2010

HAPPY BIRTHDAY MY GOOD FRIEND ISSABELAH WA V-fm

ISABELLAH NSHAMA

Leo tar 25 Nov ni siku nzuri na ya furaha kwa rafiki yangu wa ukweli...Isabellah Nshama wa Victoria fm ya mjini Musoma..wengi walitamani wafikie umri ulionao wewe but ilishindikana..hongera sana na MNM inakutakia birthday njema..we wish u to blow a lot of candles one day...Happy Birthday Isabellah..

Friday, November 19, 2010

IN THE MAKING OF THE MOVIE...(JINA KAPUNI).....PT I










HAPPY BIRTHDAY MY YOUNG SIS NEMY NIQY..

NEEMA KILUVIA aka NEMY NIQY

Leo Nov 19 ni siku muhimu sana kwa familia ya Mr&Mrs Kiluvia,coz kitinda mimba aka mziwanda aka lastborn Neema Kiluvia aka Nemy Niqy anakumbukia siku yake ya kuzaliwa..mimi kama brother na kwa niaba ya wana familia wote..namtakia birthday njema,Mungu amsaidie atimize yale yote anayoota kila siku...Happybirthday Ney..

Saturday, November 13, 2010

Monday, November 8, 2010

MBEYA...KAZI IMEANZA..NI EBONY FM PEKEE...

Ki-historia ni muziki ambao inasemekana haujawahi kutokea..but Ebony fm imebadili kabisa hali ya hewa ya burudani jijini Mbeya...MTIKISIKO 2010 "bata mreeefffffffff" sana ameliwa Mbeya jumamosi ya wiki iliyopita..ilikuwa ni noma..kwa udhamini wa VodaCom Tanzania,Kilimanjaro Premium Lager na PSI Tanzania...tazama down hapa>>>>

Muonekano wa stage wakati ikifungwa mchana...ni Ebony Entertainment banaaaa.......


Na hii ni namna ambavyo stage ilikuja kuonekana usiku mnene kwenye bataaaa....


Akhsanteni Mbeya kwa kutusapoti....here we are na burudani zitakuja zaidi na zaidi na zaidi


Visigino vya Twanga vilisuguliwa kama kawa...Twanga Pepeta on stage..


Linah kutoka THT..akiwakilisha kama kawa kama dawa pale kati..


Juma Kassim Kiroboto aka Juma Nature..mmoja kati ya wasanii wasiochuja hata kama hana ngoma mpya redioni..huu ndio ulikuwa moto wake..."msichana mtundu,msichana mtundu,msichana mtundu.".



Dj Mubba "the proffessional" on the wheel of steel...schrachings!!
Sasa mpango mzima ni Jmosi hii Iringa town katika viwanja vya Samora...MTIKISIKO 2010.."bata mreeeeeeffffff" tutaendelea kumla pale..usiikose..

Friday, October 29, 2010

EBONY FM..HERE WE COME AGAIN..MTIKISIKO 2010.

STAGE ON CONSTRACTION

Mwaka wa nne now...tamasha lilianza since 1997...Bigtime Highland Company Ltd na Ebony Entertainment....kupitia d' hottest radio stations never appeard on Earth...Ebony fm n' Hot 89.5fm..wanadondosha only a single but rememberable East African Music Festival day...almaaruf "MTIKISIKO"..its once upon a year...na mwaka huu ni MBEYA & IRINGA regions...this year it goes with the slogan "bata mrefffff!!!"...Artistslist ni ndefu balaa...but special appearance ni ma'men WEASEL&RADIO from Kampala n' one&only sexy lady all the way from Naiii...called herself WAHU...hii ni kwa uchache tu..sticky around with MNM for more info....

WAHUU WITH HUSBAND NAMELESS

Tuesday, October 26, 2010

BAADA YA JADEN....NOW SMITH'S FAMILY PRESENTS...WILLOW SMITH..

WILLOW SMITH

Hii ni baada ya familia kumsapot na kufanikiwa kumtoa first born wa Jada Pinket Smith...Jaden Smith katika movie Karate Kid now Smith's family inamtambulisha kwenu last born wa Will Smith...Willow Smith..lakini sasa sio katika movie tena..ni katika muziki...jana nimebahatika kutazama 106&Pack na Willow alikuwa anatambulisha singo yake ya kwanza "Whip My Hair"...ni bongebonge moja la track...ni njia nzuri kwake na ni dalili za kuja kuwa moto ile mbaya..sasa je wazazi wa kitanzania twajifunza nini kutoka Smith's family???

SMITH'S FAMILY WAKIINGIA KWENYE STUDIO ZA BET

PIGO JINGINE IN REGGAE MUSIC...GREGORY ISAACS HAS GONE FOR GOOD...

GREGORY ISAACS

Ni kifo cha Jamaican Reggae Icon Gregory Isaacs kilichotokea jana asubuhi nyumbani kwake London Uingereza..baada ya kuugua kwa muda mrefu sana ugonjwa wa ini kushindwa kufanya kazi..Meneja wake Copeland Forbes amethibitisha kutokea kwa kifo hicho...amefariki akiwa na miaka 59..alizaliwa July 15 1951 huko Fletcher's Land Kingstone Jamaica na alianza rasmi kurekodi mwaka 1960...na ndipo kabla ya mwaka 1970 akachomoza na hit kali zilizomtambulisha kama "Love is Overdue" na "All I have is Love"....mimi nilimtambua zaidi katika "Night Nurse"...MUNGU ailaze roho ya marehemu Gregory Isaacs mahali pema peponi..Aamin!!

Tuesday, October 12, 2010

ZINANIKUMBUSHA MBALI...."BROWN SUGAR" BY D' ANGELO..

"BROWN SUGAR"

Released July 3, 1995

Recorded 1994–1995
Battery Studios, RPM Studios
(New York, New York)
Pookie Lab
(Sacramento, California)
Genre R&B, neo soul, soul, funk
Length 53:17
Label EMI
Producer D'Angelo, Kedar Massenburg (exec.), Ali Shaheed Muhammad, Bob Power, Raphael Saadiq
D'Angelo chronology
Brown Sugar
(1995) Voodoo
(2000)
Singles from Voodoo
1."Brown Sugar"
Released: August 1, 1995
2."Cruisin'"
Released: October 12, 1995
3."Lady"
Released: February 20, 1996
4."Me and Those Dreamin' Eyes of Mine

ALI KIBA HUYOOO...INTERNATIONALY...

ALI KIBA

Awali nilipopata taarifa kuwa Ali Kiba ameachana na management ya awali chini ya G-Records ya mtu mzima Gulu aka G lover nilihuzunika sana...na nikaona sasa kijana amepotea na muda si mrefu tutamsahau...aisiii..i was wrong...very wrong bana...kijana juzi kati ame-sign na kampuni ya kimataifa ya "RockStar4000" yenye uhusiano na Sony BMG ya nchini Marekani na soon ataanza kusikika kimataifa zaidi...kazi ya kwanza ya kampuni hiyo kwa Kiba ni kusambaza nyimbo zake za albam zake mbili za kwanza kimataifa zaidi... na mengine tutajulishwa...hii ni akili jamani au sio??kila la kheri mwana!!

RAY&KANUMBA IN THE BATTLE ONCE AGAIN....

"PRETTY GIRL"(COVER)

Hii ni mara ya pili kwa wasambazaji wakubwa wa filamu za kibongo kampuni ya Steps Entertainment kulifanya hili....kuingiza sokoni kwa wakati mmoja filamu mbili za magwiji wa filamu nchini...Ray Kigosi na Stiven Kanumba...na ile ya kwanza niliiripoti hapa pia..sijui matokeo yalikuwaje kibiashara nadhani Steps wenyewe wanalo jibu...sasa this time ni "Pretty Girl" toka RJ Company na "Uncle JJ" toka Kanumba TheGreat Films...zote kwa wakati mmoja zitakuwa sokoni time yoyote kuanzia sasa...tuone tena "Nani ni Nani"..

Thursday, October 7, 2010

MAONI YA MDAU TAJI LIUNDI BAADA YA "BLACK SUNDAY" PREMIER..

BLACK SUNDAY(COVER)


Nilipewa DVD ya kuangalia kabla ya filamu kuzinduliwa na watengenezaji nikiwa ni rafiki na mshirika wao katika mambo kadhaa.
Nilisikitika mara tu nilipoanza na kujikuta naangalia filamu ambayo dhahiri ilik...uwa imeigwa. Kadri filamu ilivyoendelea, nilishtushwa na hadithi, maudhui na hata tamati. Vyote kwa sehemu kubwa vilitokana na filamu ya mwaka 2007 iliyotengenezwa Canada inaitwa BUTTERFLY ON A WHEEL.
(ANGALIENI PROFILE WALL KUONA TRAILER ZA FILAMU HIZI MBILI)
BUTTERFLY ON A WHEEL ni sawa na kusema KIPEPEO KWENYE GURUDUMU. Kama kweli unataka kumkanyaga kipepeo, basi gurudumu ni kitu kikubwa sana. Mantiki ni jina hilo ni sawa na kusema kwamba, 'jitihada kubwa mno inatumika kutimiza swala dogo sana"
Ndivyo zilivyo hadithi zote mbili. Mtekaji anatumia mbinu na kila jitihada kuwabughudhi wapenzi wawili kutwa, kwa sababu ambayo inabainika kuwa ndogo lakini nyeti. Ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
Black Sunday ina mapungufu mengi sana.Imeigwa.
Haina uhalisia, hata kama ni filamu ya kubuni. Kanumba kwa mfano anaonyesha bastola waziwazi, anawapa wahanga wake nafasi nyingi za kutoroka na labda kubuni mbinu za kumzidi.
Haiwezekani kutoa Shilingi 50+milioni siku ya Jumapili bila benki yeyote (Pilipili Bank?) kutaka kujua kwanini au kukudadisi kwa undani?i!Jinsi ya mtoto katika filamu inajichanganya!Mara binti, mara mvulana???
PLOT: haina nguvu, si ajabu kwani imeigwa na kuleta uhalisia wa Tanzania iliwashinda waandaaji.
Mf.Mlela na Yvonne hawana hata sumni mfukoni, lakini wanapotumwa kuombaomba hela, wanaonekana kufika hadi MJINI kutoka Giraffe Ocean View Hotel! Labda Mrwanda hataelewa sawa...
Uigizaji wa Kanumba sio mzuri. Anavituko vya "kitoto' sijui niseme? Kugonganisha meno, kula Big G na kuifanya iwe kama kitu cha msingi sana. Kiujumla SCRIPT yake ni mbaya. Hasemi lolote la maana kwa robo tatu ya filamu.Kuna umihimu wa kukubali STRONG CHARACTERS siku nyingine.
Mlela na Yvonne hawapati nafasi ya kuzungumza wala kuigiza haswa kwa zaidi ya robo tatu ya filamu nzima.Hata hivyo, filamu inaisha na matukio ya kushangaza akili za mtu mwerevu!
Hakuna utaalamu wa taa, SPECIAL EFFECTS, na LOCATION au utafutaji wa maeneo ulikuwa finyu sana!
Sijaelewa waandaaji wanawaza nini? Sifahamu kama waigizaji walifahamu kwamba walikua wanatoa kopi. Hawajajibu maswali yangu niliyotuma kabla ya kuandika haya.
Nashindwa kuzipenda sana kazi za nyumbani. Umakini, ubunifu na utungaji hadithi zenye kina unatuangusha.
Kitu kizito zaidi ni SOKO. Mlimani pale wanaenda watu wa tabaka la juu kuangalia kwa mfano INCEPTION. Matarajio yao ni kuangalia filamu za kiwango cha juu sana. Wanaweza kila wiki kuingia kuangalia filamu kwa Tsh 8.000-15 elfu!Kama panajiendesha na soko hilo tu peke yake, je kama rafiki yangu Kanumba angeweza kujitahidi kufikia viwango vya kukubalika na soko hili? Si angefaidika sana?
Soko la KWELI sio la VIDEO ni la MAJUMBA YA CINEMA. Uuuzaji wa video ni BAADAYE kabisa.Lakini hili ni somo la siku nyingine...Haya, nimenena. Ni matarajoio yangu kwamba wengi mtaona nimekuwa mkali kwenye maoni. Nimekuwa mkweli. Kama hukwenda kuiona, ione kwanza au inunue kisha pitia upya niliyoandika. Kwa wasanii husika, msinichukie, msichukie niliyoandika, hebu chukulieni maneno haya kwa fikra chanya.Naamini sisi ni marafiki na rafiki mwema ni yule ambaye haogopi kusema ukweli. Ukweli unauma. Ukweli unajenga.Naandika kuwafumbua macho na kuwatakia maendeleo. Hakuna fani yenye kukosolewa zaidi kama FILAMU. Nipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi katika mawazo. Natumaini waungwana wengine wataandika maoni yao nao.
Kila la kheri.
TajiSee More


Tuesday at 2:02pm · LikeUnlike

Tuesday, October 5, 2010

TONIGHT ON 106 & PACK @ BET...JEREMIAH IN THE BUILDING...

JEREMIAH

Leo usiku kwenye 106 & Pack ya BET...bongebonge moja la interview la mtu mzima Jeremiah...so kama vp cheki mida ya saa tatu kamili usiku kwa saa za kibongo...