BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, July 2, 2010

"MTAMBUE HUYU".....THE LATE LYNDEN DAVID HALL

Jamaa alizaliwa May 7 1974 Wandsworth,South London,ni mwanamuziki aliyekuwa anafanya muziki wa Soul na Neo-Soul,lakini pia alikuwa mwandishi na mtayarishaji muziki(producer).Maelezo ya huyu mchizi sio marefu sana,mwaka 1999 Hall alikuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka U.K kupigiwa kura nyingi na kupata Best Male Artist,tunzo ambayo hutolewa na "Britain's Blues & Soul" magazine,mzigo wake wa kwanza "Medicine 4 my Pain" wa mwaka 1997 na mikono miwili mikali kutoka humo ndani "Do I qualify" na "Sex Cinderella" ilisumbua vibaya-vibaya na kujizolea mashabiki lukuki sio U.K tu bali dunia nzima.Naweza sema ndio mikono iliyonifanya hata mimi pia nikamfahamu huyu mchizi.

THE OTHER SIDE(ALBUM)

Mwaka 2000 Hall akaachia mzigo mwingine "The Other Side" ambamo ndani yake kulikuwa na mikono kibao tu iliyoshika na kusumbua mno.


LYNDEN DAVID HALL

Mwaka 2003 akatokea katika movie "Love Actually" ambayo ilichezwa na Keira Knightley na Chiwetei Ejiofor,humo ndani Hall aliimba katika harusi(ya kifilamu) ya mastaa hao,miaka miwili baadae akaachia albam yake ya tatu na ya mwisho "In Between Jobs" chini ya record lebel yake mwenyewe "Random Records",pia ni albam iliyoonesha mafanikio sana kwake japo naweza sema Lynden David Hall hakupata nafasi ya kuyafaidi mafanikio hayo,coz mwaka huohuo alianza kuugua sana kutokana na "cell transplant" alizowekewa Jan ya 2005,Lynden David Hall alipata ugonjwa wa "Hodgkin's Lympoma" Octoba mwaka 2003.14 Feb 2006 Lynden David Hall akafariki dunia mikononi mwa mkewe mpendwa Nikkie Hall,alifariki akiwa na miaka 31 tu.

MEDICINE 4 MY PAIN(ALBUM)

Muda mfupi kabla ya kifo chake akiwa hospitalini David Hall na mkewe walifanya tamasha lenye mafanikio(Lynden Wish Concert) ambalo lilifanyika London Jazz Cafe kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasaidia wenye matatizo,tamasha ambalo kwa mara ya kwanza liliwakusanya wanamuziki wote weusi nchini humo kwa ajili ya kuchangia fedha hizo ambazo pia zilitengeneza kitu kinaitwa "Lynden Wish Charity" ambayo iko mpaka kesho.May 23 2006 The African Leukaemia Trust waka-organize kumbukumbu ya kumkumbuka Lynden David Hall ambayo ilifanyika The Kensington Roof Gardens ambayo wanamuziki kibao wali-perfom,London Community Gospel Choir wakaimba wimbo "All You Need is Love" ambao David Hall aliuimba katika "Love Actually" movie,wimbo ambao uliwatoa wengi waliohudhuria machozi,Huyu ndie Marehemu Lynden David Hall,mtambue sasa...

HAPPY B'DAY MARY LOVE & YOU....

MARY LOVE

Una birthday leo??safi sana,basi unashea birthday na star huyu kutoka London U.K,anaitwa Mary Love,anafanya muziki wa R&B,Soul na Jazz,amezaliwa tar kama ya leo mwaka 1970,Happy B'day Mary Love na wewe pia...

Thursday, July 1, 2010

"MTAMBUE HUYU" KESHO...LYNDEN DAVID HALL...

LYNDEN DAVID HALL

Utamjua vizuri(nje ndani) huyu mjamaa,ila nikudokeze tu kuwa ni MKALI,MKALI ile mbaya...anaitwa Lynden David Hall....usiikose hii...

IN STORES NOW..."KARATE KID" THE MOVIE..

KARATE KID

Mzigo unamuelezea dogo ambaye maskani kabisa ni Detroit-Marekani lakini kutokana na mambo ya hapa na pale anasafiri na mama'ke na kwenda kuweka makazi Beijing-China,huko anakutana na madogo wenzake ambao wanajua hu!ha!(kareti) balaa..na katika hao madogo kuna mmoja anakuwa anamuonea sana coz yeye hawezi hizo ishu..kutokana na hilo dogo anakwenda kwa "karate master" na kuomba kufundishwa..sasa hebu pata picha kilichokuja kutoka baadae ni nini..hii ni movie mpya kabisa ambayo hutakiwi kuikosa,rasmi imezinguliwa tar 11 mwezi uliopita nchini Marekani.Tangu July 2009 mpaka Octoba 16 mwaka huohuo watu walikuwa busy waki-shoot mzigo huu huko pande za Beijing-China.

JADEN SMITH

Humo ndani yumo mtoto wa Will Smith anayekuja juu ile mbaya Jaden Smith...ambaye kaigiza kama huyo dogo anayekuja kufundishwa kareti,pia Taraji P Henson,kaigiza kama mamake na Jaden..na mtu mzima Jackie Chan..ambaye ndie kun fu master anayekuja kum-train huyo dogo..mzigo kau-direct Harald Zwards..producers ni Will Smith na wife wake Jada Pinket Smith na James Lassiter..imeandikwa na Christopher Murphey..mtunzi ni Robert Mark Kamen na inasambazwa na Colombia Pictures.Mdau original ya mzigo huu ni kutoka katika mzigo mwingine uliokuwa katika jina hilihili ambao ulitengenezwa mwaka 1984...hebu utafute uone dogo alivyofanya mambo huko ndani..ni mnona joh!!!

