BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Wednesday, March 31, 2010

GURU WA GANGSTARR AENDELEA VIZURI!!!


              Rapper GURU anayejulikana kama "the one of the most HipHop influential emcees" hapa juzi kati aliripotiwa kuwa katika hali tete(critical condition),vyanzo kibao vya mbele vilipata nafasi ya kujuza kuwa GURU mmoja kati ya wakali wa mapema miaka ya 80's,90,s na 00,s aliyekulia kwenye kitongoji kinachotoa emcees watata cha Bloocklyn ndani ya jiji lenye maisha ghari duniani New York na memba wa kundi kongwe la GangStarr hivi majuzi alipatwa na mshtuko wa moyo(heart attack) lakini hivi sasa anaendelea vizuri na ameweza kuzungumza tena.
              GURU alizaliwa na kukulia kwa muda mfupi Boston lakini baadae mwanzoni mwa miaka ya 80 alihamia Bloocklyn ambapo Gangstarr iliundwa na soon ika-realise albam ya kwanza chini ya producer 45 Kings.1988 kundi likamsajili Dj mkali PREMIER na mwaka uliofuata wakaachia mzigo mwingine mrefu ajabu "No More Mr Nice Guy" chini ya Wild Pitch Records na bits za ajabu za Dj Premear mwenyewe.
             Baada ya hapo wakawa wanaachia mizigo kibao mfululizo chini ya Chrysalis/Virgin/EMI kama"Step in The Arena"(1991), "Hard to Earn"(1994) na "Moment of Truth"(1998),albam yao ya mwisho ilikuwa "The Ownerz" ya mwaka 2003 ambayo ndani pia zipo vocoz za wakali kibao kama JadaKiss,Fat Joe na mkali Freddie Fox, mwaka 2004 wakatangaza kuachana kutokana na tofauti zao binafsi.Huo ndio mustakabali wa GURU na kundi zima la Gangstarr,kila mpenda HIPHOP damu kama mimi kwa IMANI zetu tumuombee mchizi arudi kama kawa ili tuendelee kupokea mawe toka kwake bana au vp!!!!!!!!!!

0 comments: