BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, July 6, 2010

MY CRAIZY BET 2010 SHOW....EMINEM'S...& ALICIA KEY'S


Mdau ilikuwa ni bonge-bonge moja la show,kwa ujumla kwa yule aliyekuwa makini na kuitizama mwanzo mwisho BET Awards 2010 hatanipinga kwa hiki ninachosema,nimekuwa nikiangalia awards za BET kwa miaka kama sita hivi mfululizo lakini hii ya mwaka huu...dah!!!!..show ilianza kama saa mbili usiku kwa saa za huku kwetu..but ilianza BET Awards pre-show nje ambayo ilifanyika nje ya ukumbi ambao show ilipigwa,vilifanyika vitu vingi ikiwa ni pamoja na perfomances kutoka kwa wasanii ambao hawakuwa nominees kwenye awards hizo...pamoja na upitaji na upigaji picha katika RED CARPET na vitu ka' hizo,hosts walikuwa ni Tarrance na Rocsie ambao huwa wanafanya kipindi cha 106 & Pack na mtu mzima Nick Canon...


 Kama nilivyosema kwa ujumla awards zilikuwa poa ile mbaya ila katika show zote,show iliyonivutia mimi binafsi ni ya mtu mzima Eminem,dahhhh!!!!jamaa alipiga bonge-bonge moja ya show..si kitoto..Alicia Keys pia alifanya vizuri sana japo ali-perfom na ujauzito mkubwa tu.. so naweza kusema ni mtu wa pili kwangu ambaye niliipenda zaidi show yake..mi nadhani wadau na waandaaji wa tunzo zetu hapa bongo wajitahidi kuwa wanafuatilia na kutazama awards za wenzetu ili kuona cha kujifunza na kuboresha awards zetu hapa..ni hayo tu mdau wangu..

0 comments: