BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, April 30, 2010

"MAKENGEZA" YAMEZIDI JAMANI!!

Leo sina maneno mengi jamani,wiki iliyopita nilikuwa na Avant na R-Kelly,leooooo!!!!

                                               REMMY MA

                                                    LIL KIM

Nimezingatia suala la gender zaidi ijumaa hii,hao ni akinadada ambao wote ni ma-rapper,Remmy Ma na Lil Kim,hivi hawafanani kweli??hebu comment basi tuonee!!!

MNM'S ALBUM OF THE WEEK(Raymond Vs Raymond By Usher Raymond)

Hey!hey!Wadau na fans wa blog ya burudani,kwanza kabisa niombe radhi kidogo.Kwakweli wiki hii mambo ya mtandao naweza sema yamenichanganya sana,kuna mambo mengi sana nilipanga kukupatia mdau na fans wangu lakini mtandao uliniangusha sana,lakini sio ishu.Leo ni ijumaa tuangalie yale ya kiijumaa ijumaa zaidi au sio??KARIBU sasa katika ile segment yetu ya kila ijumaa "My album of the week".Baada ya wiki iliyopita kuwa na mchizi toka NAIJA leo narudi pande zilezile za mbele kupitia albums ambazo zinafanya vizuri sana kwa sasa,leo niko na mtu mzima USHER RAYMOND na kitu "Raymond Vs Raymond".

                       RAYMOND VS RAYMOND(FRONTFACE)

Hii ni albam ya sita ya mchizi ambayo imetumbukia kunako maduka 30st March kwa U.S.A,baada ya albam yake ya tano ya 2008 ya "Here I Stand" ambayo kwa wachambuzi wa masuala ya burudani kama mimi hivi tunaweza sema ilimbwela(ilishindwa kufanya vizuri),na hii ilitokana na kushindwa kabisa kuuza baada ya wiki mbili nzuri za mwanzo za kimauzo wakati albam hiyo inaingia sokoni,albam hiyo ilitanguliwa na "Confessions" ambayo iliuza kinoma,baadhi ya singles kutoka ndani ya "Confessions" ziliweza kushika no 1 karibu nusu nzima ya mwaka na kuvunja rekodi ya charts mbalimbali duniani.Lakini ilionekana kama ni self-confession ya Usher mwenyewe ambae kwa wakati huo alikuwa akishughulikia talaka ya aliyekuwa mkewe TAMEKA FOSTER.

                      RAYMOND VS RAYMOND(BACKFACE)

Mzigo umetoka LaFace Records na una jumla ya ngoma 14 za ukweli,mbili zizokwishaachiwa ni "Hey Dady(Dady's Hom)" feat;Plies na huu ambao duh! unasumbua sana saivi "OMG" feat;Will.I.am.Zingine ni "There goes my baby","Lil Freak"feat;Nicki Minaj,"She don't know"feat Ludacriss,"Mars Vs Venus","Pro Lover","Foolin' around","Papers","So many girls","Guilty"feat T.I,"Okay" na "Makin' love(into the night).

                           HERE I STAND(USHER RAYMOND)

Hope maelezo hayo yanatosha sana kukufanya uitafute albam hii na kutoa muda wako kuisikiliza pia au vipi,cha kuongeza tu ni kuwa hivi nnavyoipost hii ishu hapa kwenye blog ya burudani "Raymond Vs Raymond" iko katika nafasi ya tano ndani ya chat zinazoaminika za BILLBOARDS katika albam 200 bora za wiki hii.Asentiiii!!!!

Wednesday, April 28, 2010

MNM BLOG MEETS...EZDEN JUMANNE aka THE ROCKER.


PROFILE;
NAME;Ezden Jumanne
NICKNAME;The Rocker
OCCUPATION;Radio Presenter
MEDIA;Kiss Fm
LOCATION;Rock City/Mwanza
AGE;24yrz
HOBBIES;Knowing new people,
reading books,music etc
Wadau na fans ndio j5 yenyewe hii,na segment yetu ndio tumeianza hivyo na mchizi hapo juu,so kama vp nawe waweza nicheki na kunitumia picha zako na maelezo yako kidogo khs wewe halafu mpango mzima ukawa hapa kwenye blog ya burudani si ndio??poa.

Tuesday, April 27, 2010

TOMMOROW ON "MUZIKI NA MAISHA MEETS"

Jamani fans nawasisitiza tena,nafasi ndio hii basi itumie,ile segment yetu mpya ya "muziki na maisha meets" inaanza kesho,so kama nawe utaona pouwa kutokea hapa kwenye blog ya burudani,fanya fasta kunitumia picha zako katika bizzo4shizzo@ymail.com au renatuskiluvia@ymail.com na maelezo yako kidogo kuhusu wewe halafu j5 ijayo UTAKUWA WEWE.So keshoooooo muziki na maisha meets...........


Utamjua vizuri kesho.......................

HAPPY BIRTHDAY EMILY RIOS&LISA JENSEN.

Leo ni tar 27 April,j4 safi kabisa,katika pitapita zangu katika mitandao mbalimbali nikagundua kuwa siku ya leo ni birthday ya mastaa kibao,ila mimi nakuletea mastaa wawili tu.

                                                             EMILY RIOS

 Huyu ni wa kwanza anaitwa Emily Rios,ni star mdogo anayechipukia wa movie nchini Marekani,amezaliwa tar kama ya leo mnamo mwaka 1989,unaweza kumcheki katika "The main of a certain age" ambapo amecheza kama Maria,ni movie ya mwaka huuhuu na ametokea pia katika episode ya 2008 ya series inaitwa "House".Ni hivi majuzi tu amesaini mkataba wa kutokea katika kipindi cha Tv cha Friday Night Lights(FNL) katika angalau episodes sita za kipindi na ataigiza kama Epyck ambapo utengenezwaji utaanza mwezi huu baada ya kumalizika kwa msimu wa nne kupitia DIRECTV,na premieres ni katika NBC May 7.So kama leo ni birthday yako shea naeeee!!!

                                              LISA JENSEN

Mwingine ni huyu,Miss Tanzania no 3 wa mwaka 2006,Lisa Jensen,leo hii ni birthday yake,amezaliwa tar kama ya leo miaka kadhaa iliyopita,hivi sasa anajihusisha na masuala ya mitindo na matangazo kibao ya biashara,shea nae basi siku hii star huyu wa kibongo.Happy Birthday Emily Rios na Lisa Jensen. 

Monday, April 26, 2010

PREMIER YA LOVELY GAMBLE J5&MY DREAMS IN STORES THIS WEEK

                              LOVELY GAMBLE(MOVIE COVER)

Movie imetengenezwa na URBUN PULSE na imeshutiwa Uingereza,ndani kuna "galacha" wa filamu za kibongo ambaye ni kama alitushtua hv kwamba nasi tunaweza ishu hizi,anaitwa Steven Kanumba,naamini ni moja kati ya kazi za kitanzania ambazo hutakiwi kuzikosa aisii,sababu ziko kibao lakini mimi nakupa moja tu nzito ambayo sisi wadau wa haya mambo ya kuzitengeza hizi tunajua undani wake,ni kwamba imetengenezwa kwa muda mrefu(haijaripuliwa),nathubutu kusema imetumia mwaka mzima kutayarishwa mpaka kuletwa kwako,tofauti na zileeeeee za wiki mbili tayari eti unaambiwa iko dukani.Keshokutwa j5 pale club Billcanas inaoneshwa kwa mara ya kwanza(primiered).Ni Lovely Gamble itakayosambazwa na KAPICO TANZANIA Ltd.Usiikose.

                                                  MY DREAMS(MOVIE COVER)

Mzigo mwingine huu hapa wa "swahiba",unaitwa "My Dreams",huu utauona wiki hiihii kitaani kwako koz town nzima imeshachafuka na posters zake kali,umepigwa na RJ Company "vijana wa kazi"(sidhani hata kama huwa wanalala hawa jamaa) na unasambazwa na Steps Entertainment,nimeufuatilia sana mzigo huu katika hatua zote za utengenezwaji wake,naamini utakuwa NOMA sana,humo ndani macho yako yatamshuhudia Mahsein Awadh(Cheni),Rose Ndauka,Irene Uwoya(Mama Ndiku) na Vicent Kigosi(Ze dairekta),GRM wameshughulika,camera kabeba Razaq Ford na kwenye mashine "kaumiza mgongo"(editing) Ray mwenyewe,hebu fanyafanya kuutafuta.MY DREAMS.