BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, June 1, 2010

MAONI YA ZAVARA KUHUSU MARACAS MUSIC FESTIVAL 2010..


Habari zenu ndugu zangu.
Kwa waandaaji wa hili tamasha, naomba kuweka nasaha zangu ama kuleta changamoto kwenye mjadala huu.
Nilivyosikia Maracas mimi binafse hisia ya mwanzo kiukweli niliwaza ni jambo fulani lenye uhusiano na Marekani ya kusini. 
 Je Muaandaaji ni mtu wa huko ama?
 Kama ndio  je sisi tunaweza kumshawishi aweke jina la kiswahili ama la Kizaramo, hasa ukizingatia linafanyikia kwenye himaya ya WAZARAMO pale Bwagamoyo, hasa ukizingatia pale Bagamoyo kuna mzizi wa mila na desturi za kiswahili uliobobea sana.
Kama la. Sisi kama wadau wa sanaa na utamaduni tunaweza kumshauri muandaaji ama waandaaji kuangalia kanuni ya msingi kabisa ya kiutamaduni (UWAKILISHI).
Niliposoma ile orodha nimegundua kuwa asilimia 100 ya washiriki jukwaani ni wasanii wa hapa nyumbani.  
Je tukiangalia Biashara , kama ndo kigezo kilotumika.  Kwenye kanuni ya kibiashara na mauzo si ingekuwa vyema ukiwa na Bidhaa ya mahala fulani basi jina lake nalo liwakilishe hiyo bidhaa inakotoka?! Mfano magari ya Kijapani, tunayatambua tu kwa majina yake. Toyota, na pikipiki Honda na ya maeneo mengine  hali kadhalika.

Hebu tuangalie hili jambo kwa makini maana inawezekana ndugu waandaji kwa uwingi wa majukumu wanaweza kuwa hawakulipa uzityo uliostahili, mimi naongea kama mdau wa sanaa na wakati huo huo mlaji wa bidhaa hii. Hivyo nadhani nastahili kitu kilicho bora na ningekaa kimya nisingetumia haki yangu ya kimsingi kama mteja wa hawa walio andaa.

Nashauri kama kuna mtu anaweza kuusogeza huu mjadala pia kwa BASATA, ili tuwawajibishe nao pia maana kwa vyovyote waandaaji walipitia huko..Sasa BASATA inaonekana ama walipitiwa kwa hilo au wamekuwa wepesi wa kuokea ada za usajili na kuangalia vitu nyeti kama hivi vinawapita huku wakikenua na kutoa mikono ya kila la kheri kwa wahusika baada ya kupokea ada.

Miaka ya awali ya 1999 hadi 2001. Nilikuwa nikituma nyaraka mfululizo kwa taasisi inayoitwa Clouds entertaiment kama sikosei waliokuwa wakiandaa Summer Jam..Ilikuwa kichekesho ama kioja kuwa na jina la namna hii(walau mimi nliona hivyo) maana moja ya swali nilikuwa nikiwauliza ni kuwa wamesahau kuwa Dunia sio ubapa tena(kama mataifa ya magharibi walivyokuwa wakiamini awali, hadi Galileo alivyowabumburusha). Huwezi kuwa na msimu wa Kiangazi kizio cha kaskazini na cha kusini kwa wakati mmoja. Ilichukua muda hadi wao kuliona hilo lakini mwishoe walibadili na hili tamsha sasa linaitwa Fiesta.

Najaribu kuwaza kwa mchanganuo alioutoa nadhani ndugu Vitalis, basi ingekuwaje kama tungeita labda hili tamasha Zeze, ama Marimba na kutoa maelezo mazuri tu ya mahusiano yetu na Marimba(Nadhani ni neno la upande huu wa Afrika).  Jibu nnalopata kwa haraka haraka ni kwamba litaleta mvuto sana kulinganisha na Maracas. Asilimia kubwa watashindwa kutamka na watakaoweza basi kutakuwa na fungu kubwa la watakaokwazwa na tofauti ya R na L hivyo WENGI watasikika WAKIITA MALAKAZ.

Kutoweka kwa ari na msisimko wa UZALENDO unachangia sana kuzorota kwa uchumi (MJADALA MREFU SANA HUU), najua wachumi na wasomi wa sayansi ya jamii wanaweza wakawa na mitazamo tofauti ama inaweza kuleta mijadala mirefu sana lakini ukiangalia kiundani kuna ukweli.  Nisimalize wino hapa wakati kuna wengi watakaopenda kuchangia. Naomba nasaha zenu ndugu na jamaa zangu.
Mdogo wenu Zavara, enh yule yule wa Kwanza Unit, Harakati za UKOMBOZI wa mtu mweusi kwa njia ya Sanaa na mengineyo.

Kazi njema

0 comments: