BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Monday, April 19, 2010

DRAKE "ANAVYOHARIBU" WATU WETU!!!

Inakuwaje wadau & fans wa blog yetu ya burudani??Weekend ilikuwaje??naamini ilikuwa bomba sana au sio??mi binafsi weekend yangu ilikuwa poa sana,ok!ni jumatatu ambayo nimekuja na hii ishu moja nzito ambayo naomba tuijadili kidogo,koz nimekaa nimejifikiria sana na nikaona sio ishu nikishea nanyi fans halafu tuone inakuwaje.

                                                                    DRAKE
Juzi jumamosi nilikuwa home katika yale mapumziko ya weekend, nikaona sio kesi ngoja leo nitoe muda wangu nisikilize vipindi vya Bongo Fleva katika redio mbalimbali,kama tujuavyo wabongo tulioko hapa nyumbani(Bongo) jumamosi ni siku ambayo karibu redio zote zinakuwa na vipindi vya Bongo Fleva kuanzia mapema sana asubuhi kwahiyo kwa msikilizaji kazi yake inakuwa ni ku-touch dial tu kubadilisha station moja kwenda ingine kuendelea kusikiliza fleva.Sasa wakati nasikiliza, kituo kimoja hivi kikawa kinatambulisha nyimbo mpya za wasanii zilizowafikia,hapo nikapata nafasi ya kusikiliza nyimbo nyingi tu ikiwamo wimbo mpya wa Moxie ambao ndo umenipelekea kutaka kushea nanyi hili jambo.
                                                                 MOXIE 
Moxie kaachia ngoma mpya baada ya "chupa nyingine" aliyoifanya pale Fish Crab kwa Lamar,hii ngoma mchizi kafanyia Kiumbe Records kwa producer mmoja anaitwa Masoud,ngoma ni kali mdau wangu lakini kupitia ngoma hii nimemfahamu MOX mwingine kabisa tofauti na yule nimjuae mimi,Mox huko ndani ame-rap kidogo sana na sehemu kubwa kaimba(amini usiamini).Kichwa cha habari cha waraka huu ni "DRAKE ANAVYOHARIBU WATU WETU",Drake ni rapper ambaye kwa sasa yuko hot ile mbaya na track zake kibao zimefanya na zinafanya vizuri mpaka sasa,but style yake ya kuimba ni MBAYA na INABOA(nionavyo mimi),Drake sio mwimbaji,ni rapper,kwahiyo anapoimba anakuwa hana "tuning" ya sauti,anaimba kwa sauti kama anayotumia pia ku-rap,cha zaidi ana-"melody" na always anakuwa "onkey".Kinachofanyika ili ku-sound vizuri kile ambacho Drake anafanya ni "outotuning".Outotune ni software fulani ambayo ikiwekwa katika voko za mwanamuziki baada ya kurekodi huweza kutia nakshi na kuiremba sauti ili iwe na mvuto zaidi kwa msikilizaji(mambo ya teknolojia).Sasa wasanii wa kibongo ambao tuliwazoea katika zile styles zilizokuwa zinaonesha "realskills" zao leo wanafanya kama Drake,kweli???kitu ambacho mi sidhani kama kuna mtu yeyote anaweza akashindwa kukifanya,kuimba just kuimba kwa sauti yako halafu producer akaku-"outotune" nani anashindwa??
                                        MIKE TEE
Mdau hicho ndicho Moxie amekifanya kwenye ngoma yake hii mpya,na nataka nikuambie kitu mdau,sio Moxie tu ambaye ametumbukia katika mkumbo huo,wako wengine pia,kama vipi tafuta ngoma ya sasa ya Mike Tee "i love you" halafu sikiliza koras na ngoma ya sasa ya J-Mo "i need some money" sikiliza koras pia.Ni hayo tu mdau na fans wangu,unless otherwise ngoma zote zimesimama na ziko tight sana.Ukishindwa ku-comment hapa tafadhali nicheki katika bizzo4shizzo@ymail.com.
                                         J-MO

0 comments: