BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Monday, May 31, 2010

ANTI-VIRUS WA KIRUSI CHA BONGO FLEVA HUYU HAPA...

SUGU aka MR II
Habari hizi mdau nimezipokea toka mapema siku ya jana,ni kwamba yule kirusi anayeendelea kumtafuna Bongo Fleva tayari ameshapatiwa dawa(antivirus),ni ukweli ulio wazi na ambao auhitaji hata darubini kuuona,kuwa Bongo Fleva now inaelekea kunako kaburi kwa kasi ya ajabu sana,na kinachoiua hii Bongo Fleva kipo kinajulikana na kinaonekana,sasa ma-legendari wa muziki huu wameamua kuitafutia game hii dawa ya kuhakikisha inarudi juu na suala la kifo chake kubaki kama sinema tu,wakiongozwa na SUGU aka MR II,kuna MKOLONI kutoka iliyokuwa WAGOSI WA KAYA,DOTTO wa MAPACHA,ZE DUDU,G-SOLO na wengineo wengi wameamua kutengeneza albams za bure kwa mtindo wa "mix tapes"(kutumia ala zilizokwishatumika) ambazo zitakwenda kwa mtindo wa VOLUMES na EPISODES ambazo zimebatizwa jina la "UNTI-VIRUS",kitakachofanyika ni kila Mc kuimba topic yake kwa kuwataja kwa majina halisi "MAFISADI" wanaoiua Bongo Fleva ili wapenzi wa muziki wajue na watambue kilichoko nyuma ya pazia katika muziki huu.

WAGOSI WA KAYA

Albams zote zitagawiwa bure bila gharama yoyote kwa yeyote atakaezitaka na kuwekwa katika mitandao mbalimbali ili yeyote aweze kuzi-download na kuzimiliki,na kwa kuanza washkaji wanaanza na "ANTI-VIRUS Vol 1" ambayo itakuwa na nyimbo kumi na sita(16) na baada ya hapo zitafuata zingine mpaka Vol 10 na kuendelea,haya wadau hizi ni harakati zingine baada ya "NGURUWE" ya ZE DUDU,tungoje tuone kama italeta mabadiliko yoyote katika game hili na kubadili upepo ambao kiukweli si mzuri ktk muziki huu kwa sasa.1 comments:

Anonymous said...

itakuwa poa sana wakifanya hvyo sababu bongo flava hii ina virus wakali sana duuuuuuuuuh!!!!!


big up ma man bizzo

zealot