BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Monday, September 6, 2010

TANGU JANA TAR 06..


Hii mdau imeanza jana kule Arusha...

Arusha International Cultural Diversity Festival (AICDF) 2nd Edition, As planned, this festival will take at three vanues: Alliance Francaise Arusha, WHAT at gallery masai café, Viavia cultural cafe/natural history museum from 6th to 12th Sept 2010.

The main theme of the festival is acknowledging, appreciating, valuing differences and celebrating culture and diversity.
This is a great opportunity for you to explore Arusha and to discover it’s beauty and diversity…huu ulikuwa mualiko wangu but sijapata nafasi ya kuhudhuria...thanx kwa consideration wadau..

VOTE FOR ZUBERI KABWE ZITTO KIGOMA KASKAZINI...

Friday, September 3, 2010

7 YEARZ AGO..SENGEREMA MWANZA..(CHOKA MBAYA RECORDS)

DAW MAJUKANO&RENATUS KILUVIA

Nimeona sio vibaya nikishea nanyi fans wangu..asb ya leo nimepokea simu toka kwa mshkaji wng wa ukweli sana Daw Majukano na kunipa taarifa zilizonishangaza sana...eti blog tuliyoifungua miaka nane iliyopita bado iko hewani mpk leo hii..duh!!Kweli bana..nilipoi-google nikafanikiwa kuifungua na kuiona...aisiii!!kiukweli nimekumbuka mbali sana mdau..hii ilikuwa ni blog ya kuitangaza studio yetu ya kwanza kabisa "Choka Mbaya Records" ambayo tuliifungua na kuanza kufanya kazi ya recording mwaka 2002 Sengerema Mwanza wkt huo tukiwa watangazaji wa kituo cha redio 98.8 fm cha wilayani humo...baadae tulihamisha studio jijini Mwanza na kubadili jina toka Choka Mbaya na kuwa Stonetown Records, halafu Zanzibar(Stonetown I) na Shinyanga(Stonetown II) na mwisho zikaungana mwaka 2007 Kinondoni Dar es Salaam.

STONETOWN RECORDS

Ni safari ndefu ambayo sitakaa niisahau kamwe katika maisha...hapa chini nakuwekea baadhi ya posts tulizoweka kujitambulisha ktk blog hiyo....
"Maelezo kidogo kuhusiana na Studio za CHOKAMBAYA

Choka mbaya records ilibuniwa mwaka 2000. lakini ilianzishwa rasmi mwaka 2003--- december chini ya ma-deejayz wawili ambao ni David james majukano. a.k.a deejay daw na mwenzie Renatus Albinus kiluvia a.k.a rennie bizzo wote wakazi wa jijini Mwanza Tanzania East afrika.CHOKAMBAYA RECORDS ni Studio ya kurekodi muziki aina zote. Neno "chokambaya" linamaanisha kuchoka vibaya( so tired records) hehehehehehe!!! alisema rennie bizzo!! nia na madhumuni ya kuanzisha STUDIO hii na kuisimika jijini mwanza ni kuinua vipaji vya;WASANII chipukuzi wa muziki mbalimbali. kama..HIP-HOP,R&b;b,ZOUK, REGGAE NYIMBO ZA DINI;NYIMBO ZA KITAMADUNI (TRDITIONAL; MUSIC) NK!!! CHOKA MABYA RECORDS ni Studio pekee iliyoko maeneo ya Sengerema na inawakilisha maeneo mbalimbali kwa mfano Geita, mpaka Ngara !!! Dee-jay Daw ni mtangazaji wa radio vilevile ni "PRODUCER" wa "CHOKAMBAYA RECORDS" Rennie Bizzo nae ni mtangazaji na pia ni PRODUCER" ndani ya "CHOKAMBAYA RECORDS"
                      
                    WASANII WOTE MNAKARIBISHWA!!


"Kama wewe ni msanii wa maigizo,muziki wa aina yoyote basi kuwa huru kuwasiliana na sisi .kwa msanii anae toka mbali kidogo na maeneo ya sengerema yaani kwa mfano mwanza city kuja kwetu kurecord atarudishiwa ghalama zake za usafiri na huwa tunawapa kipau mbele sana wansanii kutoka mbali"

Link yenyewe ni http://www.chokambayarecords.8m.com/

Thursday, September 2, 2010

MKOLONI WA WAGOSI KTK HALI TETE...

DK JOHN NA MKOLONI

Mdau na fan wangu,hii nimeinasa hivi punde japo imewekwa kitambo kama cha masaa 19 yaliyopita katika Facebook na mwandishi wa habari za burudani toka Mwananchi Communication na mtangazaji wa kipindi kipya cha "kituo cha kazi" 100.5 Times fm Henry Mdimu..imesomeka kama hivi..
"BREAKING NEWS: Mshkaji wetu Fred Mariki, a.k.a Mkoloni wa kundi la wagosi wa Kaya, ambaye ni producer wa kipindi cha kituo cha kazi, amezimika baada ya kunywa supu inayodaiwa kuwa na madawa, na amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako amepumzishwa, tusaidiane kumuombea ili arudi katika uzima wake,na mambo yawe hewani kama kawaida..."
Hii imetokea Meeda BAR Sinza,tuungane pamoja tumuombee arejee barabarani soon.

MABIBI NA MABWANA..NAMLETA KWENU..JANE MISO.

JANE MISO


Baada ya kutamba na album yake ya kwanza "OMOYO" aliyoimba kwa lugha ya kisukuma ktk baadhi ya nyimbo, sasa anakaribia kupakua "UINULIWE" yenye nyimbo maalumu za kuuombea uchaguzi mkuu wa Oct 31 mwaka huu,ambao awali alipanga kuizindua albam yake aliyokuwa akiitengeneza kwa muda mrefu "MOTEMA" yenye mahadhi ya Lingala yenye nyimbo sita ambayo sasa itazinduliwa wakati mwingine. Kwa sasa yuko tayari kuileta kwenu (audio na video) "UINULIWE" Sept 19 katika ukumbi wa Diamond Jubilee na maandalizi yote yamekwisha kamilika ambapo ataisambaza punde atakapomaliza uzinduzi huo ambao pia utapambwa na wahudumu wengine wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Wednesday, September 1, 2010

DIDDY AKUBALI MATOKEO......

SEAN PUFFY COMBS

Rappa the "big name" anaye-own Bad Boys Ent Sean Puffy Combs aka Diddy amekubali matokeo na kumtumia salamu za pongezi rappa aliye-"make headlines" za mitandao kibao juzi kati baada ya kuripotiwa kuwa ndie anayeongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu aka mapene aka pesa Sean Cutter aka Jay Z,wachambuzi wa masuala ya watu maarufu aka wadaku wamesema huo ni uungwana na ni kuonesha ni jinsi gani mchizi amekuwa mtu mzima sasa..hiyo ndio mambo...

SEAN CUTTER