BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, September 23, 2010

KIDBWOY AENDELEA VZR..AHAMISHWA WODI..

KIDBWOY

Wadau na fans wengi walitaka kujua mchizi anaendeleaje..baada ya kuripotiwa kuvamiwa na kuumizwa vibaya na mtu asiyefahamika anayesadikiwa kuwa ni msanii....Mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa TETEMESHA Records ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Free Africa ya Mwanza Sandu George Mpanda al-maarufu kama KidBwoy kwa sasa hali yake inaendelea vzr..ameweza kuzinduka na kuzungumza japo kidogo baada ya kuwa nusu kaputi kwa zaidi ya masaa 15 baada ya tukio...ila habari mpya zinasema mshkaji imebidi ahamishwe wodi ili kuhepuka usumbufu wa fans kibao ambao daily walikuwa wanajitokeza hospitali ya Bugando alikolazwa kwa nia ya kumjulia hali na kutaka kupigapiga nae stori ishu ambayo madaktari wake wamesema si salama sana kwa sasa coz anahitaji mapumziko zaidi...awali alikuwa wodi no C 606 ghorofa ya sita...kwa sasa amehamishiwa wodi ambayo bado haijawekwa wazi ili apate mapumziko na kuharakisha kupona kwake...Get Well Soon Kid.

0 comments: