BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, June 25, 2010

BET AWARDS 2010 JUMAPILI HII.....


Keshokutwaaaaaaa!!!!!!!!!!imefika bana,nilikuwa naona mbali kumbe kariiibuuuu,wadau zile tuzo ambazo naweza sema kwa sasa zinaheshimika sana BET Awards 2010 ni keshokutwa tu tar 27,tuzo hizo ambazo mwaka huu ni mwaka wake wa kumi toka zianzishwe zinategemewa kuwa kali sana kuliko miaka yote iliyopita,Mc ni Queen Latifah na tutegemee kuona shows kali kutoka kwa Chris Brown,Lil Wayne,Drake,Nicki Minaj na wasanii wengine kibao tu,mi yangu macho nani atakuwa nani...ntakushushia hapahapa MNM....

"MTAMBUE HUYU"...BILAL OLIVER...

Jana wakati nakufahamisha kuwa ntamchambua mshkaji huyu leo nilikuahidi kitu,kuwa nitakutajia redio moja hapa Dar ambayo mimi nimekwisha bahatisha kusikia ngoma ya huyu mchizi,kwingine waweza kesha na usisikie kamwe,ni kwamba lazima uwe deep ndo uweze kuzipata na kuzicheza nyimbo za watu kama hawa,102.6 Choice fm,Natasha akiwa mzigoni ndo waweza msikia Bilal,haya sasa mcheki hapa down......

BILAL SAYEED OLIVER

Mchizi anaitwa Bilal Sayeed Oliver,ni mmarekani alizaliwa tar 21 Aug 1979 huko Philadelphia Sennsylivania,ktk stage anajulikana kama Bilal,anaimba muziki wa Neo-Soul na Jazz,alikuwa memba wa kundi laitwa Soulquarians.Lebel alizofanya nazo kazi ni pamoja na Universal Records na Plug Research.Mwaka 2001 mchizi aliachia albam yake ya kwanza inaitwa "1st Born Second" ambayo ndani kulikuwa na mikono ya producers kibao kama Dr Dre na wengineo,lakini sijui ni "kimavi"??mzigo ulikuwa mkali lakini haukufanya vizuri kabisa sokoni,labda wimbo "Soul Sister" ambao ulikuwa hit sana hasa katika vipindi vya nyimbo za kubembeleza usiku ktk redio mbalimbali.

BILAL(1ST BORN SECOND)

Ingawa mzigo haukutoka sana lakini bado mchizi aliweza kufanya vizuri sana katika shows zake mbalimbali alizokuwa akipiga kwa kujaza maelfu ya mashabiki kitu ambacho kilimpa heshima sana hasa kwa wale waliotambua uwezo wake katika "freeform style perfomance".Miaka iliyofuata jamaa akaendelea kutokea katika projects kibao tu za washkaji wengine kama Common and Jill Scott, on "Funky For You",Common on "Nag Champa (Afrodesiac For The World)" ,Guru and J Dilla on "Certified" from Jazzmatazz, Vol. 3: Streetsoul,Jermaine Dupri on "Supafly" from Instructions na zingine kibao,pia akiendelea kutayarisha mzigo mwingine chini ya Interscope Records na producers Dr Dre na J Dilla,kutokana na kutofikia makubaliano mzigo huo ukasitishwa kutoka.


 
BILAL

2006 Bilal akaachia albam yaitwa "Love For Sale" chini ya usimamizi wake mwenyewe,ndani kulikuwa na ngomaz kibao ambazo mchizi kaziandika mwenyewe na kuzitengeneza mwenyewe isipokuwa "Something to hold onto" ambao ulitengenezwa na producer Nottz.Lakini ni kama Interscope walikuwa na kinyongo nae vile,coz walichelewa kuiachia katika tarehe iliyopangwa na kusababisha mzigo ku-leak kwenye mtandao na kusababisha biashara yake kuwa mbovu hivyo kutomfaidisha chochote mchizi.Kutokana na hilo fans mbalimbali walipata nafasi ya kutoa maoni yao na kuwalalamikia sana Interscope kwa kusababisha hasara isiyokuwa ya lazima kwani ilishaonekana kama isingevuja basi mchizi angegonga copies kibao sana za albam hii.

BILAL SAYEED OLIVER

Mchizi hakukata tamaa,akaendelea na tour zake mpaka mwaka jana aliposign na Plug Research na sasa yuko tayari kabisa kudondosha mzigo waitwa "Air Tight's Revenge" tar Sep 14 2010,wadau wanasema albam hii ya jamaa ni kama "kijembe" kwa wote waliom'bania kwa kipindi chote hicho,mdau kama ulikuwa hujui, kubaniana sio hapa BONGO tu hata mbele pia kuna wabanaji,huyu ndio Bilal Sayeed Oliver..Mtambue sasa..


8 YRZ AGO...98.8 FM...SENGEREMA MWANZA...

BIZZO

Hapa nakumbuka nilikuwa nafanya kipindi cha "Bongo Page",nilikuwa nachapa Bongo Fleva za akili sana na KidBway,Mako Chali,Dj Majizo,Abuubakary Sadiq na washkaji wengine kibao ndio waliokuwa wananitumia nyimbo mpyampya wakati huo,hii ilikuwa ni redio yangu ya pili kupiga mzigo,kabla ya hapa nilikuwa sehemu ingine(ntakudondoshea picha next time),fans huko bado wananikumbuka mpaka leo na huwa wananipigia sana simu,onelove kwa wote wanaonimiss kiukweli coz hata mi pia nawamiss vibaya mno...sapoti yenu ilikuwa ya ukweli sana..

R.I.P MICHAEL...WE TRULY MISS U..1YR UNNIVESARY..

MICHAEL JACKSON

Ilikuwa ni kama utani vile,na watu wengi hawakuamini bana,lakini ukweli ukabaki palepale kuwa King of Pop Michael Jackson "kaondoka" na hatarudi tena,leo ni mwaka mmoja kamili tangu Dunia nzima ilipozizima kwa taarifa za kifo chake,"tutakukumbuka daima Michael,upumzike kwa amani,We Miss U Michael"..

IN THE MAKING OF "THE DATE OF MARRIAGE" MOVIE..

Ni D-One Production tena,baada ya kufanya vizuri kwa "Upside Down" mwaka jana,"Where is Love" na "Fake Pregnant" mwaka huu,now crew nzima ya D-One Production imeingia mzigoni tena kupiga kitu chaitwa "The Date of Marriage".......

ON SET


Cameraman Faridu Nankape na D.O.P Ayubu Santana wakifanya mambo kunako location,isubiri soon itatia timu kitaa chako....


Humu ndani kuna stars kibao,hapa Daudi Michael akioneshana kazi na Ester Mushi katika moja ya scene za movie hii..


Still on set,Daudi Michael ambaye ndo star wa "The Date of Marriage" na Ester Mushi...Wadau hapa nimefanya kama kuwaonjesha kiduchu tu kilichokuwa kinafanyika jana kunako utengenezwaji wa "The Date of Marriage",sehemu ya pili ni hapahapa wiki ijayo pamoja na profile za mastar wote ndani ya mzigo huu...


Thursday, June 24, 2010

2MOROW KTK "MTAMBUE HUYU"....BILAL OLIVER

BILAL OLIVER

Mdau waweza pita redio zote,na ukatoa muda wako mwingi tu kusikiliza na bado usisikie wimbo wowote wa mchizi hapo juu,usiniulize mimi nimemjua vipi coz niko deep sana kwenye haya mambo na sijaanza jana wala juzi,nitakwambia redio pekee ambayo mimi huwa nabahatishabahatisha kusikia nyimbo zake,na ndio kitu kilichonifanya nimkubali mtangazaji ambaye hucheza nyimbo za jamaa huyu,yuko deep pia,kesho nitamchambua hapahapa MNM,usisite kupita hapa,mchizi anaitwa BILAL OLIVER..ni noma..utamtambua soon...

OLD SKOOL.........."SALT 'N' PEPA....

SALT N PEPA

Hope utakuwa unawakumbuka halafu kama una-wish warudi vile,kama ni hivyo basi uko ka' mimi,leo nimesikia ngoma yao moja "lets talk about sex" duh!!nikakumbuka mbali sana,ni SALT N PEPA,kundi lililokuwa linaundwa na akina dada wawili na Dj wao mmoja(mwanadada pia),so jumla walikuwa watatu,Cheryl "Salt" Wray,Sandra "Pepa" Denton na Deidra Roper aka Dj Spinderella ambaye alijiunga baadae na kuchukuwa nafasi ya dj wao wa kwanza kabisa Latoya Hanson,kundi lilifanya kazi kuanzia mwaka 1985 mpaka 2002,zaidi walifanya muziki wa Hiphop na dance na makazi yalikuwa ni katika kitongoji cha Queens New York City.Lebel walizofanya nazo kazi ni Next Plateau,London/Polygram na Red Ant Entertainment.

SALT N PEPA

Singo yao ya kwanza ilikuwa ni "Super Nature" na baadae mwaka huohuo 1985 wakatoa tena "The Showstopper" ambayo ilitumika kama soundtrack katika movie "Revenge of the Neds",kiukweli hii ni single iliyowaonesha njia sana baada ya kuchezwa sana katika vipindi mbalimbali vya redio zilizokuwa zikicheza sana muziki wa rap wakati huo na kuifanya kuwa hit ile mbaya.Albam yao ya kwanza ni "Hot,Cool & Vicious ya mwaka 1986,mwaka 1988 wakaachia "A Salt with a Deadly Pepa",mwaka 1993 ikaja "Very Necessary" baada ya hapo wakaparaganyika halafu wakarudi tena mwaka 1997 na mzigo "Brand New",mwaka 2000 wakashusha "Salt N Pepa:The Best of",rasmi Salt N Pepa ikafa 2002.Wako wapi sasa???sikia hii.....Pepa(Sandra) aliolewa na Treach wa Naught By Nature July 27 1999 na wakatalikiana July 31 2001,mwaka 2008 akatoa kitabu "Lets Talk About Pep" ambacho humo aliizungumzia Salt N Pepa na kupanda na kushuka kwake kimuziki,aliuza sana.Salt(Cheryl) yeye alisema kabisa kuwa muziki hana hamu nao tena na hatakuja kujihusisha tena na masuala ya muziki katika maisha yake yote yaliobakia,sasa anafanya shughuli zake mwenyewe.Deidra ni mtangazaji wa redio moja inaitwa KKBT 100.3 fm L.A na show anayopiga inaitwa "The Backspin" na Dj Mo'Dav,pia anagonga ngoma katika clubs mbalimbali hapo L.A.Unaonaaa!!!

COMING SOON...."THE SON OF CHICO BUSTY" BY BIG BOY..

THE SON OF CHICO BUSTY(COVER)

Mchizi alikuwa na mshkaji wake mmoja anaitwa Andre na kwa pamoja walikuwa wanaunda "OUTCAST",anaitwa BIG BOI,jamaa anakuja na mzigo wake kama solo artist,unaitwa "The Son of Chico Busty",mzigo rasmi unadondoka kitaa tar 6 July,i mean ni mwezi ujao tu,na mpaka sasa keshadondosha ngoma moja matata sana  "shutterbug" toka ndani ya mzigo huu,so tumsubirie tuone....

HAPPY BIRTHDAY SOLANGE KNOWLES...

SOLANGE KNOWLS

Ni sister'ke na Beyonce Knowles,anafanya muziki pia japo yeye hajapata mafanikio bado kama ya mdogo wake,ila ndiko anakokwenda huko,anajishughulisha na biashara ya mitindo na somehow filamu,anaitwa Solange Knowles,leo tar 24 June ni birthday yake,alizaliwa tar kama ya leo mwaka 1986,so kama unasheherekea birthday yako elo fahamu kwamba unashea birthday na star huyu toka familia ya Knowles,Happy Birthday Solange..

Wednesday, June 23, 2010

MNM MEETS.....NEEMA KILUVIA aka NEY NIQ

NEEMA KILUVIA

NAME:NEEMA KILUVIA
NICK NAME:NEY NIQ
OCCUPATION:STUDENT
BIRTHDAY:19 Nov 1992
HOBBIES:MUSIC,MOVIES and SPORTS

HUYU NDIE JUMA NIMJUAE MIMI......

JUMA NATURE

Niwe mkweli jamani,Juma Kassim Kiroboto aka Juma Nature ni mmmoja wa wanaharakati wa muziki wa Bongo mwenye mafanikio sana,hiyo haina ubishi hata chembe,but,Juma Nature wa awali kabisa si Nature huyu wa miaka hii miwili mitatu ya sasa,amebadilika sana kimuziki,kuanzia uandishi,styles mpaka flows,kama wewe ni mfuatiliaji wa karibu wa muziki huu hiyo utakuwa umeigundua...nadhani ndio sababu ya kutoku-shine inavyotakiwa mbali na airtime kiduchu anayopata.Sasa Juma yule tumjuae,yule wa "Jinsi Kijana" na "Sonia" amerudi tena,Juma kaachia mkono mpya kabisa "mtoto mtundu" toka Halisi Records pande za Mbagala Dar,mkono ni mkali na naamini utamrudisha kule alikokuwa mchizi...hebu tumpe nafasi basi tuone...

FIESTA 2010..."JIPANGUSE" RRRRRAAAAA!!!!

FIESTA 2009.."ONELOVE"

Haya fans na wala bata wooooote...hii ni habari njema kwenu..baada ya FIESTA "One Love" mwaka jana kuwa na mafanikio ya kutosha..sasa inakuja FIESTA 2010.."Jipanguse" rrrrrrrraaaa!!!!Soon!!kiprofesa na kisomi zaidi....

LADIES & GENTLEMEN NA SASA NAMLETA KWENUUUUUU........LINEXXXXX!!!!!!...

LINEX

Kama hustling mchizi ka-hustle sana,tena sana,miaka kibao nyuma jamaa kakomaa vibayavibaya bila kukata tamaa na sasa hii ni TIME YAKE,ladies and gentlemen....anaitwa LINEX,mshikaji toka Kigoma kule mwisho kabisa wa reli kaachia mkono ambao ndio "ntolee"...ikirudi tena pancha.."Mama Halima" ndio mkono brand new kutoka kwa LINEX,mkono ambao mimi naamini utamfikisha pale anapotaka kufika kimuziki,muda mrefu sana mchizi alikuwa anaachia mikono mikali balaa lakini baadhi ya wadau ni kama walikuwa wanam'bania asi-shine inavyopaswa vile?"Mama Halima" umetengenezwa na Tudd Thomas pale Ngoma Records,sasa ni zamu yake,so msikilizeni yeye saivi....LINEX.

Tuesday, June 22, 2010

TOMORROW ON MNM MEETS....??????

??????????

Hii ni kesho katika MNM Meets....huyu ni nani??utamjua kesho........??????

"KITAANI LEO".....THANK ME LATER YA DRAKE....

DRAKE "THANK ME LATER"

Fans wa Drake,jamani leo ni tar 22 June,ile albam ya mtu mzima Drake ambayo imesubiriwa kwa hamu sana iko kitaa rasmi kuanzia leo hii,albam inaitwa "Thank Me Later",Drake kasema ni albam poa na amewadiss wale wote wanaomdiss na kumzushia ishu kibao ambazo zinaweza kumuharibia biashara yake ya muziki,so mzigo ndo huo kama vipi hebu anza kuutafuta bana.....

MARADONA'S HAND GOAL 1986..


Mdau,tar kama ya leo mwaka 1986 katika World Cup iliyofanyika Mexico straika Diego maradona wa Argentina(ambaye sasa ni kocha wa timu hiyo) alitikisa nyavu kwa bao la mkono ambalo lilileta utata na mitafaruku kibao dunia nzima,so tulikumbuke ki hivi wakati fainali za mwaka huu zikiendelea huko Afrika ya Kusini....