BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, April 1, 2010

IJUMAA KUU NJEMA!!!!

Nawatakia Ijumaa Kuu njema,japo ni weekend lakini chondechonde wadau,tusiende kwenye starehe,ijumaa kuu ni siku ambayo tunaadhimisha mateso na kusurubiwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwahiyo ni siku ya huzuni na kutokula nyama,hivyo basi ni vizuri kama ukitulia nyumbani na kutafakari kwa umakini tukio hilo zima na ukumbuke kuwa yote hayo yametokana na dhambi zetu sote mimi na wewe,alisurubiwa ili mimi na wewe TUPATE KUOKOKA.

UNCLE CHARLIE ANA KANSA!!!!

Uncle Charlie


      Huyu ndio Charlie,the last name Wilson

Mkongwe wa slowjams Charlie Wilson a.k.a Uncle Charlie amewakumbusha wanaume wote wamarekani weusi nchini humo kuwa na utamaduni wa kwenda kucheki afya zao mara kwa mara.
Mkali huyo anayetamba na ngoma "there goes my baby" ametoa angalizo hilo hivi karibuni baada ya kupimwa na daktari wake na kuambiwa kuwa ana kansa."kiukweli nilishtuka sana na nikaona huu sasa ndio mwisho wa maisha yangu lakini nilipata moyo na nguvu mpya baada ya daktari wangu kuniambia kuwa ni kansa iliyo katika hatua za awali kabisa kwahiyo tunaweza kuishughulikia mpaka ikatoweka kabisa"amesema.Na kutokana na hilo Charlie Wilson kwasasa amekuwa karibu zaidi na kufanya kazi za kujenga umakini(build awareness) kwa raia na wamarekani weusi zaidi.Huyu ndio Uncle Charlie bana!!!

DJ CHANCY nakukumbuka sana kaka!!!!!


                                                             Dj Chany(Tripple "A")
Kaka nakukumbuka sana kaka,wakati nafanya field 87.5 Kili fm-Moshi mwaka 2007 tulikuwa karibu sana,nilikuwa nawe katika shows karibu zote ulizokuwa unafanya pale,naikumbuka show moja kali sana ulikuwa unaifanya na FDK-One "The Storm" mchana kuanzia 8:00-10:00 jioni,wewe ni mkali sana na naamini ukali wako umezidi mara dufu sasa kwakuwa uko na wanaoijua kazi hasa (Tripple "A" fm).Nakutakia kazi njema ya usukumaji wa gurudumu la burudani huko pande za A-Town.

Wednesday, March 31, 2010

GURU WA GANGSTARR AENDELEA VIZURI!!!


              Rapper GURU anayejulikana kama "the one of the most HipHop influential emcees" hapa juzi kati aliripotiwa kuwa katika hali tete(critical condition),vyanzo kibao vya mbele vilipata nafasi ya kujuza kuwa GURU mmoja kati ya wakali wa mapema miaka ya 80's,90,s na 00,s aliyekulia kwenye kitongoji kinachotoa emcees watata cha Bloocklyn ndani ya jiji lenye maisha ghari duniani New York na memba wa kundi kongwe la GangStarr hivi majuzi alipatwa na mshtuko wa moyo(heart attack) lakini hivi sasa anaendelea vizuri na ameweza kuzungumza tena.
              GURU alizaliwa na kukulia kwa muda mfupi Boston lakini baadae mwanzoni mwa miaka ya 80 alihamia Bloocklyn ambapo Gangstarr iliundwa na soon ika-realise albam ya kwanza chini ya producer 45 Kings.1988 kundi likamsajili Dj mkali PREMIER na mwaka uliofuata wakaachia mzigo mwingine mrefu ajabu "No More Mr Nice Guy" chini ya Wild Pitch Records na bits za ajabu za Dj Premear mwenyewe.
             Baada ya hapo wakawa wanaachia mizigo kibao mfululizo chini ya Chrysalis/Virgin/EMI kama"Step in The Arena"(1991), "Hard to Earn"(1994) na "Moment of Truth"(1998),albam yao ya mwisho ilikuwa "The Ownerz" ya mwaka 2003 ambayo ndani pia zipo vocoz za wakali kibao kama JadaKiss,Fat Joe na mkali Freddie Fox, mwaka 2004 wakatangaza kuachana kutokana na tofauti zao binafsi.Huo ndio mustakabali wa GURU na kundi zima la Gangstarr,kila mpenda HIPHOP damu kama mimi kwa IMANI zetu tumuombee mchizi arudi kama kawa ili tuendelee kupokea mawe toka kwake bana au vp!!!!!!!!!!






Gangstarr (The Ownerz)
Their Last Album 2003

Gangstarr (Step In the Arena)
1991 Album

Gangstarr (The Daily Operation)

                                              Mass Appeal (The Best of Gangstarr)
                                                 

MOTO MKUBWA NYIMBO ZA INJILI PASAKA HII KANDA YA ZIWA


                                  Mkurugenzi wa MSAMA PROMOTION Mr. Alex Msama

Msama Promotion wameandaa Tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litakalofanyika sikukuu ya PASAKA Kuanzia Tarehe 4 Aprili 2010 mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Mara. Akiongea hivi karibuni Mkurugenzi wa Msama Promotions ndugu Alex Msama amesema hivi karibuni ”Tamasha lililopita lililofanyika Diamond Jubilee sikukuu ya Krismas ni mwanzo mzuri wa matamasha yatakayofanyika Shinyanga uwanja wa Kambarage, Mwanza uwanja wa CCM Kirumba na Musoma uwanja wa Karume, viingilio ni sh 2000 kwa kila mmoja”



Amewataja waimbaji watakaoimba siku hiyo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Solomon Mukubwa, Peace Muiru kutoka Kenya na waimbaji kutoka Kanda wengi toka kanda ya ziwa.Kazi kwenu wakazi wa kanda ya ziwa,i wish ningekuwepo mwanawane!!!!

Tuesday, March 30, 2010

S'KIKA NEW SEASON IS BACK(NOW ON EAST AFRICA)

Ile show ya ukweli,nnayoiamini "S'kika" a.k.a "be heard" imerudi tena katika season mpya kupitia palepale CHANNEL O "viewer's edition",na sasa ni home sweet home East Africa,show inaanza kwa kucheki maisha ya wanamuziki mastaa wa Kenya,utaanza kuwacheki KALAMASHAKA halafu JUACALI baada ya hapo ni AMANI,CANIBAL na wengine kibao,mzigo ukimalizwa pande hizo show itatimba Uganda and then Bongo,so ukipata time cheki channel O uoneeeee!!!!!

CANIBUS!!!!!!!LIVE IN SOUTH AFRICA!!!

Media patner wa Channel O "Conscious Soul Ent" na "Urbun Phenomenon Ent" wanamleta American Rapper "Canibus" live ndani ya Bassline Newtown South Africa Ijumaa kuu hii ya tar 2.
Mchizi ana asili ya Senegal pia(kama Akon) na alianza mapema sana akiwa karibu zaidi na memba wa zamani wa Fugeez "Wyclef Jean" jamaa pia alishawahi kuwa ndani ya beef zito na mkongwe LL Cool J kipindi fulani hivi,alishawahi kupiga mzigo na washkaji kibao kama Wyclef Jean mwenyewe,Kurupt toka Dog Pound,Rass Kass,Kool G Rap,Keith Murray,Heltah Skeitah,Jed Mind Tricks,Redman,R.Kelly na machizi wengine kibao.Kama wallet iko poa hebu jisogeze tuoneee!!!

Monday, March 29, 2010

RJ COMPANY


Hawa ndio Rj company,kiukweli jamaa wako serious kweli bwana na ndoto yao ya kuipeleka movie industry katika level za kimataifa naamini itatimia soon,hebu fanya hivi, tafuta movie yao yoyote and then itazame halafu utaniambia mwenyewe,inshort mi nawakubali sana tu,na sasa naisubiri kwa hamu "My Dreams".Pigeni kazi vijana,nawaamini.

HAPPY BIRTHDAY DI' DADA!!


Japo hujasema ni kalenda ya ngapi umechana leo lakini kwangu sio ishu,mi nakutakia tu uchane kalenda mia zaidi na kila ndoto unayoota iwe kweli,happy birthday bi' dada!!!!