BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, September 3, 2010

7 YEARZ AGO..SENGEREMA MWANZA..(CHOKA MBAYA RECORDS)

DAW MAJUKANO&RENATUS KILUVIA

Nimeona sio vibaya nikishea nanyi fans wangu..asb ya leo nimepokea simu toka kwa mshkaji wng wa ukweli sana Daw Majukano na kunipa taarifa zilizonishangaza sana...eti blog tuliyoifungua miaka nane iliyopita bado iko hewani mpk leo hii..duh!!Kweli bana..nilipoi-google nikafanikiwa kuifungua na kuiona...aisiii!!kiukweli nimekumbuka mbali sana mdau..hii ilikuwa ni blog ya kuitangaza studio yetu ya kwanza kabisa "Choka Mbaya Records" ambayo tuliifungua na kuanza kufanya kazi ya recording mwaka 2002 Sengerema Mwanza wkt huo tukiwa watangazaji wa kituo cha redio 98.8 fm cha wilayani humo...baadae tulihamisha studio jijini Mwanza na kubadili jina toka Choka Mbaya na kuwa Stonetown Records, halafu Zanzibar(Stonetown I) na Shinyanga(Stonetown II) na mwisho zikaungana mwaka 2007 Kinondoni Dar es Salaam.

STONETOWN RECORDS

Ni safari ndefu ambayo sitakaa niisahau kamwe katika maisha...hapa chini nakuwekea baadhi ya posts tulizoweka kujitambulisha ktk blog hiyo....
"Maelezo kidogo kuhusiana na Studio za CHOKAMBAYA

Choka mbaya records ilibuniwa mwaka 2000. lakini ilianzishwa rasmi mwaka 2003--- december chini ya ma-deejayz wawili ambao ni David james majukano. a.k.a deejay daw na mwenzie Renatus Albinus kiluvia a.k.a rennie bizzo wote wakazi wa jijini Mwanza Tanzania East afrika.CHOKAMBAYA RECORDS ni Studio ya kurekodi muziki aina zote. Neno "chokambaya" linamaanisha kuchoka vibaya( so tired records) hehehehehehe!!! alisema rennie bizzo!! nia na madhumuni ya kuanzisha STUDIO hii na kuisimika jijini mwanza ni kuinua vipaji vya;WASANII chipukuzi wa muziki mbalimbali. kama..HIP-HOP,R&b;b,ZOUK, REGGAE NYIMBO ZA DINI;NYIMBO ZA KITAMADUNI (TRDITIONAL; MUSIC) NK!!! CHOKA MABYA RECORDS ni Studio pekee iliyoko maeneo ya Sengerema na inawakilisha maeneo mbalimbali kwa mfano Geita, mpaka Ngara !!! Dee-jay Daw ni mtangazaji wa radio vilevile ni "PRODUCER" wa "CHOKAMBAYA RECORDS" Rennie Bizzo nae ni mtangazaji na pia ni PRODUCER" ndani ya "CHOKAMBAYA RECORDS"
                      
                    WASANII WOTE MNAKARIBISHWA!!


"Kama wewe ni msanii wa maigizo,muziki wa aina yoyote basi kuwa huru kuwasiliana na sisi .kwa msanii anae toka mbali kidogo na maeneo ya sengerema yaani kwa mfano mwanza city kuja kwetu kurecord atarudishiwa ghalama zake za usafiri na huwa tunawapa kipau mbele sana wansanii kutoka mbali"

Link yenyewe ni http://www.chokambayarecords.8m.com/

0 comments: