BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, September 2, 2010

MABIBI NA MABWANA..NAMLETA KWENU..JANE MISO.

JANE MISO


Baada ya kutamba na album yake ya kwanza "OMOYO" aliyoimba kwa lugha ya kisukuma ktk baadhi ya nyimbo, sasa anakaribia kupakua "UINULIWE" yenye nyimbo maalumu za kuuombea uchaguzi mkuu wa Oct 31 mwaka huu,ambao awali alipanga kuizindua albam yake aliyokuwa akiitengeneza kwa muda mrefu "MOTEMA" yenye mahadhi ya Lingala yenye nyimbo sita ambayo sasa itazinduliwa wakati mwingine. Kwa sasa yuko tayari kuileta kwenu (audio na video) "UINULIWE" Sept 19 katika ukumbi wa Diamond Jubilee na maandalizi yote yamekwisha kamilika ambapo ataisambaza punde atakapomaliza uzinduzi huo ambao pia utapambwa na wahudumu wengine wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

0 comments: