Vizazi vya Bongo Fleva ni ngumu sana kuyafahamu haya,na nimegundua kitu ambacho nataka ku-share nawe mdau wa blog hii ya burudani,hivi leo kuna baadhi ya ma'redio djs na watangazaji ambao wanajifanya wanaujua sana muziki huu wa KIZAZI KIPYA ,lakini kiukweli HAWAUJUI,nikijaribu kuwasikiliza kwa makini nagundua kuwa muziki wanaoujua ni muziki wa kuanzia miaka ya 2002 kuja mpaka hivi sasa,wanaujua muziki wa kuanzia enzi za hits za Bongo Records(P-Funk) kuja mpaka sasa,NIJUAVYO MIMI NI NGUMU KUKIJUA KITU VIZURI KAMA HUJUI KILIPOTOKEA,KILIPO NA KINAPOKWENDA,na huwezi kujua KILIPO na KINAPOKWENDA kama hujui kilipotokea.
Kwanza Unity Foundation Makanga,ML Chriss(Blue)&Abbass(Yellow)
Hao hapo juu ni Kwanza Unity(K.U Crew),moja kati ya makundi waasisi wa muziki wenu huu ambao leo mnauita Bongo Fleva na ambao karibu kila mtu sasa anajifanya anaujua sana,kundi hili lilikuwa linaundwa na washkaji kibao tu kama akina K-Single(Kibacha),Easy B,Nigga One(RIP),Rhymson(Zavara),D-Rob(RIP),Fresh G na wengineo na walianza michakato hii mwishoni kabisa mwa miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90 kipindi ambacho ndo "awamu ya kwanza" ya muziki huu wa kizazi kipya,kipindi ambacho tulikuwa tunaita "Swahili Rap".Na katika kipindi hiki ni makundi machache sana ndio yaliyokuwepo likiwamo hili la Kwanza Unity.Wengine walioweza kujitokeza katika awamu ya pili ambayo ilianza kwenye miaka ya 1994 ambapo muziki huu ulitambulika zaidi kama "BONGO HIPHOP ni G.W.M toka pande za Kurasini,Diplomats toka Sinza,The Hard Blasters,Cycle Tack,Dar Young Mobb,W.W.A,Mawingu Band(walikuwa wanaimba),Bad Skins,Mack Muga(Solo artist),Erick aka E-Atack(Solo artist)Sos B(Solo artist),II Proud(Solo Artist),Ras Pompidou(Solo artist),Saleh Jabir toka Znz(Solo artist)Jotwa Jokeri toka Mwanza(Solo artist),WEPWAA toka Mwanza pia na wengine kibao ambao siwezi kuwataja wote hapa.
Kwanza Unity Crew isipokuwa K-Singo na Samia X
Katika awamu hii ya kwanza ya muziki huu jamaa walifanikiwa kufanya albam moja "Kwanza Unity" ilokuwa na hit kama "amani" na zingine kibao tu,mwishoni mwa miaka ya 1994( awamu ya pili) ya muziki huu ambayo pia ndo ili-change jina kutoka "swahili rap" mpaka "Bongo Hiphop" ilikuja baada ya kuanza kwa vituo binafsi vya redio katika masafa mapya kwa wakati huo(masafa ya fm) na kidogo kuanza kutoa airtime ya nyimbo hizo wakati huo,Nakumbuka Radio One stereo(kipindi hicho ilikuwa 99.6fm now 89.5fm) ndo ilikuwa redio ya kwanza kwa hapa Dar na ilianza mwaka 1994 na kipindi cha kwanza cha vijana na kutoa airtime kwa nyimbo hizi kilikuwa ni Dj Show ya wakati huo na watangazaji walioanza kuzicheza nyimbo hizo ni Taji Liundi(Master T) na Mike Pesambili Mhagama.......
Mike Mhagama(kushoto) na Dj J4(kulia) 1997
Makala hii itaendelea wiki ijayo usikose....usikose kupitia blog ya burudani,comments zinahitajika..
0 comments:
Post a Comment