BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, June 25, 2010

"MTAMBUE HUYU"...BILAL OLIVER...

Jana wakati nakufahamisha kuwa ntamchambua mshkaji huyu leo nilikuahidi kitu,kuwa nitakutajia redio moja hapa Dar ambayo mimi nimekwisha bahatisha kusikia ngoma ya huyu mchizi,kwingine waweza kesha na usisikie kamwe,ni kwamba lazima uwe deep ndo uweze kuzipata na kuzicheza nyimbo za watu kama hawa,102.6 Choice fm,Natasha akiwa mzigoni ndo waweza msikia Bilal,haya sasa mcheki hapa down......

BILAL SAYEED OLIVER

Mchizi anaitwa Bilal Sayeed Oliver,ni mmarekani alizaliwa tar 21 Aug 1979 huko Philadelphia Sennsylivania,ktk stage anajulikana kama Bilal,anaimba muziki wa Neo-Soul na Jazz,alikuwa memba wa kundi laitwa Soulquarians.Lebel alizofanya nazo kazi ni pamoja na Universal Records na Plug Research.Mwaka 2001 mchizi aliachia albam yake ya kwanza inaitwa "1st Born Second" ambayo ndani kulikuwa na mikono ya producers kibao kama Dr Dre na wengineo,lakini sijui ni "kimavi"??mzigo ulikuwa mkali lakini haukufanya vizuri kabisa sokoni,labda wimbo "Soul Sister" ambao ulikuwa hit sana hasa katika vipindi vya nyimbo za kubembeleza usiku ktk redio mbalimbali.

BILAL(1ST BORN SECOND)

Ingawa mzigo haukutoka sana lakini bado mchizi aliweza kufanya vizuri sana katika shows zake mbalimbali alizokuwa akipiga kwa kujaza maelfu ya mashabiki kitu ambacho kilimpa heshima sana hasa kwa wale waliotambua uwezo wake katika "freeform style perfomance".Miaka iliyofuata jamaa akaendelea kutokea katika projects kibao tu za washkaji wengine kama Common and Jill Scott, on "Funky For You",Common on "Nag Champa (Afrodesiac For The World)" ,Guru and J Dilla on "Certified" from Jazzmatazz, Vol. 3: Streetsoul,Jermaine Dupri on "Supafly" from Instructions na zingine kibao,pia akiendelea kutayarisha mzigo mwingine chini ya Interscope Records na producers Dr Dre na J Dilla,kutokana na kutofikia makubaliano mzigo huo ukasitishwa kutoka.


 
BILAL

2006 Bilal akaachia albam yaitwa "Love For Sale" chini ya usimamizi wake mwenyewe,ndani kulikuwa na ngomaz kibao ambazo mchizi kaziandika mwenyewe na kuzitengeneza mwenyewe isipokuwa "Something to hold onto" ambao ulitengenezwa na producer Nottz.Lakini ni kama Interscope walikuwa na kinyongo nae vile,coz walichelewa kuiachia katika tarehe iliyopangwa na kusababisha mzigo ku-leak kwenye mtandao na kusababisha biashara yake kuwa mbovu hivyo kutomfaidisha chochote mchizi.Kutokana na hilo fans mbalimbali walipata nafasi ya kutoa maoni yao na kuwalalamikia sana Interscope kwa kusababisha hasara isiyokuwa ya lazima kwani ilishaonekana kama isingevuja basi mchizi angegonga copies kibao sana za albam hii.

BILAL SAYEED OLIVER

Mchizi hakukata tamaa,akaendelea na tour zake mpaka mwaka jana aliposign na Plug Research na sasa yuko tayari kabisa kudondosha mzigo waitwa "Air Tight's Revenge" tar Sep 14 2010,wadau wanasema albam hii ya jamaa ni kama "kijembe" kwa wote waliom'bania kwa kipindi chote hicho,mdau kama ulikuwa hujui, kubaniana sio hapa BONGO tu hata mbele pia kuna wabanaji,huyu ndio Bilal Sayeed Oliver..Mtambue sasa..


0 comments: