BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, April 23, 2010

MY ALBUM OF THE WEEK(Elevated by J-MARTINS)

Mdau na fans wiki iliyopita nilipata nafasi ya kukumwagia uhondo unaopatikana katika albam ya mwanadada Erykah Badu iitwayo "New Amerykah pt II(the return of Ankh)",naamini hivi sasa albam hiyo itakuwa ktk library yako ndogo nyumbani(gheto) si ndio??Leo fans narudi home Afrika,na niko na mchizi ambaye hivi leo ana show pande za Rock City(Mwanza) pale VillaPack pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba,anaitwa J-Martins.Na nataka nikufahamishe kuwa hivi majuzi tu(mwezi uliopita) mchizi alikuwa na tour moja ndefu sana U.K.

                                                    J-MARTINS(ELAVATED)

Jamaa ni mwandishi na ni producer pia katika studio za Don Family Records jijini Lagos,na ame-produce albams zote za wadogo zake(si wa tumbo moja) P-Square,pia ame-produce mwenyewe albam yake hii,albam ya Bracket na albam zingine kibao,kwahiyo akaona sio kesi nae kaamua kufanya albam yake mwenyewe.J-Martins alianza kuachia ngoma ambayo iliwashtua wengi "Good or Bad" na ambayo ilianza kusikika hapa Bongo kabla ya kwingine kokote Afrika hii(kwenye show ya kwanza ya P-Square Bongo mwaka juzi),baadae akaachia hit ingine "Oyoyo" na now anafanya poa sana na "Iva".

                                 J-MARTINS (UK TOUR)

Albam ina mikono kumi iliyoshiba ambayo ni "Oyoyo","Iva","Believe","Jukpa"feat;Bracket,"Change",
"Tonight"feat;Phyno&Douglas na "Good or Bad"feat;Victor.Zingine ni "Chameleon"feat;IllBliss,Waje&Real Macoy,"Kudi"feat;Wyre toka Kenya na "So fly remix"feat;Victor,Muna&Jesse Jagz.Rasmi iliingia kitaa Nov 2 mwaka jana 2009.So hebu fanyafanya uicheki halafu unipe matokeoooo au sio???

0 comments: