BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, July 30, 2010

OLD SKOOL...."HORACE BROWN"

HORACE BROWN

Ndoto yake kubwa wakati anakuwa ilikuwa ni kuja kuwa mcheza mpira wa kikapu maarufu NBA..lakini ndoto hiyo ikaja kuyeyuka baada ya kuumia mguu alipokuwa in court..Huyu si mwingine ni mchizi anaitwa Horace Brown..ambaye alizaliwa huko Charlotte,North Carolina,US...amekulia kanisani na hata muziki pia alianza kuimba kanisani...DeVante Swing wa Jodeci alipata kuisikia demo ya jamaa akamkubali..then akamtafutia vi-dili vya kuwa backvocalist wa Christopher Williams na Terri & Monica..hiyo ikampa nafasi ya kuonwa na rais wa Uptown Records Andre Harrel,akasainishwa mkataba pale..1994 mchizi akaachia singo yake ya kwanza kabisa "Taste your Love" ambayo ilitamba sana South..lakini ikabuma kwenye chat zinazoaminiwa..baadae Andre Harrel akahamia Motown Records,akahama nae,huko akaachia singo zingine mbili katika kuipromoti albam yake "Horace Brown" na 1996 ikaingia kitaani rasmi,humo kuna mashavu ya Diddy(Puffy Daddy),Faith Evans,Fox Brown na Jay Z..2007 akatokea kwenye albam ya mwanamuziki wa R&B wa kijerumani Lisha "Nice To Meet you" katika mkono "I want that"...Huyu ndo Horace Brown.

0 comments: