BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, August 6, 2010

ZINANIKUMBUSHA MBALI..."THE DIARY" By SCARFACE

THE DIARY(COVER)

Anaitwa Brad Jordan kwa jina halisi..ambaye wakati analitumikia kundi la Gheto Boys(sio lile la Afande Sele wa Moro) alikuwa anatumia Akshen..alizaliwa Nov 9 1969 Houston US..Huu ni mzigo wake wa tatu baada ya kuamua kufanya solo projects(hakujitoa kabisa kundini)..wa kwanza ulikuwa "Mr Scarface is Back" wa 1991...halafu "The World is Yours(face II face)" wa 1993..."The Diary" ambao aliuachia Oct 18 1994 ni moja kati ya mizigo ambayo inanikumbusha mbali ile mbaya nikiusikiliza..na huwa nikitaka kupumzisha akili yangu baada ya "stress" za hapa na pale za kimaisha nausikiliza mzigo huu,haunichosi aisii..


MY HOMMIES(COVER)

Una mikono 13 ukijumlisha na intro na outro ambayo ni "The White Sheet", "No Tears", "Jesse James", "G's", "I see a Man Die", "One", "Goin' Down", "One Time", "Hand of a Dead Body", "Mind Playin' Tricks" na "The Diary"..Producers waliotia mautundu yao huko ndani ni Scarface mwenyewe, Mike Dean, Ice Cube, Unkle Eddy na N.O.Joe..Def Jam ndo lebel husika japo baadae mchizi akaamua kuanzisha lebel yake Rap-A-Lot Records,baada ya hapo mchizi akawa anadondosha tu mizigo mikali kitaa..kama


THE WORLD IS YOURS(COVER)

"Untouchable"(1997).."My Hommies"(1998).."The Last of a Dying Breed"(2000)..."The Fix"(2002)..."Balls & My Word"(2003)..."My Hommies Pt II"(2006) ambayo haikufanya vizuri kama alivyotegemea kitu ambacho kilimfanya aungane na marapa flani wadogo Young Malice na Willie Hen na kuachia "One Hunid" mwaka huohuo 2006 na mzigo wake wa mwisho ni "M.A.D.E wa 2007.Ama kweli cha kale dhahabu(The Diary). 

0 comments: