BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, April 16, 2010

MY ALBUM OF THIS WEEK(NEW AMERYKAH PT 2 by ERIKAH BADU)

Haya!haya!haya!haya tena wadau na fans wa blog ya burudani(muziki na maisha),its another "furahi-day"(friday) kama kawa najua utakuwa unahamu ya kutaka kujua leo nimekuletea albam ya nani katika ile "segment" yetu ambayo ilianza wiki iliyopita ya "My Album of the Week",kama nilivyokuahidi hii itakuwa ndio kama bye bye ya kukutakia weekend njema kabla ya "kufunga shule" kwa wiki hii si ndiooo???sema NDIOOO!!!Leo niko na mwanadafada mkali wa SOUL MUSIC na ambaye mtindo wake wa maisha umekuwa ukiwashangaza wengi,si mwingine niiiiiiiiiiii!!!!!ERIKAH BADU!!na albam yake mpya kabisa inaitwa "NEW AMERYKAH PT 2(the Return of ANKH).Hii ni albam ya saba na ambayo mwanadada huyo ameiachia kitaa rasmi 30 March mwa huuhuu kwahiyo bado iko moto kabisa.Lakini hii ni part II ya albam yake ingine aliyoiachia February 26 2008 chini ya lebo ya MOTOWN iliyoitwa "NEW AMERYKAH PT 1(4th World War).

NEW AMERYKAH PT 1
Mwanadada kajifungua mtoto mzuri wa kike Feb 1 mwaka huu na ilim'bidi kurudi home kwao BROOKLYN na mwezi wa tatu tu akaachia mzigo huu,mzigo una ngoma 12 zilizoshiba sana katika Soul na Hiphop Soul,vichwa vilivyopiga mzigo huo katika suala zima la production ni yeye mwenyewe pamoja na washkaji wengine kibao kama 9th Wonder,James Poyser,Shafik Huseyn wa SA-RA Creative Patners,Taarak,J Dilla,Madllib na Karriem Riggims.Ndani utasikia mikono mikali kama "20 feet tall","Window seat","Agitation","Get Money","Dont be Long","Love","Fallin in Love" na mingine kibao.Akizungumzia maana ya neno "ANKH" kama alivyolitumia kwenye albam yake hii(The Return of Ankh) Erikah Badu ametanabaisha kuwa "ankh" ni neno la kiarabu lenye maana ya "internal life" kwahiyo kiujumla amesema albam hii imebeba ujumbe wa "mvutano mkali wa kiimani na kihisia za ndani kabisa za mtu"(spritual and emotional battle).Na mzigo huu uko katika nafasi ya tisa kwenye BILLBOARD TOP 200 ALBUM CHAT.
NEW AMERYKAH PT 2
Boyfriend wake wa sasa anaitwa Jay Electronica na ambaye ndio baba wa mtoto wake aliyemzaa Feb mwaka huu,Erikah ana watoto watatu hivi sasa na kila mtoto ana baba yake,baba wa mtoto wake wa pili ni Big Boy aliyekuwa memba wa OUTCAST na ambaye walipata bahati ya kufunga ndoa na baadae kutalikiana.Huyu ndo ERIKAH BADU banaaaa so chekicheki hii albam ikuburudishe weekend yote hii halafu mimi na wewe tukutane hapa jumatatu au vipiiiiii!!!WEEKEND NJEMA FANS!!!!!!!!

0 comments: