HOW I GOT OVER(COVER)
"Hey hey..once again..segment yetu imerudi na ndio hivi ijumaa leo..kila kitu ni mpango mzima hapa kati..jana nilisema kuwa leo ntaanza na hii albam ya watu wazima "The Roots" na mzigo wao huu mpya kabisa unaitwa "How I got over"..mzigo ulidondoka rasmi tar 22 mwezi uliopita na umetengenezwa kwa miaka miwili toka 2008-2010..jamaa wako chini ya Def Jam na studio iliyohusika kuutengeneza mzigo huu ni MSR Studios ndani ya New York..maproducer waliotia nakshi katika mikono iliyomo ndani ni Black Thought ambaye ndio kiongozi wa kundi,Questlove,Dice Raw na Rick Friedrich..Executive producer ni Richard Nichols.
BLACK THOUGHT
Mzigo una dk 42 na sekunde 25(42:25) na singo ya kwanza ilikuwa "Rising Down" ambayo waliiachia mwaka 2008 na "How I got over" ambao waliuachia muda mfupi kabla mzigo haujatimba kitaa..jumla ya mikono iliyoko humo ni 14 ambayo ni "A piece of light" (Feat;Amber Coffman,Angel Deradoorian na Haley Dekle), "Walk alone" (Feat;Truck North,P.O.R.N na Dice Raw), "Dear God 2.0" (Feat;Monsters of Folk), "Radio Daze" (feat. Blu, P.O.R.N., Dice Raw), "Now or Never" (feat. Phonte, Dice Raw), "How I Got Over" (feat. Dice Raw), "DIllaTUDE: The Flight of Titus", "The Day" (feat. Blu, Phonte, Patty Crash), "Right On" (feat. Joanna Newsom, STS), "Doin' It Again", "The Fire" (feat. John Legend), "Tunnel Vision", "Web 20/20" (feat. Peedi Peedi, Truck North) na "Hustla" (feat. STS).
THE ROOTS
Fans kwenye chat za billboard top 200 albums mzigo huu uko nafasi ya 33 wiki hii, nakumbuka mshua aliniambia kwenye weekend hii atakuwa tayari ameshaupata mzigo huu..so mi nategemea kuusikiliza kwa makini sana kama ntakuta mshua keshautia mikononi coz nawafeel sana hawa jamaa..Hiyo ndio "How I got Over" ya The Roots..kama vp itafute banaaaaaa"....
0 comments:
Post a Comment