Haya!haya!haya!haya tena wadau na fans wa blog ya burudani(muziki na maisha),its another "furahi-day"(friday) kama kawa najua utakuwa unahamu ya kutaka kujua leo nimekuletea albam ya nani katika ile "segment" yetu ambayo ilianza wiki iliyopita ya "My Album of the Week",kama nilivyokuahidi hii itakuwa ndio kama bye bye ya kukutakia weekend njema kabla ya "kufunga shule" kwa wiki hii si ndiooo???sema NDIOOO!!!Leo niko na mwanadafada mkali wa SOUL MUSIC na ambaye mtindo wake wa maisha umekuwa ukiwashangaza wengi,si mwingine niiiiiiiiiiii!!!!!ERIKAH BADU!!na albam yake mpya kabisa inaitwa "NEW AMERYKAH PT 2(the Return of ANKH).Hii ni albam ya saba na ambayo mwanadada huyo ameiachia kitaa rasmi 30 March mwa huuhuu kwahiyo bado iko moto kabisa.Lakini hii ni part II ya albam yake ingine aliyoiachia February 26 2008 chini ya lebo ya MOTOWN iliyoitwa "NEW AMERYKAH PT 1(4th World War).
Friday, April 16, 2010
MY ALBUM OF THIS WEEK(NEW AMERYKAH PT 2 by ERIKAH BADU)
Posted by RENATUS KILUVIA at 5:28 AM 0 comments
NAHISI NINA MAKENGEZA(HEBU CHEKI NA HAWA JAMAA HAWAFANANI KWELI??)
Posted by RENATUS KILUVIA at 4:35 AM 0 comments
Thursday, April 15, 2010
MOSE RADIO&WEASEL TV WITH NEW ALBUM.
Posted by RENATUS KILUVIA at 4:37 AM 1 comments
HUYU NDO BANANA ZORRO BWANA!!
Posted by RENATUS KILUVIA at 4:15 AM 0 comments
Wednesday, April 14, 2010
SPECIAL KWA KIZAZI CHA BONGO FLEVA......
Vizazi vya Bongo Fleva ni ngumu sana kuyafahamu haya,na nimegundua kitu ambacho nataka ku-share nawe mdau wa blog hii ya burudani,hivi leo kuna baadhi ya ma'redio djs na watangazaji ambao wanajifanya wanaujua sana muziki huu wa KIZAZI KIPYA ,lakini kiukweli HAWAUJUI,nikijaribu kuwasikiliza kwa makini nagundua kuwa muziki wanaoujua ni muziki wa kuanzia miaka ya 2002 kuja mpaka hivi sasa,wanaujua muziki wa kuanzia enzi za hits za Bongo Records(P-Funk) kuja mpaka sasa,NIJUAVYO MIMI NI NGUMU KUKIJUA KITU VIZURI KAMA HUJUI KILIPOTOKEA,KILIPO NA KINAPOKWENDA,na huwezi kujua KILIPO na KINAPOKWENDA kama hujui kilipotokea.
Kwanza Unity Foundation Makanga,ML Chriss(Blue)&Abbass(Yellow)
Hao hapo juu ni Kwanza Unity(K.U Crew),moja kati ya makundi waasisi wa muziki wenu huu ambao leo mnauita Bongo Fleva na ambao karibu kila mtu sasa anajifanya anaujua sana,kundi hili lilikuwa linaundwa na washkaji kibao tu kama akina K-Single(Kibacha),Easy B,Nigga One(RIP),Rhymson(Zavara),D-Rob(RIP),Fresh G na wengineo na walianza michakato hii mwishoni kabisa mwa miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90 kipindi ambacho ndo "awamu ya kwanza" ya muziki huu wa kizazi kipya,kipindi ambacho tulikuwa tunaita "Swahili Rap".Na katika kipindi hiki ni makundi machache sana ndio yaliyokuwepo likiwamo hili la Kwanza Unity.Wengine walioweza kujitokeza katika awamu ya pili ambayo ilianza kwenye miaka ya 1994 ambapo muziki huu ulitambulika zaidi kama "BONGO HIPHOP ni G.W.M toka pande za Kurasini,Diplomats toka Sinza,The Hard Blasters,Cycle Tack,Dar Young Mobb,W.W.A,Mawingu Band(walikuwa wanaimba),Bad Skins,Mack Muga(Solo artist),Erick aka E-Atack(Solo artist)Sos B(Solo artist),II Proud(Solo Artist),Ras Pompidou(Solo artist),Saleh Jabir toka Znz(Solo artist)Jotwa Jokeri toka Mwanza(Solo artist),WEPWAA toka Mwanza pia na wengine kibao ambao siwezi kuwataja wote hapa.
Kwanza Unity Crew isipokuwa K-Singo na Samia X
Katika awamu hii ya kwanza ya muziki huu jamaa walifanikiwa kufanya albam moja "Kwanza Unity" ilokuwa na hit kama "amani" na zingine kibao tu,mwishoni mwa miaka ya 1994( awamu ya pili) ya muziki huu ambayo pia ndo ili-change jina kutoka "swahili rap" mpaka "Bongo Hiphop" ilikuja baada ya kuanza kwa vituo binafsi vya redio katika masafa mapya kwa wakati huo(masafa ya fm) na kidogo kuanza kutoa airtime ya nyimbo hizo wakati huo,Nakumbuka Radio One stereo(kipindi hicho ilikuwa 99.6fm now 89.5fm) ndo ilikuwa redio ya kwanza kwa hapa Dar na ilianza mwaka 1994 na kipindi cha kwanza cha vijana na kutoa airtime kwa nyimbo hizi kilikuwa ni Dj Show ya wakati huo na watangazaji walioanza kuzicheza nyimbo hizo ni Taji Liundi(Master T) na Mike Pesambili Mhagama.......
Makala hii itaendelea wiki ijayo usikose....usikose kupitia blog ya burudani,comments zinahitajika..
Posted by RENATUS KILUVIA at 3:04 AM 0 comments
Tuesday, April 13, 2010
HEBU SANUKA NA HII!!
Posted by RENATUS KILUVIA at 3:36 AM 0 comments
Monday, April 12, 2010
MILAZO 101 YA MILLAD NEW SEASON ON MAY
Posted by RENATUS KILUVIA at 3:27 AM 0 comments
ETI HEMED ANAKULA MARA 8 KWA SIKU,DUH!!
Posted by RENATUS KILUVIA at 3:05 AM 0 comments