BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, October 7, 2010

MAONI YA MDAU TAJI LIUNDI BAADA YA "BLACK SUNDAY" PREMIER..

BLACK SUNDAY(COVER)


Nilipewa DVD ya kuangalia kabla ya filamu kuzinduliwa na watengenezaji nikiwa ni rafiki na mshirika wao katika mambo kadhaa.
Nilisikitika mara tu nilipoanza na kujikuta naangalia filamu ambayo dhahiri ilik...uwa imeigwa. Kadri filamu ilivyoendelea, nilishtushwa na hadithi, maudhui na hata tamati. Vyote kwa sehemu kubwa vilitokana na filamu ya mwaka 2007 iliyotengenezwa Canada inaitwa BUTTERFLY ON A WHEEL.
(ANGALIENI PROFILE WALL KUONA TRAILER ZA FILAMU HIZI MBILI)
BUTTERFLY ON A WHEEL ni sawa na kusema KIPEPEO KWENYE GURUDUMU. Kama kweli unataka kumkanyaga kipepeo, basi gurudumu ni kitu kikubwa sana. Mantiki ni jina hilo ni sawa na kusema kwamba, 'jitihada kubwa mno inatumika kutimiza swala dogo sana"
Ndivyo zilivyo hadithi zote mbili. Mtekaji anatumia mbinu na kila jitihada kuwabughudhi wapenzi wawili kutwa, kwa sababu ambayo inabainika kuwa ndogo lakini nyeti. Ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
Black Sunday ina mapungufu mengi sana.Imeigwa.
Haina uhalisia, hata kama ni filamu ya kubuni. Kanumba kwa mfano anaonyesha bastola waziwazi, anawapa wahanga wake nafasi nyingi za kutoroka na labda kubuni mbinu za kumzidi.
Haiwezekani kutoa Shilingi 50+milioni siku ya Jumapili bila benki yeyote (Pilipili Bank?) kutaka kujua kwanini au kukudadisi kwa undani?i!Jinsi ya mtoto katika filamu inajichanganya!Mara binti, mara mvulana???
PLOT: haina nguvu, si ajabu kwani imeigwa na kuleta uhalisia wa Tanzania iliwashinda waandaaji.
Mf.Mlela na Yvonne hawana hata sumni mfukoni, lakini wanapotumwa kuombaomba hela, wanaonekana kufika hadi MJINI kutoka Giraffe Ocean View Hotel! Labda Mrwanda hataelewa sawa...
Uigizaji wa Kanumba sio mzuri. Anavituko vya "kitoto' sijui niseme? Kugonganisha meno, kula Big G na kuifanya iwe kama kitu cha msingi sana. Kiujumla SCRIPT yake ni mbaya. Hasemi lolote la maana kwa robo tatu ya filamu.Kuna umihimu wa kukubali STRONG CHARACTERS siku nyingine.
Mlela na Yvonne hawapati nafasi ya kuzungumza wala kuigiza haswa kwa zaidi ya robo tatu ya filamu nzima.Hata hivyo, filamu inaisha na matukio ya kushangaza akili za mtu mwerevu!
Hakuna utaalamu wa taa, SPECIAL EFFECTS, na LOCATION au utafutaji wa maeneo ulikuwa finyu sana!
Sijaelewa waandaaji wanawaza nini? Sifahamu kama waigizaji walifahamu kwamba walikua wanatoa kopi. Hawajajibu maswali yangu niliyotuma kabla ya kuandika haya.
Nashindwa kuzipenda sana kazi za nyumbani. Umakini, ubunifu na utungaji hadithi zenye kina unatuangusha.
Kitu kizito zaidi ni SOKO. Mlimani pale wanaenda watu wa tabaka la juu kuangalia kwa mfano INCEPTION. Matarajio yao ni kuangalia filamu za kiwango cha juu sana. Wanaweza kila wiki kuingia kuangalia filamu kwa Tsh 8.000-15 elfu!Kama panajiendesha na soko hilo tu peke yake, je kama rafiki yangu Kanumba angeweza kujitahidi kufikia viwango vya kukubalika na soko hili? Si angefaidika sana?
Soko la KWELI sio la VIDEO ni la MAJUMBA YA CINEMA. Uuuzaji wa video ni BAADAYE kabisa.Lakini hili ni somo la siku nyingine...Haya, nimenena. Ni matarajoio yangu kwamba wengi mtaona nimekuwa mkali kwenye maoni. Nimekuwa mkweli. Kama hukwenda kuiona, ione kwanza au inunue kisha pitia upya niliyoandika. Kwa wasanii husika, msinichukie, msichukie niliyoandika, hebu chukulieni maneno haya kwa fikra chanya.Naamini sisi ni marafiki na rafiki mwema ni yule ambaye haogopi kusema ukweli. Ukweli unauma. Ukweli unajenga.Naandika kuwafumbua macho na kuwatakia maendeleo. Hakuna fani yenye kukosolewa zaidi kama FILAMU. Nipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi katika mawazo. Natumaini waungwana wengine wataandika maoni yao nao.
Kila la kheri.
TajiSee More


Tuesday at 2:02pm · LikeUnlike

0 comments: