TEFLON DON(COVER)
"Teflon Don" ni zaidi ya jina lake kama albam ya nne ya mchizi kutoka Def Jam William Leonard Roberts II aka Rick Ross,ni jina lenye heshima la albam ya mchizi aliyetaabika mbaya na kuongoza kwa muda mrefu sana kitu yaitwa Miami's Undergroung Rap Scene enzi hizo..na baadae kuibuka na kufanya kweli na albums tatu za kwanza ambazo ni "Port of Miami"(2006), "Trilla"(2008) na "Deeper than Rap"(2009)..July 23 ndio mzigo huu mpya mchizi akauachia kitaa..singo ya kwanza ilikuwa "Super high" akiwa na Ne-yo ambayo imefanywa na producer anaitwa Dj Clark Kent toka J.U.S.T.I.C.E league..wengine waliotia mikono ni The Runners,The Inkredibles ambao wote waligonga kwenye "Deeper Than Rap" na the Olympics.
DEEPER THAN RAP(COVER)
Ndani ya "Teflon Don" kuna mikono minene 11 ambayo ni "I'm not a star", "Free Manson", "Tears of joy", "Maybach music III", "Live fast Die young", "Super high", "No 1", "Mc Hummer", "B.M.F(Blowing Money Fast)", "Aston Martin Music" na "All the money in the world".Mzigo huu unatishia maisha ya mzigo mwingine mkali wa Eminem "Recovery" huko kunako soko....so inabidi tusikilizie tuone...hii ndio "Teflon Don" ya Rick Ross kaitafute...
0 comments:
Post a Comment