HUYU HAPA VALLEY....ZAO JINGINE KUTOKA THT..

VALLEY

Jina halisi anaitwa Valentino Michael,lakini awapo kazini(muziki) anapenda sana umuite "Valley",zao jingine kutoka THT(awamu ya kwanza),nilipomuuliza inakuwaje akachelewa sana kuja kwa mashabiki,akanijibu jibu moja fupi sana ambalo mimi nililielewa vizuri..."si unajua bro"....Sasa namtambulisha kwenu na soon utasikia kile anachokifanya,kwa sasa mchizi ana albam mkononi yenye mikono 14 mikali,na hapa ananipa mikono miwili niisikilize na ikibidi nikupe uisikilize pia(kupitia MNM),mikono hiyo ni "Nyota Yangu" ambayo kaifanya producer anaitwa AK 47(humjui wewe),kitu cha clunk hivi,na kingine chaitwa "Atupele" kaifanya producer Small Jobiso(alikuwa THT pia),na studio iliyohusika yaitwa "Tatoo Recs".Albam yaitwa "Zote Zangu" na nna uhakika itashika mbaya,hebu fanya hivi....msubiri utamwona sasa iv aki-shine....Valley!!!!

Tuesday, June 29, 2010

HAPPY BIRTHDAY NICOLE SCHERZINGER.....

NICOLE SCHERZINGER

Leo tar 29 June ni siku ya kuzaliwa mwanadada kutoka PussyCut Dolls Nicole Scherzinger,alizaliwa tar kama ya leo mwaka 1978,so kama nawe unasheherekea birthday yako leo fahamu kuwa unashea birthday na star huyu..Happy Birthday Nicole Scherzinger..and you..

Monday, June 28, 2010

SUGU MIKONONI MWA POLISI...


Hizi ni habari ambazo nimezipokea si muda mrefu sana,Mr ii aka SUGU amekamatwa na polisi leo asubuhi akijiandaa kwenda kwenye kikao cha press talk katika ukumbi wa Balaza la Sanaa la Taifa(BASATA),mpaka sasa haijafahamika sababu za kukamatwa kwa mkongwe huyo wa muziki wa Hiphop nchini..endelea kuwa hapa kwa habari zaidi....saurce:michuzijr.blogspot.com

HAWA NI BAADHI YA WALIONG'ARA BET AWARDS 2010 JUZI..

BET

Ijumaa niliweka post hapa kukujilisha kuwa zile tunzo za BET 2010 zilitakiwa zifanyike jumapili ya jana,zilifanyika na kiukweli zilifana sana japo BET wenyewe hawakuzionesha live zaidi ya baadhi ya highlights ambazo zilioneshwa leo asubuhi...wenyewe wametangaza kuzionesha jumamosi ya wiki hii tar 3 July,lakini kwa ufupi hiki ndicho kilichotokea jana....

BEST FEMALE R&B ARTIST(ALICIA KEYS)


 
BEST MALE R&B ARTIST(TREY SONGS)


 
BEST GOSPEL(MARVIN SAPP)

BEST FEMALE HIPHOP ARTIST(NICKI MINAJ)

BEST MALE HIPHOP ARTIST(DRAKE)

 
BEST GROUP(YOUNG MONEY)

 
BEST NEW ARTIST(NICKI MINAJ)

 
BEST VIDEO DIRECTOR(HYPE WILLIAMS)

 
BEST ACTRESS(MO'NIQUE)

Fans hawa ni baadhi tu ya washindi,lakini msanii kama Nicki Minaj ali-shine sana baada ya kupokea tunzo mbili, na mafanikio yalionekana zaidi kwa kundi la Young Money linaloongozwa na mkali Lil Wayne ambaye hakubahatika kuhudhuria tunzo hizo kwakuwa yuko gerezani akitumikia adhabu yake,wenye Dstv na Startimes BET Awards 2010 zitaoneshwa jumamosi July 3 kuanzia saa tatu kamili usiku kwa saa za kibongo.

BRAND NEW NGOMAZ ON MNM...

IZO B

Mdau na fans wote wa MNM mambo vipi??naamini kila kitu kiko sawa kabisa au sio??weekend pia ilikuwa mzuka mbaya,basi freeeeeshhhh!!!!!Hapa nina taarifa kwako nzuri sana,kupitia MNM Blog now unaweza sikiliza nyimbo mpya ambazo zimeongezeka,utasikia wimbo wa Shetta Ft:Binamu,Godzilla,Nicki Mbishi-"Mi naplay" rmx, Nicki wa pili Ft:Lina-"Kitu Changu", Izo B Ft:Suma Lee-"Bussines", Linex-"Mama Halima", Amini(THT)-"Ndio unikimbie", Ben Paul F:Stereo na Nicki Mbishi-"Pata Raha", Noorah Ft:Ngwea-"Chembavament" na Madee Ft:Godzilla-"Game inavyochange".Kama kawa kama dawa MNM itaendelea kukuburudisha zaidi na zaidi na zaidi,so endelea kupita hapa,si ndio???