BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, July 23, 2010

MNM'S ALBUM OF THE WEEK.."HOW I GOT OVER" BY THE ROOTS

HOW I GOT OVER(COVER)

"Hey hey..once again..segment yetu imerudi na ndio hivi ijumaa leo..kila kitu ni mpango mzima hapa kati..jana nilisema kuwa leo ntaanza na hii albam ya watu wazima "The Roots" na mzigo wao huu mpya kabisa unaitwa "How I got over"..mzigo ulidondoka rasmi tar 22 mwezi uliopita na umetengenezwa kwa miaka miwili toka 2008-2010..jamaa wako chini ya Def Jam na studio iliyohusika kuutengeneza mzigo huu ni MSR Studios ndani ya New York..maproducer waliotia nakshi katika mikono iliyomo ndani ni Black Thought ambaye ndio kiongozi wa kundi,Questlove,Dice Raw na Rick Friedrich..Executive producer ni Richard Nichols.

BLACK THOUGHT

Mzigo una dk 42 na sekunde 25(42:25) na singo ya kwanza ilikuwa "Rising Down" ambayo waliiachia mwaka 2008 na "How I got over" ambao waliuachia muda mfupi kabla mzigo haujatimba kitaa..jumla ya mikono iliyoko humo ni 14 ambayo ni "A piece of light" (Feat;Amber Coffman,Angel Deradoorian na Haley Dekle), "Walk alone" (Feat;Truck North,P.O.R.N na Dice Raw), "Dear God 2.0" (Feat;Monsters of Folk), "Radio Daze" (feat. Blu, P.O.R.N., Dice Raw), "Now or Never" (feat. Phonte, Dice Raw), "How I Got Over" (feat. Dice Raw), "DIllaTUDE: The Flight of Titus", "The Day" (feat. Blu, Phonte, Patty Crash), "Right On" (feat. Joanna Newsom, STS), "Doin' It Again", "The Fire" (feat. John Legend), "Tunnel Vision", "Web 20/20" (feat. Peedi Peedi, Truck North) na "Hustla" (feat. STS).

THE ROOTS

Fans kwenye chat za billboard top 200 albums mzigo huu uko nafasi ya 33 wiki hii, nakumbuka mshua aliniambia kwenye weekend hii atakuwa tayari ameshaupata mzigo huu..so mi nategemea kuusikiliza kwa makini sana kama ntakuta mshua keshautia mikononi coz nawafeel sana hawa jamaa..Hiyo ndio "How I got Over" ya The Roots..kama vp itafute banaaaaaa"....

DIDDY KAFANYA MAMBO KWA DOGO...

DIDDY

"Nimeinyaka hii sasa ivi...kuwa Diddy amemkubali sana dogo Justine Bieber..na akaona kusema tu kuwa amemkubali haijatosha,so??.. kaamua kabisa kumkabidhi dogo funguo za gari la kifahari aina ya Lambogene.. dogo hivi anakula bata kwa kusukuma mashine hiyo town..na si Diddy tu..washkaji kibao inasemekana wamemkubali dogo ile mbaya,kati ya hao Dr Dre pia alipata nafasi wakati fulani kukiri kuwa dogo ni mkali ile mbaya"...

Thursday, July 22, 2010

OLD SKOOL..."ZHANE"....(JAH-NEY)

ZHANE

"Japo mshua alikuwa hajafanya mambo ili niwepo katika dunia hii..lakini si vibaya nami pia nikijitumbukiza kwenye Old Skool segment..wanaitwa Zhane..inatamkika Jah-Ney..ambao walifanya vizuri sana kuanzia mwaka 1993-1999..kundi liliundwa na wadada wawili Renee Neufville na Jean Norris-Baylor wote kutoka Philladelphia,Pennslyvania US..vipaji hivi vilivumbuliwa na Queen Latifah..katika kipindi hicho chote walipata nafasi ya kufanya albams mbili tu..Feb 15 1994 waliachia mzigo unaitwa "Pronounced Jah-Ney" ambao ulikwenda mpaka platinum..humo ndani kulikuwa na hits kama "Groove Back" na "Sending My Love"...halafu April 22 1997 wakaachia "Saturday Night"..baada ya kusambaratika Zhane..Jean Norris-Baylor alifanya albam moja kama msanii wa kujitegemea "Tesmony:My life" ambayo haikufanya vizuri sana..Renee Neufville yeye aliamua kujiunga na Roy Hargroves katika projects zake za mambo ya viwanda..najua unawamiss kama mshua anavyowamiss...Zhane"..



JAH-NEY

"ALBUM OF THE WEEK" IZ BACK PIPOOOOO!!!

"Kama nilivyopata nafasi ya kuwaahidi jana kuwa nitazungumza na mshua ili kama vp tuone kama twaweza rudisha ile segment kali iliyokuwa inawashika fans kibao ya "MNM'S ALBUM OF THE WEEK"..Mshua kakubali bana...sema safiiiiiiii!!!!SAFIIIIIII!!!!so kuanzia tomorrow ambayo ni kesho si ndio??tutakuwa na hiyo segment..na kwa kuanza mimi ntaanza naaaaa".........

THE ROOTS "HOW I GOT OVER"

Kamwe usithubutu kukosa aisiiii.......

"BABA KASEMA ETI LEO NI B'DAY YA BABA MDOGO"....


"Ile naamka tu baba ananitumia sms..ati leo ni birthday ya huyu jamaa..anaitwa Hamisi Mandi aka B-12 aka B-Dozen na aka zingine kibao tu,eti ba'mdogo unafikisha miaka mingapi leo eti?kwa niaba ya mshua pamoja na fans wote wa MNM nakutakia maisha marefu na yenye fanaka tele wewe na yeyote mwingine aliyezaliwa tar kama ya leo..Happy Birthday B-12"..

Wednesday, July 21, 2010

I HAVE TOLD MY DADDY.."I LOV THIS DUDE"..

ALBINO FLANI

"Nilishamwambia hata mshua kuwa "eti nikiwa mkubwa naomba niolewe na huyu"..mshua akanambia "dont be worried my daughter,its all about love,if u love him,u r gun to marry him"..ALBINO FLANI anaitwa..nnampenda kwakweli..na kukudhihirishia hilo nimekutupia mpini wake mpya kabisa "Niko na Wewe" kamshirikisha Pipi..kama vipi sikiliza pembeni kule kwenye real playa"..

TONIGHT ON BET'S 106 & PACK...NE-YO

NE-YO

"Sina hakika sana mdau kama bado nitakuwa sijalala ama la!!ila ishu ni hivi leo usiku ndani ya "the number one music countdown show" 106 & Pack ndani ya BET kutakuwa na bonge la interview la mtu mzima Ne-Yo..hiyo ni kuanzia saa tatu kamili kwa saa za kibongo so kama vipi inabidi uipimie hii..si ya kukosa japo mi naweza kuikosa...kama kawa Tarrance na Rocsie watakuwa pale kati wakifanya mambo".. 

IN STORES NOW.."TEFLON DON" BY RICK ROSS..

TEFLON DON(COVER)

"Ni moja kati ya vitu ambavyo mshua aliniambia nisiviache kamwe..ni hii albam ya mtu mzima Rick Ross..inaitwa "TEFLON DON"..mzigo huu umeingia rasmi kitaa jana tar 20 july na tayari uliishatanguliwa na mikono kama "Super High" yuko na mchizi Ne-Yo pale kati na sasa "Freemanson" ambayo kamtupia Jay Z na John Legend..baaanaa dah!!!bonge bonge moja la mkono asikwambie mtu..mzigo una mikono kumi na mmoja na yote mikali..kwa info hizi inatosha..ila kitu kimoja ntamkumbusha mshua airudishe ile segment ya "album of the week" ili kama vp tuisome albam hii kwa mapana yake siku moja au vp???"..

AM BACK ON BEHALF OF MY DADDY....

CAROLYN KILUVIA

"Habari zenu fans...kwanza wakubwa shikamooni..size zangu mambo zenu vp??..wadogo zangu marahabaaa!!...mimi naitwa Carolyn Renatus Kiluvia..ninakaribia miaka miwili sasa..kwa niaba ya mshua aka dingi aka baba aka dadii wangu Renatus ambaye ndiye mmiliki wa mtandao huu napenda kuwaombeni radhi kwa kuwa kimya kwa muda kitambo...ni muda mrefu sana jamani..na hii ni kutokana na mshua mwenyewe(Renatus) kuikubali malaria wakati haikubaliki..sasa wakati anasubiri afya yake itengemae, nikaona sio ishu kama nikichukua jukumu la baba aka mdingi kuendelea kuwaburudisha kwa kushusha ma-ishu kubao tu kama kawa kama dawa..na kwa kuanza naanza hivi..KARIBUNI TENA..MNM the sagga continues"..