BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, July 29, 2010

ZINANIKUMBUSHA MBALI...."Age Ain't Nothing But A Number" By Aaliyah

AGE AIN'T NOTHING BUT A NUMBER

Hii ni segment mpya kabisa na itakuwa inakuja hapa kila alhamis kama ya leo hivi..hapa nitakuwa nakuchambulia albam moja ya kitambo ambayo mimi kiukweli nikiisikiliza inanikumbusha long-long time mazee....leo naanza na mzigo wa kwanza kabisa wa marehemu Aaliyah.."Age Ain't Nothing But A Number"..Mzigo huu ulidondoka rasmi kitaa mnamo June 13 1994 chini ya Jive na Blackgroung Records...hii ilikuwa ni baada ya kusainiwa na anko wake Barry Hankerson na kutambulishwa kwa mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki gwiji R-Kelly akiwa na miaka 12 tu na mchizi ndie aliyefanya kazi yote ya albam hii..mzigo una urefu wa dk 48 na sekunde 54(48:54) na ulianza kurekodiwa tangu sept 1993 mpaka May 1994 wakati huo Aaliyah akiwa na umri wa miaka 14 tu...Mzigo ulikuwa na hit kama "Back & Forth" na "@ your best(you are love)" ambazo zilichukua gold award toka Recording Industry Association of America(RIAA) na baadae zikafuatiwa na hit kama "Age Ain't Nothing" wenyewe na "No One Knows How To Love"...Mzigo huu kwa taarifa yako mdau ulifikia mpaka nafasi ya 18 kwenye Billboards Top 200 Albums na kuuzwa zaidi ya nakala milioni mbili kwa Marekani tu...kama huna ama bado hujausikiliza hebu fanya kuutafuta..ni mkali sana na mimi binafsi huwa sichoki kuusikiliza aisii...unanikumbusha mbali sana..

0 comments: