BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Wednesday, April 21, 2010

RAPPER MWINGINE PIMP C AKUTWA AMEKUFA.

                                                          PIMP C
Baada ya jana blog ya burudani kuripoti juu ya kifo cha rapper mkongwe na memba wa kundi la Gangstarr GURU,leo blog hiihii ya burudani inaripoti juu ya kifo cha rapper mwingine PIMP C(pichani) ambae amekutwa amekufa  asubuhi ya leo kwenye chumba cha hotel aliyofikia,imeripotiwa kuwa mtu mmoja alipiga no 911 na L.A Country Fire kumkuta amelala juu ya kitanda chake akiwa tayari ameshakata roho.
PIMP C ambaye jina lake halisi ni Chad Batler alikuwa mmoja kati ya memba wawili wa bendi ya Hiphop ijulikanayo kama UGK,bendi ambayo ilijichukulia umaarufu sana baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Jay Z "Big Pimpin" mwaka 2000,mara ya mwisho walionekana kwenye video ya wimbo wa OutCast "International Player Anthem(i choose you)".
Perfomance ya mwisho ya mshkaji huyu ilikuwa pamoja na rapper mwingine Too Short na ilifanyika pale House of Blues L.A jumatatu ya wiki hii.R.I.P brother.

0 comments: