BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, July 30, 2010

POLENI TRIPLE "A" FM-ARUSHA

THE LATE NEEMA


MAREHEM NEEMA LUSANDA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TRIPLE A FM AFARIKI DUNIA

MAREHEM ALIKUA MTANGAZAJI WA MUDA MREFU NA MWENYE UWEZO MKUBWA HAKIKA
TUMEPOTEZA MTU MUHIMU KATIKA HABARI NEEMA ALIFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI
YA MOUNT MERU BAADA YA KUSUMBULIWA NA SHINIKIZO LA DAMU KWA WIKI KADHA KITU
AMBACHO KILICHOMPELEKEA UMAUTI WAKE HAPO JANA MAREHEM AMEACHA MTOTO MOJA
NA MJANE TAARIFA UTARATIBU WA MAZISHI NI KESHO KATIKA MAKABURI YA NJIRO
TAARIFA HIZI NI TOKA KWA RADIO MANAGER WA TRIPLE BWANA BORRY MBARAKA KWA
YEYETO ANAYETAKA KUWASILIANA NA CREW YA TRIPLE A FM APIGE NUMBER HII
0655707022
ROHO YA MAREHEMU ILALE MAHALI PEMA PEPONI AMINA

MNM says..Poleni Triple "A" fm-Arusha.

MNM'S ALBUM OF THE WEEK...TEFLON DON By RICK ROSS

TEFLON DON(COVER)

"Teflon Don" ni zaidi ya jina lake kama albam ya nne ya mchizi kutoka Def Jam William Leonard Roberts II aka Rick Ross,ni jina lenye heshima la albam ya mchizi aliyetaabika mbaya na kuongoza kwa muda mrefu sana kitu yaitwa Miami's Undergroung Rap Scene enzi hizo..na baadae kuibuka na kufanya kweli na albums tatu za kwanza ambazo ni "Port of Miami"(2006), "Trilla"(2008) na "Deeper than Rap"(2009)..July 23 ndio mzigo huu mpya mchizi akauachia kitaa..singo ya kwanza ilikuwa "Super high" akiwa na Ne-yo ambayo imefanywa na producer anaitwa Dj Clark Kent toka J.U.S.T.I.C.E league..wengine waliotia mikono ni The Runners,The Inkredibles ambao wote waligonga kwenye "Deeper Than Rap" na the Olympics.

DEEPER THAN RAP(COVER)

Ndani ya "Teflon Don" kuna mikono minene 11 ambayo ni "I'm not a star", "Free Manson", "Tears of joy", "Maybach music III", "Live fast Die young", "Super high", "No 1", "Mc Hummer", "B.M.F(Blowing Money Fast)", "Aston Martin Music" na "All the money in the world".Mzigo huu unatishia maisha ya mzigo mwingine mkali wa Eminem "Recovery" huko kunako soko....so inabidi tusikilizie tuone...hii ndio "Teflon Don" ya Rick Ross kaitafute...

OLD SKOOL...."HORACE BROWN"

HORACE BROWN

Ndoto yake kubwa wakati anakuwa ilikuwa ni kuja kuwa mcheza mpira wa kikapu maarufu NBA..lakini ndoto hiyo ikaja kuyeyuka baada ya kuumia mguu alipokuwa in court..Huyu si mwingine ni mchizi anaitwa Horace Brown..ambaye alizaliwa huko Charlotte,North Carolina,US...amekulia kanisani na hata muziki pia alianza kuimba kanisani...DeVante Swing wa Jodeci alipata kuisikia demo ya jamaa akamkubali..then akamtafutia vi-dili vya kuwa backvocalist wa Christopher Williams na Terri & Monica..hiyo ikampa nafasi ya kuonwa na rais wa Uptown Records Andre Harrel,akasainishwa mkataba pale..1994 mchizi akaachia singo yake ya kwanza kabisa "Taste your Love" ambayo ilitamba sana South..lakini ikabuma kwenye chat zinazoaminiwa..baadae Andre Harrel akahamia Motown Records,akahama nae,huko akaachia singo zingine mbili katika kuipromoti albam yake "Horace Brown" na 1996 ikaingia kitaani rasmi,humo kuna mashavu ya Diddy(Puffy Daddy),Faith Evans,Fox Brown na Jay Z..2007 akatokea kwenye albam ya mwanamuziki wa R&B wa kijerumani Lisha "Nice To Meet you" katika mkono "I want that"...Huyu ndo Horace Brown.

MY TEAM OF INSPIRATION...RADIO ONE 1995

WALIOKAA MBELE..CHARLES HILARY,MIKIDAD MAHAMOUD
JULIUS NYAISANGA(BAADA YA MZUNGU)..WALIOSIMAMA NYUMA
TOKA KULIA...TAJI LIUNDI(MASTA T),SUNDAY SHOMARI,ABUUBAKAR LIONGO,
MBELE YAKE KUNA LILIAN(MRS TAJI NOW),VICK MSINA,FROLAH NDUCHA,
PIECE KWIYAMBA,MIKE MHAGAMA NA DJ RANKIM RAMADHANI.

Mdau hii haiwezi kuja tokea tena bongo hii...ndo maana naiita "My team of inspiration"...ni DREAM TEAM ya Radio One Stereo mwaka 1995..naikumbuka team hii na nakumbuka mbali sana...nakumbuka "kumepambazuka" ya wakati ule ya kina Piece Kwiyamba na Frolah Nducha...nakumbuka "Dj Show" ya Taji, Mike na Dj Rankim Ramadhani...nakumbuka "Chombeza Time" ya Sunday Shomari, nakumbuka "Chaguo la msikilizaji" ya Mike Mhagama.."Spoti Leo" ya Abuubakar Liongo ambae ndio kawaharibu watangazaji wetu karibu wote wa vipindi vya michezo, nakumbuka "Miwani ya maisha" ya Vick Msina..aahh!!!"Nani zaidi" ya .........,Kweli hii ilikuwa ni Dream Team..na haiwezi rudi tena..watu walipiga kazi na ikaonekana..ama kweli CHA KALE DHAHABU.

MIKE MHAGAMA AKIJIANDAA KUM-INTERVIEW
INNOCENT GALINOMA(KULIA) KTK DJ SHOW
1995.

Thursday, July 29, 2010

WALAKA TOKA KWA SHABIKI WA BONGO FLEVA..MTOTO WA VITOTO

WASANII NA CHAMA

Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi october mwaka 2010,huu ni waraka wangu kwa wasanii wote wa mziki wa kibongo!. Najua kuna miaka mingi sana ya kuukomboa huu mziki wetu lakini wazungu wanasema "One step at a time"...na muda ndio huuu..........!!!!

Miaka kibaao sasa wasanii mmekuwa mkilalamika juu ya kudhulumiwa haki zenu kwa kuibiwa kazi zenu na kulipwa malipo madogo ya album zenu kiwango kisichokidhi mahitaji yenu,hilo ni sawa kabisaaa!!
LAKINI je!! mmejipanga vp kumaliza hili tatizo lenu? kila kukicha viongozi wanawa-ahidi kwa mdomo kuwa watamaliza tatizo lenu bila utekelezaji wa vitendo kitu ambacho mimi nakiona kama ni kiini macho na nyinyi wenyewe mnakifahamu....
Viongozi hawa hawa ambao wanakataa kwa "makusudi" kusimamia maslahi yenu ndio hao hao wanaokuwa wa kwanza kuwachukua nyinyi wakati wa uchaguzi ili muwasaidie kuwapigia kampeni kwa kutoa burudani pindi wanapokuwa kwenye mikutano yao,,,,
Sasa inakuwaje mnatumika kirahisi namna hii? wakati kwenye interview zenu wengi wenu mnajinadi kuwa nyinyi ni wanaharakati na sasa mnafanya mageuzi ya huu mziki wenu,vp mageuzi ndio haya? Mnapotumiwa kwenye kampeni mnacheka cheka kwa furaha pale mnapopewa laki kadhaa au vimilioni kama shukrani ya "kinafki" kutoka kwa hao watu waliowatumia!!!! Na baada ya kumaliza kampeni zao hao hao wakiwa madarakani wanawasahau na kujifanya hawawakumbuki tena hadi wakati mwingine wa uchaguzi.....(huu ni utumwa wa kifikra) najua mtasema mnaangalia pesa na ndio mana mnawafanyia kazi yao na sio kitu kingine!!! Sawa sikatai huenda ni kweli pesa ndio mnayofuata,,, sasa je? nyie wasanii wa kiume ikitokea wamama wakiwapa pesa za kutosha na kuwataka mkatumbuize kwenye "kitchen party" yao mtaenda kudhalilishwa sababu ya pesa au mtakataa?
Sidhani kama ntapata dhambi nikisema kuwa kitendo cha wasanii kutumiwa kwa muda na hawa watu mi nakifananisha na binti wa kike ambae bwana wake huwa anajifanya kumjali na kumfuata pale anapotaka penzi lake tu!! na akishamaliza shida zake anaondoka na kumuacha binti huyo akiteseka na hali ngumu ya maisha bila ya msaada wowote na hurudi tena pale anapokuwa na shida hiyo!!
Enyi wasanii kwanini mnajipa thamani ndogo kiasi hicho???
Huu ndio wakati wenu wasanii kuonesha mapinduzi yenu na misimamo yenu na zile harakati ambazo kila kukicha mmekuwa mkizitaja kwenye nyimbo zenu na interview zenu,,,yawapasa kudai maslahi yenu kwanza kuliko kutumika kuhangaikia maslahi ya watu wengine....
Sitoona ajabu nikiwaona wasanii wale wale wanaokuwa wa kwanza siku zote kudai haki zao wakitumika kwenye kampeni mwezi october na kisha baada ya uchaguzi mwakani wasanii hao hao tutawaskia tena wakilalamika kutokumbukwa na viongozi husika!!!
"CALCULATE THE RISK,BEFORE YOU JUMP"
By Mtoto wa vitoto..
(Ze' son of babiez)
2010...

COMING SOON..."I'AM THE WEST" By ICE CUBE

IAM THE WEST(COVER)

Waweza pata picha gani katika huu mzigo wa mtu mzima ICE CUBE??Dah!!Namuheshimu sana huyu mchizi..mi sipati picha aisii.."watoto" wamechafua sana hali ya hewa na vi-clunk vyao visivyokuwa na kichwa wala miguu..na vi-swaga vyao...sasa mtegemee mchizi anayekuja kusafisha hali ya hewa ya muziki wa HIPHOP..Ice Cube anadondosha mzigo huu Sept 28 mwaka huu..."I am The West"...Usubiri.

ZINANIKUMBUSHA MBALI...."Age Ain't Nothing But A Number" By Aaliyah

AGE AIN'T NOTHING BUT A NUMBER

Hii ni segment mpya kabisa na itakuwa inakuja hapa kila alhamis kama ya leo hivi..hapa nitakuwa nakuchambulia albam moja ya kitambo ambayo mimi kiukweli nikiisikiliza inanikumbusha long-long time mazee....leo naanza na mzigo wa kwanza kabisa wa marehemu Aaliyah.."Age Ain't Nothing But A Number"..Mzigo huu ulidondoka rasmi kitaa mnamo June 13 1994 chini ya Jive na Blackgroung Records...hii ilikuwa ni baada ya kusainiwa na anko wake Barry Hankerson na kutambulishwa kwa mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki gwiji R-Kelly akiwa na miaka 12 tu na mchizi ndie aliyefanya kazi yote ya albam hii..mzigo una urefu wa dk 48 na sekunde 54(48:54) na ulianza kurekodiwa tangu sept 1993 mpaka May 1994 wakati huo Aaliyah akiwa na umri wa miaka 14 tu...Mzigo ulikuwa na hit kama "Back & Forth" na "@ your best(you are love)" ambazo zilichukua gold award toka Recording Industry Association of America(RIAA) na baadae zikafuatiwa na hit kama "Age Ain't Nothing" wenyewe na "No One Knows How To Love"...Mzigo huu kwa taarifa yako mdau ulifikia mpaka nafasi ya 18 kwenye Billboards Top 200 Albums na kuuzwa zaidi ya nakala milioni mbili kwa Marekani tu...kama huna ama bado hujausikiliza hebu fanya kuutafuta..ni mkali sana na mimi binafsi huwa sichoki kuusikiliza aisii...unanikumbusha mbali sana..

Wednesday, July 28, 2010

MNM MEETS..FREDRICK BUNDALA aka SKY WOKA..

SKY WOKA aka WEEZY

NAME;FREDRICK BUNDALA
NICK NAME;SKY WOKA(Sky Weezy)
BIRTHDAY;Dec 1' 1982
OCCUPATION;RADIO PRESENTER&PRODUCER
MEDIA;RFA(Radio Free Africa)
HOBBIES;MUSIC,MOVIES,SPORTS etc

10 YEARS ANNIVERSARY OF LADY JAY DEE MUSIC...

Nimetupiwa hii longtime ila sio ishu nkikutupia wewe leo....


Nawaalika Tena Mzalendo Pub Tar 6 August 2010

Nasherehekea kutimiza miaka 10 tangu niingie kwenye biashara/ kiwanda cha muziki Tanzania
Kuna mengi nilioyafanya mazuri au pengine yasio mazuri lakini nashukuru MUNGU bado ameniweka kwenye ramani.
Tutazindua pia album ya COMBINATION ya Machozi Band, Kutakuwa na Jarida la mitindo la Shear Illusions ambapo ukinunua unapata CD ya bure.
Nitaimba nyimbo zote kutokea album ya MACHOZI, BINTI, MOTO NA SHUKRANI na Collabo nyingine nyingi nilizofanya na watu na ambazo mngependa kuzisikia.
Nawapa fursa ya kuchagua nyimbo mnazozipenda pengine mimi huwa sizipigi
Natumaini kuonana na nyinyi siku hiyo ambapo pia hata stage itakuwa sio ile mliozoea kuiona kila siku
with lots of love and respect to you all


Lady Jay Dee.

HAPPY BIRTHDAY SOULJA BOY....

SOULJA BOY

In a full of fact mood..nimerejea bana dah!!!haya mambo hayana mwenyewe haya..ya kuugua??asikwambie mtu bana..poa!poa!wadau na fans naamini bata zilikuwepo kama kawa..na kwa muda kidogo ilibidi niiache hii kitu kwanza(blog) ili nirudishe afya na vitu ka hizo...nimerejea na kwa kuanza naanza na haya mambo yetu ya B'days..leo tar 28 July ni b'day ya bwana mdogo hapo juu..Soulja Boy..yeye alizaliwa tar kama ya leo mwaka 1990..so km nawe ni b'day yako leo jua unashea b'day na huyo bwana mdogo..Happy Birthday Soulja Boy..

DADDY GOT WELL...IZ BACK ON HIS MNM BLOG..

MY DADDY(BIZZO)

"Jamani kitu cha kwanza labda niwashukuru tu kwa muda wa kama ka'wiki hivi ambako nimekuwa nikiiendesha hii blog ya mshua wangu..ni kwamba mshua sasa yuko fit na anaweza kuendeleza libeneke kama kawa kama dawa...kiukweli nime-enjoy sana kuwa nanyi fans wote wa MNM ambao kila siku mnapita hapa kuona yote mazuri tunayowaangushia..iko poa hiyo..so mimi sasa nakaa kando..nnasubiri chochote ambacho mshua atanipa nifanye coz hii ilikuwa ni kama interview kwangu japo kweli mshua aliikubali malaria..asanteni wote kwa sala zenu..nawatakia kila lililo jema..asanteni na bye!bye!bye!"
By Carolyn..

ME,MYSELF&I(CARO)

Tuesday, July 27, 2010

TOMMOROW ON "MNM MEETS"......???????

???????

IN STORES..WIKI IJAYO.."FAKE PREGNANT"

FAKE PREGNANT(COVER)

"Jana nilikudondoshea mzigo mpya kutoka D-One Production unaitwa "Aunt Suzzy"..nkakwambia utaupata kitaani kwako very soon..sasa kabla ya huo kuna huu hapa ambao utatangulia..ni kutoka katika kampuni ileile D-One Production..mzigo huu mdau ni noumer joh!!yaani usiupimie kabisa..hivi nnavyozungumza nawe town nzima imeshachafuka kwa posters zake..wiki ijayo tu upo kitaani kwako..

FAKE PREGNANT

Sasa niskiize kwa makini..wakati unaisubiria "Aunt Suzzy" burudisha macho yako na hii kwanza..ndani utamuona Daudi Michael..Soud Ally..Amina Kibiki na Ester Falvian Mushi..kazi kwako mdau wangu..ni FAKE PREGNANT".

MTAMBUE HUYU..."JOSEPH VAN VICKER"

VAN VICKER

"Mchizi ni raia wa Ghana na alizaliwa Aug 1 1977..mshua wake ni Mdatch na mama yake ni kutoka Liberia..ndo maana ukimcheki fresh mchizi kama kachanganya rangi vile..si ndio??Mshua alifariki mapema sana wakati dogo ana miaka sita tu na kutokana na hilo mchizi akalelewa na mama tu..mpaka leo mchizi anam-appriciate sana mamake na anamuita shujaa wake..kiskuli jamaa kapiga ktk skuli moja yaitwa Mfantsipim.

VAN

Mchizi aliingia kwenye kiwanda cha burudani mwaka 2003 kama mtangazaji wa redio na Tv(Metropolitan Television) na mwaka huohuo akatokea kwenye series moja iliyokuwa ikitengenezwa na kurushwa palepale Ghana "Suncity"..na pale alitumia jina la LeRoy King jr..alicheza kama mwanafunzi wa sanaa aliyezaliwa US na kuja hapo Suncity kumalizia masomo yake..Baada ya kufanya vizuri katika series hiyo Van Vicker akapata mwaliko kama msanii msaidizi katika movie yake ya kwanza "Divine Love" ambamo humo alikutana na wakongwe waliokuwa wakifanya vizuri wakati huo kama Jackie Aygemang na Majid Michael.Ni movie ambayo ilimfungulia milango ktk industry hii huko West Africa..na baada ya hapo ikawa historia..mchizi anakula mashavu ya movies kila kukicha na ameonekana kufanya vizuri zaidi katika soko la Nigeria zaidi kuliko nchini kwake Ghana..amekuwa mkali sana wa romantic movies na ameonekana kuwapiku mghana mwenzake Majid Michael na mnigeria Ramsey Noah.

WITH HIS FAMILY

Kwa wale mademu mnaommezea mimate mchizi huyu hebu sikieni hii..Van Vicker ameoa tyr na ana watoto wawili..kimafanikio mchizi yuko safi mbaya sana..anamiliki kampuni inaitwa Sky & Orange ambayo inadil na matangazo ya biashara na kampuni ingine inaitwa Babetown inayohusika na kuandaa matamasha mbalimbali pale Accra, pia mchizi ana bonge la Unisex Babber Shop ambalo amelipa jina hilohilo la Babetown..mambo ya kijamii pia yumo..anaendesha mfuko unaitwa Van Vicker Foundation ambao unadil na kuinua vipaji mbalimbali vya vijana katika sanaa..huyu ndio Van Vicker sasa..rrrraaaarrruukaaa"!!!

Monday, July 26, 2010

AGOSTI HII...THE BATTLE..RAY vs KANUMBA...

CRAIZY LOVE(COVER)

BED REST(COVER)

"Hii kweli ni battle...hawa naweza waita ni magwiji wawili wa movie za kibongo..na kiukweli ndio wanaofanya vizuri hata sokoni pia...tena sana tu..sasa mwezi ujao wa nane jamaa wanadondosha kwa pamoja mizigo yao..Kanumba kupitia KANUMBA THE GREAT FILMS atadondosha "Craizy Love" ambayo ndani kamtupia pia Hemed Suleiman...Ray yeye kupitia RJ COMPANY atadondosha kitu "Bed Rest" ambamo ndani kuna wakongwe watupu kwenye tasnia hii..sasa tuone nani atakuwa nani mwezi ujao..zote ni kupitia "Steps Entertainment"

FID Q AWA MTANGAZAJI WA REDIO...

FID Q

"Mdau leo nimepata nafasi ndogo ya kumsikiliza Fid Q akifanya show ya mchana kupitia Clouds fm..show ambayo imekuwa ikifanywa na mtangazaji mkali Hamis Mandi aka B-12 inayokwenda kwa jina la XXL kubwa kuliko..but hakuwa peke yake bali alikuwa na Adam Mchomvu..nilichogundua ni kwamba mchizi pia yuko tight upande huo mwingine wa ajira..so km akiona muziki unazingua(si kushindwa coz ni mzima balaa) anaweza pia akaja huko na kufanya poa pia..hiyo ilikuwa ni show maalum ya promotion ya "Fiesta" jipanguse ambayo weekend hii inadondoka pande za Mwanza na Fid ndio mwenyeji wa show hyo pande hizo".

KITAANI SOON..."AUNT SUZZY" THE MOVIE..

AUNT SUZZY PT 1

"Huu ndio mpango mzima wa D-One Production..kampuni ijayo juu ile mbaya ktk movie production..huu ni mzigo mwngn ambao bado wa moto kabisa...na ndio kwanza umemalizwa studio..unaitwa "Aunt Suzzy"..ni story ya ukweli sana coz mi nimebahatika kuuona ht kabla haujatimba kitaani kwako..

AUNT SUZZY PT 2

Sasa ngoja nikwambie kitu...humo ndani utampata Mzee Magari..Daudi Michael..Sarah Sudi..Ester Mushi na wengine kibao ambao wamekamua balaa..mimi nasema hv..hebu fanya kuisubiri halafu utanambia...si mchezo"..