BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, June 4, 2010

MNM'S ALBUM OF THE WEEK..."HERE I AM"..BY MARVIN SAPP...

MARVIN SAPP

Mshikaji AMEOKOKA,nimeiandika kwa herufi kubwa kuonesha msisitizo,kazaliwa mwaka 1968 Grand Rapids,Michigan na muziki anaoufanya ni Gospel,Contemporary Christian,Insiparational/Worship,na alianzia kuimba kanisani akiwa na miaka minne tu,kabla hajafikisha miaka 20 amepitia vikundi vingi sana vya nyimbo za injili kabla ya kualikwa kundini na mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu sana nchini Marekani Fred Hammond kuimba "Commissioned" mwaka 1991 baada ya Keith Staten kuondoka kundini humo,alidumu mpaka mwaka 1996 alipoamua kuondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Marcus R. Cole.Kuanzia mwaka huo Marvin akaamua kuanza kufanya shughuli za muziki akiwa peke yake(Solo) na mpaka sasa ameshafanya albams saba.Wimbo kama "Never would Have Made it" kutoka ndani ya mzigo wake "Thirsty" aliouachia mwaka 2007 ulifika mpaka nafasi ya 14 katika US Billboard Hot R+B/Hiphop songs na nafasi ya 82 katika US Billboards Hot 100.Jamaa ana tunzo ya BET ya mwaka 2008 kama BEST GOSPEL ARTIST.

THIRSTY(COVER ALBUM)

Sasa mdau tuache yote hayo,turudi katika mzigo wake huu ambao nimeuchagua kukumwagia leo hii,mzigo una ngoma kumi na mbili kali vibaya vibaya kama "I came", "Keep holding on", "Fresh wind", "Comfort zone", "Wait", "He has his hands on you", "Don't count me out", "The best in me", "Here I am", "Praize you for ever" na "More than a conqueror".Exucutive producer ni James Jordan aka Jazzy,pia kuna waliosaidia kuitengeneza hii kazi kama Buddy Strong ambaye alihusika sana katika keyboard,Mike Martz(trampet),Jamil Freeman na Aisha Cleaver(backvocalists) na producer aliyemaliza mchongo mzima ni Arron W. Lindsey.

HERE I AM

Mzigo ulidondoka rasmi kitaa March 16 mwaka huu,mchizi kwa sasa yuko katikati kabisa ya majina makubwa na yanayoaminika katika muziki wa injili duniani kama akina Kirk Franklin, Donnie McClurkin, Mary Mary and Yolanda Adams,BET kuna show kila j2 kuanzia saa tano kamili asubuhi(saa za kibongo) inaitwa "Sunday Gospel with BOBBY JONES,ukitumbuatumbua macho huwezi kukosa kumuona huyu jamaa,"Here i am" mzigo uko nafasi ya 60 katika Billboard Top 200 albums chat,huyu ndio MARVIN SAPP bana,kama unafeel kuenjoy na gospel ukiikosa "Here I am" utakuwa hujajitendea haki,itafute.


0 comments: