BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, June 3, 2010

"MTAMBUE HUYU".....JILL SCOTT.....

JILL SCOTT

Ni JILL SCOTT,niko nae leo katika "mtambue huyu",ni mama wa miaka 38 sasa,alizaliwa April 4 1972 Philadephia,Pennsylvania US,ni mwanamuziki anaimba Soul,R&B,Jazz na Spoken Word(kama ngonjera),mwandishi wa nyimbo na mashairi mbalimbali lakini pia ni muigizaji.Kalelewa na mamake anaitwa Joyce Scott na bibi yake huko North Philadelphia,wakati yuko mdogo bado alipata nafasi ya kuhojiwa na jarida moja liitwalo "Jet Magazine" na alikuwa mtoto mchangamfu,mjanja na mwenye furaha kuliko wote waliopata nafasi kama hiyo wakati huo na hivyo kumshangaza hata mhariri wa jarida hilo,baadae akasoma Philadelphia High School for Girls kabla ya kumaliza hapo na kujiunga na Temple University,kwa wakati huohuo akifanya kazi mbili za muda mfupimfupi.
KTK POSE(JILL)

Kipaji chake kilivumbuliwa na mchizi anaitwa Amir Thomson wa The Roots ambaye alimwalika kujiunga na band yao ya hiphop na kufanya collabo "You Got Me",hiyo ilikuwa mwaka 2000,baadae akacollabo na Erick Benet,Will Smith na Common,alikuwa mwanamuziki wa kwanza ku-sign "Stive McKneever's Hidden Beach Recording lebel".Albam yake ya kwanza "Who is Jill Scott?Words and Sounds Vol 1" iliachiwa mwaka 2000 na singo "A long walk" ilifanya vizuri sana katika chats mbalimbali,mwaka 2003 akawa nominated Grammy Awards katika Best Female Vocal Perfomance lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuipata tunzo hiyo,ilikwenda kwa Erika Badu,mwaka 2005 akachukua tunzo ya Grammy kama Best Urbun/Altenative R&B Perfomance kupitia mkono "Cross my mind",2001 aliachia mzigo "Expirience;Jill Scott 826+ halafu ikafuata "Beautiful Human;Words and Sounds Vol 2" mwaka 2004.

WITH AWARDS

Baada ya hapo Jill akaendelea kuandika sana mashairi,kwa mfano shairi lake kama "The Moments,The Minutes,The Hours" ambalo lilitolewa na St. Martins Press mwaka 2005.Mwaka 2007 Sept 25 akaachia mzigo mwingine "The Real Thing;Words and Sounds Vol 3 ambamo humo ndani kuna mkono unaitwa "Hate on Me",2008 akaachia albam yake ya pili ya live "Live in Paris" na ndani kuna mikono nane(8) ambayo ilirekodiwa wakati wa tuwa yake moja iliyobatizwa "Big Beautiful Tour".Kutokana na ushauri wa rafiki yake wa karibu director "Ozzie Jones" Jill alianza kujihusisha na masuala ya kuigiza filamu mwaka 2000 ambapo alijiunga na thieta(theatre) company moja huko Philadelphia ambapo alijifunza masuala ya uigizaji filamu.Mwaka 2004 aliigiza kama Donna katika season 4 ya series moja inaitwa "Girlfriends" na baadae ktk movie "Cavedwellers" akiwa na Kelvin Bacon na Kyra Sedgwick,2007 alitokea katika "Hounddog" kama Big Mama Thomton(itafute hii) na pia katika "Why Did I Get Married".2009 ametokea katika muendelezo wa "Why Did I Get Married" ambayo ni Pt II.Huyu ndio JILL SCOTT,i love this woman and i want u to lave her too,mtambue sasa.
BEAUTIFUL JILL SCOTT

0 comments: