BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, September 16, 2010

HALI YA KIDBWOY WA TETEMESHA RECORDS NA R.F.A NI TETE..

KIDBWOY

Habari zilizonishtua na kuniharibia kabisa siku yangu leo ni hizi...KidBwoy..mtangazaji wa Radio Free Afrika na mmiliki na mtayarishaji muziki katika studio za TETEMESHA RECORDS amevamiwa kwake jana na mtu anayesemekana kuwa ni msanii na kumjeruhi vibaya....ifuatayo ni sms toka kwa mtangazaji na mshikaji wake wa karibu Fredrick Bundala(SkyWoka)..."Kid amevamiwa jana kwake mida ya jioni na mtu anayedhaniwa kuwa ni msanii, amemjuruhi vibaya kwa kumchoma na bisibisi maskioni na kumpiga na kitu kizito kichwani, yuko Bugando Hospital wodi namba C 603 ghorofa ya 6, hali yake si nzuri sana..."...Jamani muziki wetu umefika hapa kweli????Kid get well soon bro...twakuombea,soon utakuwa sawa na kuendelea na kile ukifanyacho kila siku,hii ni kwa niaba ya MNM.

0 comments: