BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, June 4, 2010

"MAKENGEZA" YA WIKI HII......TAZAMA VIZURI...

Makengeza bado yapo mdau wangu coz watu ninaowafananisha bado wapo kibao,na sijui kama wataisha leo au kesho,wiki iliyopita nilikuwa na LADY GAGA na CHRISTINA AGUILERA,leo je??......

BLACK THOUGHT


KANYE WEST

Tumbua mijicho hiyo,au kama vipi toa miwani kwenye huo mkebe vaa,halafu TAZAMA VIZURI...

MNM'S ALBUM OF THE WEEK..."HERE I AM"..BY MARVIN SAPP...

MARVIN SAPP

Mshikaji AMEOKOKA,nimeiandika kwa herufi kubwa kuonesha msisitizo,kazaliwa mwaka 1968 Grand Rapids,Michigan na muziki anaoufanya ni Gospel,Contemporary Christian,Insiparational/Worship,na alianzia kuimba kanisani akiwa na miaka minne tu,kabla hajafikisha miaka 20 amepitia vikundi vingi sana vya nyimbo za injili kabla ya kualikwa kundini na mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu sana nchini Marekani Fred Hammond kuimba "Commissioned" mwaka 1991 baada ya Keith Staten kuondoka kundini humo,alidumu mpaka mwaka 1996 alipoamua kuondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Marcus R. Cole.Kuanzia mwaka huo Marvin akaamua kuanza kufanya shughuli za muziki akiwa peke yake(Solo) na mpaka sasa ameshafanya albams saba.Wimbo kama "Never would Have Made it" kutoka ndani ya mzigo wake "Thirsty" aliouachia mwaka 2007 ulifika mpaka nafasi ya 14 katika US Billboard Hot R+B/Hiphop songs na nafasi ya 82 katika US Billboards Hot 100.Jamaa ana tunzo ya BET ya mwaka 2008 kama BEST GOSPEL ARTIST.

THIRSTY(COVER ALBUM)

Sasa mdau tuache yote hayo,turudi katika mzigo wake huu ambao nimeuchagua kukumwagia leo hii,mzigo una ngoma kumi na mbili kali vibaya vibaya kama "I came", "Keep holding on", "Fresh wind", "Comfort zone", "Wait", "He has his hands on you", "Don't count me out", "The best in me", "Here I am", "Praize you for ever" na "More than a conqueror".Exucutive producer ni James Jordan aka Jazzy,pia kuna waliosaidia kuitengeneza hii kazi kama Buddy Strong ambaye alihusika sana katika keyboard,Mike Martz(trampet),Jamil Freeman na Aisha Cleaver(backvocalists) na producer aliyemaliza mchongo mzima ni Arron W. Lindsey.

HERE I AM

Mzigo ulidondoka rasmi kitaa March 16 mwaka huu,mchizi kwa sasa yuko katikati kabisa ya majina makubwa na yanayoaminika katika muziki wa injili duniani kama akina Kirk Franklin, Donnie McClurkin, Mary Mary and Yolanda Adams,BET kuna show kila j2 kuanzia saa tano kamili asubuhi(saa za kibongo) inaitwa "Sunday Gospel with BOBBY JONES,ukitumbuatumbua macho huwezi kukosa kumuona huyu jamaa,"Here i am" mzigo uko nafasi ya 60 katika Billboard Top 200 albums chat,huyu ndio MARVIN SAPP bana,kama unafeel kuenjoy na gospel ukiikosa "Here I am" utakuwa hujajitendea haki,itafute.


LEO USIKU KTK "TUPO PAMOJA" SHOW...

ARNIE GIZZLE

Mdau ijumaa ndio hii,bata bata za weekend ndo twazianza hivi,lakini kabla ya chochote hebu nikusaue na hii,"Tupo Pamoja" show ya Ttv kama kawa iko hewani leo usiku kuanzia saa tatu kamili,na ni nini ambacho utakiona pande hizo....kaa nami vizuri nikujuze....Arnie Gizzle amemaliza season ya kwanza ya show,hivyo basi ni wakati mzuri wa wewe kucheki kwa ufupi vipindi baadhi vya season ya kwanza in case kama hukusanuka kabla,"SIDE A" kuna interview ya Hakeem 5,ni time yake leo,na ktk "SIDE B" mcheki bosi wa TMK Wanaume Family Saidi Fella,tukutane pale tufurahishe macho yetu bana......au vipi???

Thursday, June 3, 2010

TOMORROW ON MNM'S "ALBUM OF THE WEEK".....

MARVIN SAPP

Kesho fans wangu msikose kupita hapa,nitakuwa na "Here I am" ya Marvin Sapp katika gospel,tumepitia sana muziki wa kidunia,sasa tuhamie upande huu pia,usikose....

"MTAMBUE HUYU".....JILL SCOTT.....

JILL SCOTT

Ni JILL SCOTT,niko nae leo katika "mtambue huyu",ni mama wa miaka 38 sasa,alizaliwa April 4 1972 Philadephia,Pennsylvania US,ni mwanamuziki anaimba Soul,R&B,Jazz na Spoken Word(kama ngonjera),mwandishi wa nyimbo na mashairi mbalimbali lakini pia ni muigizaji.Kalelewa na mamake anaitwa Joyce Scott na bibi yake huko North Philadelphia,wakati yuko mdogo bado alipata nafasi ya kuhojiwa na jarida moja liitwalo "Jet Magazine" na alikuwa mtoto mchangamfu,mjanja na mwenye furaha kuliko wote waliopata nafasi kama hiyo wakati huo na hivyo kumshangaza hata mhariri wa jarida hilo,baadae akasoma Philadelphia High School for Girls kabla ya kumaliza hapo na kujiunga na Temple University,kwa wakati huohuo akifanya kazi mbili za muda mfupimfupi.
KTK POSE(JILL)

Kipaji chake kilivumbuliwa na mchizi anaitwa Amir Thomson wa The Roots ambaye alimwalika kujiunga na band yao ya hiphop na kufanya collabo "You Got Me",hiyo ilikuwa mwaka 2000,baadae akacollabo na Erick Benet,Will Smith na Common,alikuwa mwanamuziki wa kwanza ku-sign "Stive McKneever's Hidden Beach Recording lebel".Albam yake ya kwanza "Who is Jill Scott?Words and Sounds Vol 1" iliachiwa mwaka 2000 na singo "A long walk" ilifanya vizuri sana katika chats mbalimbali,mwaka 2003 akawa nominated Grammy Awards katika Best Female Vocal Perfomance lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuipata tunzo hiyo,ilikwenda kwa Erika Badu,mwaka 2005 akachukua tunzo ya Grammy kama Best Urbun/Altenative R&B Perfomance kupitia mkono "Cross my mind",2001 aliachia mzigo "Expirience;Jill Scott 826+ halafu ikafuata "Beautiful Human;Words and Sounds Vol 2" mwaka 2004.

WITH AWARDS

Baada ya hapo Jill akaendelea kuandika sana mashairi,kwa mfano shairi lake kama "The Moments,The Minutes,The Hours" ambalo lilitolewa na St. Martins Press mwaka 2005.Mwaka 2007 Sept 25 akaachia mzigo mwingine "The Real Thing;Words and Sounds Vol 3 ambamo humo ndani kuna mkono unaitwa "Hate on Me",2008 akaachia albam yake ya pili ya live "Live in Paris" na ndani kuna mikono nane(8) ambayo ilirekodiwa wakati wa tuwa yake moja iliyobatizwa "Big Beautiful Tour".Kutokana na ushauri wa rafiki yake wa karibu director "Ozzie Jones" Jill alianza kujihusisha na masuala ya kuigiza filamu mwaka 2000 ambapo alijiunga na thieta(theatre) company moja huko Philadelphia ambapo alijifunza masuala ya uigizaji filamu.Mwaka 2004 aliigiza kama Donna katika season 4 ya series moja inaitwa "Girlfriends" na baadae ktk movie "Cavedwellers" akiwa na Kelvin Bacon na Kyra Sedgwick,2007 alitokea katika "Hounddog" kama Big Mama Thomton(itafute hii) na pia katika "Why Did I Get Married".2009 ametokea katika muendelezo wa "Why Did I Get Married" ambayo ni Pt II.Huyu ndio JILL SCOTT,i love this woman and i want u to lave her too,mtambue sasa.
BEAUTIFUL JILL SCOTT

"STAR TIMES" MAMMMAAAA YANGUUUUU!!!!!!!

MTV BASE

Mdau nina muda kitambo sasa natumia huduma za hawa jamaa bwana,wanajiita "STAR TIMES",duh!!kiasi tunachowalipa hata hakilingani na huduma wanazotupa kabisa,imagine tunawalipa sh. za kibongo 9000 kwa mwezi,ndani jamaa "wametupia" TRACE Tv,Entertainment Tv,BET,TRACE TROPICAL na jana usiku sasa,mammmaa yanguuuu sikuamini,nimekuta "wametupia" kitu cha MTV BASE na TBC2 pale kati,na bado hapo kuna channels zingine kibwena za akili,dah!!sina la kusema ila kwakweli MAISHA safiiiiiiiiiiii,weekend hakuna kuzurura wala nini,TUNASHUKURU SANA jamani,kilichobakia sasa "tupieni" channel kama mbili hivi za latest movies bila kusahau CLOUDS Tv na DTv,aaahhhh!!!natulia zangu home tuliiiii!!!ukija unatikuta.

A NEW RADIO SOAP..."DETOUR OF REAL LOVE"

CHARACTERS WA DETOUR OF REAL LOVE

"Detour of Real Love" ama "Njia Ndefu ya Penzi la Dhati" ni tamthilia mpya ya radio ambayo imeandaliwa kwa ufundi mkubwa ili kuwapa burudani wapenzi wa tamthilia za radio wenye hamu ya kupata drama yenye mfumo wa filamu kupitia radio.Tamthilia hii ya ukweli inamhusisha kijana handsome aitwaye Ian ambaye anapata mkate wake wa kila siku kwa shughuli ya ukonda wa daladala. Katika kazi zake za kila siku anakutana na dada mrembo, msomi na mtoto wa tajiri aitwaye Rachel ambaye anapanda daladala hiyo akiwa na mpenzi wake Erick ambao wanasoma chuo kikuu. Upole, werevu na mvuto alionao Ian unampagawisha Rachel na kumfanya afanye kila aliwezalo kumpata kijana huyo bila kujali tofauti zao za maisha. Baada ya Erick kunyang'anywa mpenzi wake na konda Ian, anaamua kulipiza kisasi kwa kuwawinda wapenzi hao wapya. Furaha fupi na ahadi aliyoipata Ian kwa kupendwa na Rachel inadumu kwa muda mfupi na kuyaona maisha kama jehanamu. Fuatilia tamthilia hii kila siku za jumatatu saa tano usiku na kurudiwa jumatano muda kama huo."Detour of Real Love" imeandikwa na mwandishi anayekuja juu Tanzania aitwaye Victor Chuma na kutayarishwa na Fredrick "Skywalker" Bundala. Muziki katika tamthilia hiyo umetayarishwa na Skywalker na Amba producer kutoka Iringa.

Wednesday, June 2, 2010

COMING SOON......"CRUNK ROCK" BY LIL JON...


CRUNK ROCK(COVER ALBUM)
                       
Mzigo huu unadondoka tar 8 mwezi huuhuu,wa mtu mzima Lil Jon,ndani kuna akina Pastor Troy,Wake Flocker Flame,Souja Boy,Stephen Marley&Damian Marley,Ice Cube,The Game,Elephant Man,YingYang Twins,R-Kelly,Mario,Pitbull na wengine kibao,hebu tuusubiri tuuone.

A NEW BLOGGER...KARIBU MH. ZITTO KABWE.

MH. ZITTO KABWE

Ni habari njema kwetu wadau wa blogs na fans wote kwa ujumla,huu ni ujio wa mwanasiasa kijana na wa mfano Mh. Zitto Kabwe(Mbunge wa Kigoma-Kaskazini) ambaye now ni blogger,amefungua blog yake ambayo inahusu siasa za kidemokrasia na elimu ya kiraia,wakati wanasiasa watu wazima wakikomalia MEDIA zingine kama magazeti ya kila siku,redio na tv,Mh. Zitto anadhihirisha "ujana" wake kwa kuungana na mamilioni ya wapenzi wa blogs duniani kote na ku-share nao masuala mbalimbali,HONGERA SANA,mkamate kupitia www.zittokabwe.wordpress.com.
source;bwaya.blogspot.com

Tuesday, June 1, 2010

MAONI YA ZAVARA KUHUSU MARACAS MUSIC FESTIVAL 2010..


Habari zenu ndugu zangu.
Kwa waandaaji wa hili tamasha, naomba kuweka nasaha zangu ama kuleta changamoto kwenye mjadala huu.
Nilivyosikia Maracas mimi binafse hisia ya mwanzo kiukweli niliwaza ni jambo fulani lenye uhusiano na Marekani ya kusini. 
 Je Muaandaaji ni mtu wa huko ama?
 Kama ndio  je sisi tunaweza kumshawishi aweke jina la kiswahili ama la Kizaramo, hasa ukizingatia linafanyikia kwenye himaya ya WAZARAMO pale Bwagamoyo, hasa ukizingatia pale Bagamoyo kuna mzizi wa mila na desturi za kiswahili uliobobea sana.
Kama la. Sisi kama wadau wa sanaa na utamaduni tunaweza kumshauri muandaaji ama waandaaji kuangalia kanuni ya msingi kabisa ya kiutamaduni (UWAKILISHI).
Niliposoma ile orodha nimegundua kuwa asilimia 100 ya washiriki jukwaani ni wasanii wa hapa nyumbani.  
Je tukiangalia Biashara , kama ndo kigezo kilotumika.  Kwenye kanuni ya kibiashara na mauzo si ingekuwa vyema ukiwa na Bidhaa ya mahala fulani basi jina lake nalo liwakilishe hiyo bidhaa inakotoka?! Mfano magari ya Kijapani, tunayatambua tu kwa majina yake. Toyota, na pikipiki Honda na ya maeneo mengine  hali kadhalika.

Hebu tuangalie hili jambo kwa makini maana inawezekana ndugu waandaji kwa uwingi wa majukumu wanaweza kuwa hawakulipa uzityo uliostahili, mimi naongea kama mdau wa sanaa na wakati huo huo mlaji wa bidhaa hii. Hivyo nadhani nastahili kitu kilicho bora na ningekaa kimya nisingetumia haki yangu ya kimsingi kama mteja wa hawa walio andaa.

Nashauri kama kuna mtu anaweza kuusogeza huu mjadala pia kwa BASATA, ili tuwawajibishe nao pia maana kwa vyovyote waandaaji walipitia huko..Sasa BASATA inaonekana ama walipitiwa kwa hilo au wamekuwa wepesi wa kuokea ada za usajili na kuangalia vitu nyeti kama hivi vinawapita huku wakikenua na kutoa mikono ya kila la kheri kwa wahusika baada ya kupokea ada.

Miaka ya awali ya 1999 hadi 2001. Nilikuwa nikituma nyaraka mfululizo kwa taasisi inayoitwa Clouds entertaiment kama sikosei waliokuwa wakiandaa Summer Jam..Ilikuwa kichekesho ama kioja kuwa na jina la namna hii(walau mimi nliona hivyo) maana moja ya swali nilikuwa nikiwauliza ni kuwa wamesahau kuwa Dunia sio ubapa tena(kama mataifa ya magharibi walivyokuwa wakiamini awali, hadi Galileo alivyowabumburusha). Huwezi kuwa na msimu wa Kiangazi kizio cha kaskazini na cha kusini kwa wakati mmoja. Ilichukua muda hadi wao kuliona hilo lakini mwishoe walibadili na hili tamsha sasa linaitwa Fiesta.

Najaribu kuwaza kwa mchanganuo alioutoa nadhani ndugu Vitalis, basi ingekuwaje kama tungeita labda hili tamasha Zeze, ama Marimba na kutoa maelezo mazuri tu ya mahusiano yetu na Marimba(Nadhani ni neno la upande huu wa Afrika).  Jibu nnalopata kwa haraka haraka ni kwamba litaleta mvuto sana kulinganisha na Maracas. Asilimia kubwa watashindwa kutamka na watakaoweza basi kutakuwa na fungu kubwa la watakaokwazwa na tofauti ya R na L hivyo WENGI watasikika WAKIITA MALAKAZ.

Kutoweka kwa ari na msisimko wa UZALENDO unachangia sana kuzorota kwa uchumi (MJADALA MREFU SANA HUU), najua wachumi na wasomi wa sayansi ya jamii wanaweza wakawa na mitazamo tofauti ama inaweza kuleta mijadala mirefu sana lakini ukiangalia kiundani kuna ukweli.  Nisimalize wino hapa wakati kuna wengi watakaopenda kuchangia. Naomba nasaha zenu ndugu na jamaa zangu.
Mdogo wenu Zavara, enh yule yule wa Kwanza Unit, Harakati za UKOMBOZI wa mtu mweusi kwa njia ya Sanaa na mengineyo.

Kazi njema

SORRY FANS,OUR BLOG WAS ON CONSTRACTION....


Sorry wadau na fans wote wa MNM Blog,kuanzia siku ya jana na muda kidogo wa siku ya leo kama ulipata nafasi ya kupita hapa uliona kama mambo "hayaeleweki" vile,si ndio ehh??usijali,yote hiyo ilikuwa ni katika kuiweka blog yetu vizuri na muonekano mzuri zaidi ili ivutie zaidi,naamini hivi sasa MNM Blog ni nzuri na inavutia,haya ni maboresho ya kawaida ambayo nitakuwa nayafanya kila mara nipatapo nafasi,asante na libeneke linaendelea kama kawa kama dawa...

Monday, May 31, 2010

ANTI-VIRUS WA KIRUSI CHA BONGO FLEVA HUYU HAPA...

SUGU aka MR II
Habari hizi mdau nimezipokea toka mapema siku ya jana,ni kwamba yule kirusi anayeendelea kumtafuna Bongo Fleva tayari ameshapatiwa dawa(antivirus),ni ukweli ulio wazi na ambao auhitaji hata darubini kuuona,kuwa Bongo Fleva now inaelekea kunako kaburi kwa kasi ya ajabu sana,na kinachoiua hii Bongo Fleva kipo kinajulikana na kinaonekana,sasa ma-legendari wa muziki huu wameamua kuitafutia game hii dawa ya kuhakikisha inarudi juu na suala la kifo chake kubaki kama sinema tu,wakiongozwa na SUGU aka MR II,kuna MKOLONI kutoka iliyokuwa WAGOSI WA KAYA,DOTTO wa MAPACHA,ZE DUDU,G-SOLO na wengineo wengi wameamua kutengeneza albams za bure kwa mtindo wa "mix tapes"(kutumia ala zilizokwishatumika) ambazo zitakwenda kwa mtindo wa VOLUMES na EPISODES ambazo zimebatizwa jina la "UNTI-VIRUS",kitakachofanyika ni kila Mc kuimba topic yake kwa kuwataja kwa majina halisi "MAFISADI" wanaoiua Bongo Fleva ili wapenzi wa muziki wajue na watambue kilichoko nyuma ya pazia katika muziki huu.

WAGOSI WA KAYA

Albams zote zitagawiwa bure bila gharama yoyote kwa yeyote atakaezitaka na kuwekwa katika mitandao mbalimbali ili yeyote aweze kuzi-download na kuzimiliki,na kwa kuanza washkaji wanaanza na "ANTI-VIRUS Vol 1" ambayo itakuwa na nyimbo kumi na sita(16) na baada ya hapo zitafuata zingine mpaka Vol 10 na kuendelea,haya wadau hizi ni harakati zingine baada ya "NGURUWE" ya ZE DUDU,tungoje tuone kama italeta mabadiliko yoyote katika game hili na kubadili upepo ambao kiukweli si mzuri ktk muziki huu kwa sasa.



LAST SUNDAY KTK "MILAZO 101" SHOW....

MILLARD&JOSH
Wadau na fans wa MNM mambo vp??naamini weekend yenu ilikuwa bomba sana kama ilivyokuwa yangu au sio??nimewamiss sana kwakweli lakini ndo hivi tena j3 ingine tunakutana hapahapa kujuzana yaliyo mengi ya kiburudani zaidi ndani ya blog yetu ya burudani(Muziki Na Maisha).Ishu hii nilitakiwa niipost last friday kama nilivyokujuza awali,ni segment mpya ktk blog hii,lakini niwieni radhi jamani kwa sababu zilizokuwa nje kabisa ya uwezo wangu ikawa ngumu kwakweli,ila sio ishu naweza tu kukujuza ni nini kilifanyika jana ktk show namba wani Bongo now "Milazo 101" ya Redio One,kwanza alisikika Mashonda mke wa zamani wa Swiz Beats akiuzungumzia uhusiano wa aliyekuwa mume wake(Swiz Beats) na mwanamuziki Alicia Keys pia yalisikika mahojiano marefu na yakusikitisha ya mwanamuziki kutoka Burundi KIDUM,toka enzi alipokimbia vita miaka kumi na tano iliyopita nchini kwao mpaka kuwa star wa muziki Afrika na Mashariki bila kusahau A.Y ambaye alipita studio mara moja kutoa hi kwa fans wote wa show na kupata nafasi ndogo ya kuzizungumzia collabo zake na Sean Kingstone na J-Martins,kuanzia saa kumi na moja na nusu zikasikia ngoma kali tano ktk "FAT 5",Eminem na "Not Afraid" ikiwa ktk jackpot(nafasi ya kwanza) kwa wiki ya pili mfululizo,hiyo ndio "Milazo 101" show new season with new level and new swagz,kama uliikosa wiki iliyopita wiki hii usiikose,kwa wale wa mbele waweza isikiliza show ya jana kupitia www.babkubwa.ning.com/profile/milazo101.